Chama cha CHADEMA kimeelemewa kwa salaam za Pongezi kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi kutokana na uchaguzi mkuu wa kihistoria uliyomrejesha madarakani Freeman Mbowe.
Salaam za Karibuni ni kutoka kwa Chama cha ACT Wazalendo mshirika wa Chadema katika upinzani.
Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amempongeza Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kwa kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa kura nyingi.
Zitto Kabwe amepongeza pia viongozi wengine waliochaguliwa na jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa kwa njia ya kidemokrasia.
"Nakupongeza ndg. Freeman Mbowe kwa kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa. Nawapongeza wana CHADEMA kwa kumaliza Mkutano Mkuu wa Chama chenu na kuchagua safu ya Uongozi kwa miaka mitano ijayo. Tushirikiane kuweka mikakati ya pamoja kuhami demokrasia yetu" - Zitto Kabwe