Zitto Kabwe ameanza Ziara Majimbo ya Pemba

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
520
1,000
Leo Kiongozi wa Chama, Ndugu Zitto Kabwe ameanza Ziara ya Kichama katika majimbo yote ya Pemba. Katika ziara hiyo ameambatana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu, Mheshimiwa Othman Masoud Othman. Katika ziara pia yupo Katibu Mkuu wa Chama, Ndugu Ado Shaibu na Makamu Mwenyekiti wa Chama Zanzibar, Ndugu Juma Duni Haji.

Madhumuni ya ziara ni kuwaeleza Wapenzi, Wanachama na Viongozi wa ACT–Wazalendo maazimio ya Kikao cha Kamati Kuu iliyoketi kwa dharura Agosti 8, 2021 Mjini Unguja Zanzibar.

Leo kuanzia Saa 4:00 Asubuhi hadi 7:00 Mchana, Kiongozi wa Chama na Viongozi wenzake watakuwa Micheweni. Kisha kuanzia Saa 9:00 Alasiri hadi 11:00 Jioni watakuwepo Chake Chake.

Imetolewa na
Naibu Katibu wa Idara ya Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma.
Janeth Rithe
Agosti 9, 2021

IMG_20210809_092416_434.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom