Zitto kabwe aitimulia vumbi ccm kampeni za udiwani manispaa ya songea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto kabwe aitimulia vumbi ccm kampeni za udiwani manispaa ya songea

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Stephano Mango, Mar 29, 2012.

 1. S

  Stephano Mango Verified User

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Na Stephano Mango, Songea
  WANANCHI wametakiwa Kuonyesha hasira zao kwa watawala kwa kuwachagua wagombea udiwani waliosimamishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)katika Kata saba nchini ambazo zinafanya uchaguzi mdogo aprili mosi mwaka huu pamoja na ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki

  Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni za udiwani Kata ya Lizaboni Manispaa ya Songea Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe jana kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Madizini
  Kabwe alisema kuwa tunajitahidi sana kulalamika kwenye majukwaa mbalimbali lakini kama wananchi hamta onyesha hasira zenu wakati wa uchaguzi kwa kuipumzisha Ccm madarakani na kuipatia Chadema fursa ya kuongoza hii nchi haitakuwa na maana yoyote

  Alisema kuwa kila mwananchi mwenye hasira ya kunyimwa mbolea ya ruzuku, kupanda kwa gharama za maisha, kukosa madawa hospitali, kukosa maji, elimu bora, kukosa miondombinu basi anapaswa kuichagua Chadema ili iweze kuwatumikia wananchi bila upendeleo

  Alisema kuwa mwananchi kama kweli amechukizwa na mauaji yaliyofanyika Songea hivi karibuni na mambo mengine mengi ambayo wamekuwa wakifanyiwa wananchi na Serikali ya Chama cha Mapinduzi wanatakiwa kuipumzisha sasa Ccm madarakani

  Alieleza kuwa uchaguzi huu mdogo unapaswa uwe salamu tosha kwa watawala kuwa watanzania mmechoka na utawala usiozingatia haki za binadamu hivyo hasira zenu zinapaswa zionyeshwe kwenye sanduku la kura

  " Watanzania hamna siraha kubwa itakayoweza kuwatisha watawala zaidi ya kuwakataa kwenye sanduku la kura kwani mkiandamana watawapiga risasi, mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na virungu hivyo muda wa kuionyesha siraha yenu ni sasa kwenye uchuguzi wa aprili mosi mwaka huu" alisema Kabwe

  Alisema kuwa siku hiyo wananchi mnapaswa kuonyesha hasira zenu kwenye sanduku la kura hivyo tumieni vizuri fursa hiyo adimu kwa kuikataa Ccm kwani kura yenu ni zaidi ya kumpata Diwani hivyo kura yenu ni sauti yenu mnapaswa kuitimia vizuri siku hiyo

  Alieleza zaidi kuwa kila sehemu utakayopita utasikia wananchi wakilalamikia matatizo ya mbolea ya ruzuku kutokana na mfumo wa ufisadi ulionea kwenye dhana hiyo unaosababisha adha kubwa kwa wananchi

  Alifafanua kuwa mbolea ya ruzuku ni ufisadi mwingine unaotokana na fedha za wananchi kwani bunge lilipisha bilioni 60 kwa ajili ya kuagiza mbolea ya ruzuku ili wananchi waweze kukombolewa katika kilimo lakini wananchi hawanufaiki na ruzuku hiyo huku Serikali ya Ccm ikiendelea kunufaika na ufisadi huo

  " Ili wakala aweze kugawa mbolea anatakiwa ahonge ndipo asambaze mbolea kwa wananchi na ili wananchi waweze kunufaika nao wanalazimishwa watoe rushwa hali inayopelekea gharama za mbolea ya ruzuku kuwa kubwa kuliko bei ya mbolea ya kawaida" alieleza Kabwe

  Naye Mbunge wa Vitimaalu Chadema Chiku Abwao alisema kuwa uchaguzi mdogo ni njia ya rejareja ya kuiondoa Ccm madarakani na inapofika uchaguzi mkuu ni njia ya jumla ya kuiondoa madarakani Ccm kwa kuwa haina jambo jipya la kuwaambia watanzania hivyo uchuguzi huu unapaswa kuipiga chini Ccm na kuinyong'onyesha kabisa na kwamba utakapo fika uchaguzi mkuu ni kuidondosha kabisa

  Abwao alisema kuwa wananchi wa Manispaa ya Songea mmenyanyaswa vya kutosha sasa ni wakati wenu wa kusema basi kwa kumchagua diwani wa Chadema ili awe mtetezi wenu wa kweli kwa maslahi ya wananchi wote
  Alisema kuwa wananchi wa Kata ya lizaboni mnapaswa muone fahari kumchagua mgombe wa Chadema Mlongo kwani ni mtu jasiri na mwenye mipango ya maendeleo katika kata hii hivyo tumia kura yako kwa kumchagua kiongozi makini na mchapa kazi wa kweli

  Akizungumza kwenye mkutano huo Makamu mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Juliana Shonza alisema kuwa vijana ndio nguvu kazi ya Taifa lolote lile dunia na ndilo chimbuko la maendeleo lakini ni kundi ambalo limekuwa likipuuzwa nchini

  Shonza alisema kuwa Ccm imeshindwa kutambua mchanga wa vijana katika nchi hivyo vijana wenyewe wanapaswa kuchukua hatua ya kuwakataa watawala wanaotokana na chama hicho ili waweze kupata neema katika nchi
  Alisema kuwa katika uchaguzi huu vijana wanatakiwa kutuma salamu kwa watawala kwa kuipigia kura Chadema na kulinda kura hizo mpaka Diwani kupitia chama hicho aweze kutangazwa mshindi ili aweze kushirikiana na vijana katika ujenzi wa Songea na Taifa kiujumla

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime alisema kuwa wagombea wa Ccm wanapaswa wawaeleze wananchi walichofanya toka waanze kuiongoza nchi hii kwani ni miaka 50 sasa

  Fuime alisema kuwa wagombea hao hawapaswi kutoa ahadi mpya kwasababu ahadi hizo walikwisha kuzitoa katika uchaguzi mkuu wa 2010 hivyo sasa wanapaswa kuwaeleza wananchi toka wakati huo wametekeleza jambo lipi

  Kwa upande wake mgombea wa udiwani Kata ya Lizaboni Alanus Mlongo aliwaomba wananchi wamchague ili awe mwakilishi wao wa kweli katika kata hiyo ambayo kwa muda mrefu sasa imesimama kutokana na kutokuwa na viongozi wanaojali maslahi yao

  Mlongo alisema kuwa akiwa Diwani hatakubali kuona wananchi wakiteseka kwa kudhurumiwa haki zao na viongozi wasio na dhamira ya dhati ya kusaidiana na wananchi kuleta maendeleo stahiki ili kuyafikia maisha yenye ustawi stahiki
  MWISHO
   
 2. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante sana mkuu kwa taarifa kutoka uko Songea
   
 3. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Pasua anga wanamageuzi ili kuleta tumaini jipya Tanzania..
   
 4. Walikughu

  Walikughu Senior Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hongera zitto kwa sasa kinachotakiwa ni kutumia nguvu nyingi kwa kuelimisha wananchi ili ikapo mwaka 2015 CCM ichinjiwe Baharini. Pia kuna vyama ambavyo vinaweza vikawa vinataka ushirikiano basi msisite kuwa pamoja hasa vya Upinzani wa kweli
   
 5. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  I rily lyk m4c.
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,798
  Trophy Points: 280
  Mambo ya ushirikiano na vyama usitake kutuchanganya, viambie hivyo vyama viachane na mission ya uvyama wajiunge cdm, tuikomboe nchi.
   
 7. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  :violin:
   
Loading...