Zitto Kabwe akamatwa na Polisi baada ya kwenda kuwaona viongozi wa vyama vya upinzani waliokamatwa na Polisi

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,937
25,279
Kiongozi wa Chama, cha ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe amekamatwa na kushikiliwa na Jeshi La Polisi baada ya kufika Kituo cha Polisi Oysterbay kuwaona Viongozi wa Vyama vya Upinzani waliokamatwa tangu Juzi kwa ajili ya kuandaa maandamano ya amani ya kudai Uchaguzi mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

===

UJUMBE WA ZITTO KABWE KWA WATANZANIA KABLA HAJAKAMATWA NA POLISI

Mtanzania Mwenzangu

Kama Unasoma Ujumbe huu, fahamu kuwa nimeshikiliwa kituo cha Polisi Dar es salaam. Baada ya Viongozi wenzangu Kukamatwa kwa kudai Uchaguzi Mpya na Tume Huru za Uchaguzi Tanzania na Zanzibar, niliona leo ni vyema kwenda kuwaona, kuonyesha mshikamano nao na kuwafariji kuwa tulioko nje tunaendeleza mapambano.

Kuchagua Viongozi ni haki yetu ya Kikatiba, Haki hii imeporwa na watawala wakishirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama. Ni wajibu wetu wetu kama Wazalendo wa Taifa hili kuipigania haki hiyo iliyoporwa. Mimi naamini Maandamano ya Amani ni haki ya Kila raia

Mimi, Kiongozi wenu, SITACHOKA kuipigania haki hiyo mpaka pumzi ya mwisho ya uhai wangu. Nawasihi sana endelezeni mapambano hayo. Kukamatwa kwa Sisi Viongozi wenu kuwe chachu kwenu kuendeleza ya mapambano haya kwa njia za amani (Non Violence Means)

Sisi sio wa kwanza, na wala hatutakuwa wa mwisho kupitia mitihani hii. Mapambano ni ya kwenu na Kizazi chenu. Mapambano Haya ni yetu sote.

#TusiacheKupambana
#AlutaKontinyua

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Novemba 4, 2020
Dar es salaam
 
Free all politic cases mnaharibu sherehe ya mkuu kuapishwa kesho.
 
Huyu bwana anavyojisifu kwa ulozi kuna vitu hautarajii vimkute ila vinamkuta.
 
Lipumba "Hata aibu hawana watu hawa ni hatari, ni balaa kuzidi corona"
 
Wakamate sana wenzao nao wasisahau kuwa siku moja nao watakamatwa.
Huyu Rais wetu anachokitafuta atakipata.

Sijui ni kwa sababu elimu yake nayo ni ya kuungaunga hivyo hailewi mambo mengi kwa sababu ya kutojua kusoma kiingereza lakini ajue walikuwepo marais wenye kiburi na wanaongoza nchi zenye nguvu kabisa lakini waliishia mwisho mbaya. Au pegine anapigwa upofu kama ule wa Farao ili tuweze kuingia kwenye Tanzania mpya?
 
Hivi hawa watu hawawezi kufanya kazi zingine nje na siasa?

Maana naona wanahangaika mno kwa kushindwa!

Tunawakaribisha huku uraiani ili kushiriki ujenzi wa Taifa kwa kutumia Maarifa mtambuka.

Kuanzia sasa naanza kuamini huko bungeni watu wanakula raha tupu maana si kwa kulia hivyo.

Mwaka 2025 watu wote tunakwenda kugombea kuteuliwa maana tunaamini huko ni kula, kunywa, starehe na kusinzia tu maana ukishaingia humo hulazimishwi kuchangia!
 
Hawa jamaa watamaliza miaka mitano, kwa kukamatwa kamatwa tuu hili wasipotee kwenye game, mpaka uchaguzi ufike.
 
Back
Top Bottom