Zitto Kabwe ajaza fomu ya Utumishi, pia awasilishwa Muswada binafsi wa kulazimisha Viongozi kuweka wazi mali na madeni

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,312
Tamko langu la Rasimali na Madeni na Muswada wa Sheria kuwezesha Tamko la Mali na Madeni kuwa wazi kwa umma.

Ndugu Watanzania, Kama mnavyofahamu kuwa ibara ya 132(4) na (5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kifungu cha 9 na 11 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria namba 13 ya mwaka 1995 inataka viongozi wote wa umma kujaza fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni. Tamko hilo huwasilishwa Sekretariat ya Maadili ya Viongozi kabla ya mwisho wa kila mwaka. Kama nifanyavyo siku zote, nawajulisha rasmi kwamba nimetimiza matakwa hayo ya katiba na sheria kuhusu Maadili ya Viongozi. Nimewasilisha fomu za Tamko langu leo kwa ofisi za Bunge na Ofisi za Sekretariati ya Maadili ya Viongozi.

Inafahamika kuwa Chama Cha ACT Wazalendo, kwa mujibu wa Katiba yake na Azimio la Tabora, kimeelekeza kuwa Viongozi wake wote waweke wazi kwa Umma Tamko la Mali, Madeni na Maslahi. Kwa kufuata masharti ya Katiba ya Chama Cha ACT Wazalendo natangaza rasmi fomu zangu nilizowasilisha Leo Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Kwa ufupi Tamko langu la mwaka 2017 halina tofauti sana na mwaka 2016 isipokuwa eneo la kadhaa kama ifuatavyo;

1) kuongezeka kwa Deni jipya kutoka Benki ya Azania tshs 104 milioni na deni la mtu Binafsi la $2300

2) kupungua kwa Madeni ya CRDB kutoka tshs 214 milioni kufikia tshs 143 milioni na NSSF tshs 142 milioni kutoka 191 milioni baada ya kuyalipa kwa mwaka mzima uliopita

3) kuongezeka kwa rasilimali ambazo ni hisa 60,000 za Kampuni ya Vodacom

4) kupimwa kwa ardhi eneo la Mangamba Manispaa ya Mtwara Mikindani 42 surveyed and tittled plots).
Mengine yote ni kama mwaka uliopita.

Wito

Narudia wito wangu kwamba umefika wakati Daftari la Rasilimali na Madeni la Viongozi wa Umma liwe linawekwa wazi kwa Umma ili wananchi waweze kujua Mali, Madeni na Maslahi ya Viongozi wao na pale ambapo kiongozi ametoa habari zisizo sahihi au kuficha mwananchi aweze kutoa Taarifa kwenye Sekretariat na Baraza la Maadili liweze kufanya kazi yake ipsavyo.

Wakati kama huu mwaka Jana nilisema “Mfumo wa kuweka wazi Rasilimali na Madeni ya Viongozi wa Umma ni mfumo endelevu na muhimu kwenye vita vita dhidi ya ubadhirifu na ufisadi. Mataifa kadhaa duniani hutumia mfumo huu ( public disclosure of leaders’ assets and liabilities) kuwezesha mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Nchini Uingereza na Kanada kwa mfano, daftari la matamko ya Rasilimali na Madeni ya Viongozi lipo wazi kwa kila mwananchi kuona na huuzwa kwenye duka la vitabu la Bunge”.

Namsihi Sana Rais John Pombe Magufuli kusaidia kufanya mabadiliko makubwa ya Sheria ya maadili ya Viongozi ili kurejesha na kuboresha Miiko ya Viongozi katika kuimarisha vita dhidi ya ufisadi nchini. Ninamkumbusha Rais aongoze kwa mfano na kuweka wazi Tamko lake la Mali na Madeni. Rais afanye hivyo na aweke wazi Mali, Madeni na Maslahi yake ya Kibiashara ili awe mfano kwa Viongozi wengine Nchini.
Kitendo cha Rais kwenda Mwenyewe Tume ya Maadili ni hatua muhimu kutukumbusha watu wote wenye dhamana kutii matakwa ya sheria. Rais aende mbele zaidi kwa kuweka fomu zake wazi kwa umma.

Leo pia nimewasilisha Muswada Binafsi wa Sheria ili kuweka vifungu vitakavyolazimisha Bunge kuweka wazi muhtasari wa matamko ya Mali na Madeni ya Wabunge ( wakiwemo Waziri Mkuu na Mawaziri ).

Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
Kigoma Mjini
29/12/2017
e7165f5e10d1fea881cd76d8a162d064.jpg

2efdbca716b541d30fb328fc63c0264e.jpg

691d997a2653041d2be272e047910e34.jpg

55997fdb5944f707d013b14221248729.jpg

697a212bfc158243be800cbc2f3cecc7.jpg
Naona Zitto kapiga hatua kubwa mbele zaidi kumzidi Mh.Rais, baada ya kuonyesha fomu hadharani kitu ambacho Raisi hakukifanya.

Kwa hili pongezi kwako Zitto..!

Je hizi ndio mali pekee anazomiliki Zitto Kabwe..?

Mwisho nimwombe na Mh.Raisi aweke fomu yake hadharani ili wananchi tujue anamiliki nini kwa sasa mshahara na matumizi yake
 
Bado maskini mm nimeshikilia bombardier yenu guess my wealth hommie.
 
Je hizi ndio mali pekee anazomiliki Zitto Kabwe..?
Kuweka fomu public kunaweka tafsiri moja kwamba, kama kuna yeyote anayehisi ana mali nyingi zaidi ya hizo zilizoorodheshwa, basi na aziweke public!!!

Kinyume chake, yeyote atakayelalamika kwamba Zitto ana mali nyingi zaidi kuliko hizo alizoorodhesha, hapo ataonekana ni mtu wa majungu na fitina kwa sababu, nikisema nina TZS 1000 halafu ukadai eti nina TZS 1500, basi ni wajibu wako kuonesha hizo TZS 500 nimeziweka wapi vinginevyo utaonekana mzandiki tu!!!
 
e7165f5e10d1fea881cd76d8a162d064.jpg

2efdbca716b541d30fb328fc63c0264e.jpg

691d997a2653041d2be272e047910e34.jpg

55997fdb5944f707d013b14221248729.jpg

Naona Zitto kapiga hatua kubwa mbele zaidi kumzidi Mh.Rais, baada ya kuonyesha fomu hadharani kitu ambacho Raisi hakukifanya.

Kwa hili pongezi kwako Zitto..!

Je hizi ndio mali pekee anazomiliki Zitto Kabwe..?

Mwisho nimwombe na Mh.Raisi aweke fomu yake hadharani ili wananchi tujua anamiliki nini kwa sasa mshahara na matumizi yake
Ni imani yangu wabunge wote wa UKAWA watafuata nyayo za Zitto!
 
Back
Top Bottom