Zitto Kabwe ameongea vizuri; wahafidhina ndani ya CCM wamuache Rais Samia atekeleze maono yake

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,598
3,671
Nilipenda maelezo ya ZZK Kiongozi wa ACT katika Kikao cha Kamati Kuu ya chama chake iliyofanyika Zanzibar jana tarehe 08 Agosti, 2021. Alirejea ukweli kuwa Rais Samia alianza vema sana uongozi wake baada ya kifo cha JPM. Hata hivyo kwa siku za karibuni kuna kila dalili ametishwa na kundi la mahafidhina na mahayawani ndani ya Serikali na CCM ambayo yalifaidika sana utawala wa kipuuzi wa JPM.

Kundi hili linahusisha viongozi wa Polisi na baadhi ya wakuu wa TISS ambao hufanya assessment ya usalama hapa Nchini. Wameandaa taarifa za uwongo na kutisha hivyo kumuogofya SSH. Kundi hili la kina Sirro na wenzake walifaidi sana pesa za wizi wakati wa JPM kwa kisingizio cha mulenda usalama na kunyanyasa wapinzani. Fedha hizo hazikuwa na uwajibikaji maana JPM alipenda kudanganywa hasa katika masuala ya usalama na ukandamizaji wa wapinzani.

Miezi 3 ya mwanzo ya Utawala wa SSH kundi hili hawakupata fedha. Wanatumia kilio cha mabadiliko ya Katiba kutafuta haki ya kula fedha kama wakati wa JPM. Wanatumia jinsia ya SSH kumjengea hofu ashindwe kutawala kwa amani. Namuomba sana SSH Mungu amsaidie awe imara. Ndugu zangu Uongozi wa Nchi patika nafasi ya Rais sio kazi ndogo na hasa ukiwa mwanamke katika Nchi yenye tamaduni zetu.

Tumuombee sana SSH Mungu ampe akili ya kuishi maono yake. Hawa akina Sirro, Mwigulu, baadhi ya wakuu wa TISS. wahafidhina wa CCM waliofaidika na JPM, baadhi ya viongozi wa Dini na wengi Serikalini waliokula kwa JPM bila kunawa hawana nia ya kumsaidia.
 
Hawa wako mpaka mahakamani...

Yaani wameshikilia na kui - control mihimili yote ya dola
å Serikali/utawala (executive) kupitia idara nyeti mbili TISS na Polisi
å Bungeni
å Mahamakani

The whole issue huwa inaanzia polisi, wanakutengenezea zengwe, wanakubambikizia kesi hatari...

Wanakupeleka mahakamani na huko utakukutana na mahakimu/majaji wao ambao kazi yao ni ku - certify mashitaka hayo ya uongo. Na watasema "....kwa mujibu wa sheria nakuhukumu kwenda jela miaka..."

Hivi ndivyo tawala za kidikteta uchwara hu - operate mambo yao kwa wanaowaona kikwazo/wanakwamisha mambo yao...

Mambo huwa extremely mabaya sana kama na jeshi la nchi (JWTZ) linajikuta limetekwa na mafia walafi wa madaraka hawa...

Lakini kama siyo, mkombozi wa wananchi hubaki kuwa Jeshi la Wananchi maana huwa likiona mambo ya nchi yanaharibika ndipo haamua kuichukua nchi na ndipo tunasema "...Rais fulani kapinduliwa..."

Tuombe tusifike huko...

Tumwombee Rais neema ya kuwatambua watu hawa waovu wenye nia mbaya na kuchukua hatua haraka...

Otherwise ni kilio chake na wananchi pia...
 
Kipindi cha utawala wa magufuli Polisiccm na task force walitumia fursa ile kuwabambikia kodi kubwa kesi wafanyabiashara na wapinzani kuwafungia Account biashara zao kienyeji, kuwapa kesi za uhujumu uchumi na mambo mengi ya hovyo ambayo yalizalisha mianya mingi ya Rushwa na wao kujinufaisha kutajirika kupitia uonevu unyanyasaji wa magufuli kwa wapinzani na wafanyabiashara , baada ya mama kuingia ikulu akaanza vizuri kwa kukemea unyanyasaji mateso kwa wapinzani wakawa wamekosa pa kubambikia kesi kwenda kuwapekua kuwawekea ushahidi feki ndipo sasa wameamua kumshawishi mama awe dikiteta wapate kutumia fursa hizo kupiga pesa za oparation tokomeza upinzani, wanabuni miradi haramu ya kuvuna pesa za walipa kodi kwa njia haramu za kishetani
 
Hawa wako mpaka mahakamani...

Yaani wameshikilia na kui - control mihimili yote ya dola
å Serikali/utawala (executive) kupitia idara nyeti mbili TISS na Polisi
å Bungeni
å Mahamakani

The whole issue huwa inaanzia polisi, wanakutengenezea zengwe, wanakubambikizia kesi hatari...

Wanakupeleka mahakamani na huko utakukutana na mahakimu/majaji wao ambao kazi yao ni ku - certify mashitaka hayo ya uongo. Na watasema "....kwa mujibu wa sheria nakuhukumu kwenda jela miaka..."

Hivi ndivyo tawala za kidikteta uchwara hu - operate mambo yao kwa wanaowaona kikwazo/wanakwamisha mambo yao...

Mambo huwa extremely mabaya sana kama na jeshi la nchi (JWTZ) linajikuta limetekwa na mafia walafi wa madaraka hawa...

Lakini kama siyo, mkombozi wa wananchi hubaki kuwa Jeshi la Wananchi maana huwa likiona mambo ya nchi yanaharibika ndipo haamua kuichukua nchi na ndipo tunasema "...Rais fulani kapinduliwa..."

Tuombe tusifike huko...

Tumwombee Rais neema ya kuwatambua watu hawa waovu wenye nia mbaya na kuchukua hatua haraka...

Otherwise ni kilio chake na wananchi pia...
Kuwapekua wapinzani huwa ni fursa za Polisiccm kutengeneza mazingira ya Rushwa kwa hukamata watu hovyo hovyo ambao huwaachia baada ya kutoa Rushwa, hii Tabia mbovu ya Polisiccm kwenda kukamata wapinzani usiku wa manane kana kwamba ni Nchi yenye vita kama Somalia wanaitoa wapi?
 
Sasa ukidai katiba mpya unakuja kupekuliwa kwako itabidi wanasiasa waanze kuishi guest house ili wakienda kuwapekua wapekue guest house waache kudhalilisha familia za wapinzani
 
Acha lawama zielekezwe zinapostahili kuelekezwa.

Usitafute kupindisha mambo na kuchanganya watu ukidhani watu hao hawana uwezo wa kuangalia na kupambanua ni nani mhusika wa yote yanayotokea nchini.

Hata kama 'Maza Mizinguo' anakubali kupotoshwa kama unavyotaka watu waamini, basi hafai kuwa hapo alipo. Kupotoshwa huko hakuwezi kumpa unafuu wowote juu ya makosa yanayojitokeza ndani ya utawala wake.
 
Lakini kama siyo, mkombozi wa wananchi hubaki kuwa Jeshi la Wananchi maana huwa likiona mambo ya nchi yanaharibika ndipo haamua kuichukua nchi na ndipo tunasema "...Rais fulani kapinduliwa..."

Tuombe tusifike huko...
Sijui kama Tanzania tuliwahi kuwa na wazo la kufika huko; lakini sishangai kamwe kama kuna watu "wanaombea tufike huko" nyakati hizi!

Nchi haina matumaini tena.
 
Awamu ya tano TISS na Polisi walikuwa na fungu maalum la kufatilia mienendo ya ABDUL NONDO. Hivi kweli mtu kama Abdul Nondo ni tishio kwa hili taifa? Wizi mtupu wa kodi za wananchi.

Wengine walikuwa na fungu maalum kufatilia simu za Nape na Kinana bila kumsahau January.

Mungu lisaidie hili Taifa.
 
2848495_6B17CC8F-440B-4DEB-8E31-39E80AD09F6A.jpeg
 
Awamu ya tano TISS na Polisi walikuwa na fungu maalum la kufatilia mienendo ya ABDUL NONDO. Hivi kweli mtu kama Abdul Nondo ni tishio kwa hili taifa? Wizi mtupu wa kodi za wananchi.

Wengine walikuwa na fungu maalum kufatilia simu za Nape na Kinana bila kumsahau January.

Mungu lisaidie hili Taifa.
Kulikuwa na matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi
 
Back
Top Bottom