Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,744
lakini ni kweli hao viongozi wetu wanakuwa hawajui nini wanapaswa wafanye? mimi nadhani wengi huwa wanajua ndo maana kule kwenye kampeni wanajitahidi kutueleza nini watafanya ila wakishakamata rungu wanajifanya hawajui cha kufanya.Sii wewe pekee ningewaomba vijana wote wanaotaka kuingia siasa wajaribu sana kukutana na viongozi wa zamani wapate kujua undani wa siasa, mitandao, nafasi zao, nguvu ya dola, majukumu na uwajibikaji kwa wananchi...
Leo hii wapo wabunge kwetu hawajui kwamba unapotaka kujengewa mradi jimboni inabidi ufanye ziara kwa waziri mhusika mara kwa mara na sii kusubiri lini serikali itachagua jimbo lako. Ndio maana utaona kuna wabunge wachache wanafanya vizuri kuliko wengi wanaolala tu bungeni wakibeba madigrii yao mkobani..