Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Mbunge wa Kigoma Mjini, (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe ameshangazwa na nchi ya Tanzania kutopiga kura kulaani vitendo vya unyama na ukatili unaofanywa na Serikali ya Myanmar.
"Juzi Umoja wa Mataifa kulikuwa na kura ya Azimio la kulaani vitendo vya unyama dhidi ya watu wa kabila la Rohingya huko Myanmar. Nchi yetu ya haikupiga kura (abstained).
Kitendo cha aibu sana Tanzania kushindwa kulaani vitendo vya namna hii. Sera yetu ya Mambo ya Nje imebadilika mno tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani.
Kule Rakhine State Myanmar watu wanauawa, watoto wa kike wanabakwa (sijui makamu wa rais Samia Suluhu Hassan anajisikiaje kuona wizara yake ya mambo ya nje inaona aibu kukemea ubakaji wa watoto wa kike).
Che Guevara alipata kusema kuwa rafiki yangu ni yule ambaye anatetemeka akisikia tu kuna mtu anaonewa popote pale duniani. Tanzania ya leo sio tu haitetemeki, inaona aibu kukemea uvunjifu wa haki za binadamu ". Amemaliza kwa kuandika hivyo kwenye ukurasa wake wa Twitter, Zitto Kabwe