Zitto Kabwe, Aden Rage laivu STAR TV

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Mahojiano makali sasa hivi yanendelea STAR TV kati ya ZItto kabwe na Aden Rage........baadhi ya mambo yanayoongelewa ni pamoja na namna ya kushirikiana kuendeleza barabara za mawasiliano za Kigoma na Tabora, ushirikiano na ushindani bungeni...........
 

Plato

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
420
94
Unamwona rage? Ndo anaanza lakini mawazo yaleyale ya kina msekwa.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Nimemwona hana jipya.............Rage amtabiria Anne Makinda kushinda kura zote 252 za wabunge wa CCM na nyingine kutoka upinzani lakini Zitto amtabiria Marando kuweka historia ya kuwa mpinzani wa kwanza kuwa spika wa wabunge kama ilivyokuwa uingereza..............
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Swali la kwanza mpiga simu na msikilizaji wa Star tv ataka kujua kwa nini CCM imeweka "gender issues" kama kivuli cha kufunika maovu ndani ya bunge na kuna tetesi kuwa Anne Makinda anafadhiliwa na mtandao wa kifisadi...................sasa auliza hivi akishinda ile mikakati aliyoiweka Sitta ya kupambana na ufisadi sasa itakuwa na mwelekeo upi? Ukizingatia Makinda ni zao la mafisadi?
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Swali la pili mpiga simu ataka kujua ni kwa nini CCM imelazimisha wabunge majina 3 ya wanawake badala ya kuwapa wabunge wake nafasi ya kujichagulia wamtakaye kutokana na orodha ya wote walioomba? Aiasa CCM sasa isije ikatafuta mchawi pale ambapo Mabere Marando atakapochaguliwa kuwa Spika wa Bunge na Anne Makinda asipochaguliwa.................
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Swali la tatu na la mwisho liliulizwa na Juma Nyaiganga wa Shinyanga ambaye alitaka kufahamu kwa nini CCM inachezea demokrasia ndani ya chama hicho wakati ikijua Anne Makinda siyo mwanademokrasia bado inataka awe spika wa bunge.................rekodi ya Makinda ni kutetea u-CCM wake tu................................atoa mfano wa maswali ambayo Zitto aliwahi kuyauliza bungeni wakati Sitta akiwa ni spika na aliweza kuwashinikiza mawaziri wa CCM kuyajibu lakini kama angelikuwa ni Anne Makinda siku hiyo Zitto angelichukuliwa hatua za kinidhamu
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Juma Nyaiganga kama walivyokuwa waulizaji maswali wawili waliomtangulia washauri wabunge wa CCM kuweka masilahi ya nchi kwanza na kuukataa chaguo la mafisadi ambalo ni Anne Makinda kwa kumpigia Mabere maucho Marando kuwa spika wa kwanza kutoka upinzani ambaye ana sifa zote kwa kazi hiyo na anaweza kuhimili vishindo vyote vya mafisadi...................
 

Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
8,204
3,532
Anne Makinda is a bomb timed bomb kwa bunge, ccm na wabunge wote. She is very useless kwa Watanzania kwa sasa. Kwa namna alivyoendesha bunge kwa kuwanyamazisha wabunge wa upinzania, anachukulia siasa za ushindani as attach to herself. Her era has gone long ago!

Angeachana na siasa akaenda kucheza na wajukuu tu! (if she has any)
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Aden rage awabeza wauliza maswali wote 3 akidai ni wanachama wa Chadema .......mabezo yake hayafafanui zaidi ya kusema kwa mtu mwenye akili na busara atajua kuwa ni wanachama wa chadema tu.....................
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Aden rage aendelea kutoa mpya............adai kuwa Anne Makinda ni mlima Kilimanjaro na Mabere Marando ni kichuguu lakini hafafanui ni kwa nini.....................
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Aden Rage adai Marando hajawahi kuwa Mbunge jambo ambalo siyo kweli kwa ni Marando aliwahi kuwa Mbunge wa Jumuiya ya Afrika mashariki.................
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Aden Rage aendelea na kusema kuwa Marando hajawahi kuongoza kamati yoyote ile..........................
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Aden rage sasa ampooza Zitto Kabwe kwa kudai angalau Zitto bunge hili lililomaliza muda wake alikuwa Mwenyekiti wa Kamati nzito bungeni na hivyo ana sifa ya kuwa Spika wa Bunge ...............................Zitto achekelea kidogo.........................
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Aden rage atoa mifano ya nchi mbalimbali ambazo zimetoa maraisi na mawaziri wakuu wanawake...ataja India, Uingereza na nyinginezo........na hii aona ni hoja kwa Tanzania sasa kuwa na Spika mwanamke.....................................
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Zitto kabwe naye apewa nafasi ya kuyajibu maswali yale matatu ambayo Rage tayari kesha kuyajibu......................muda wazidi kuyoyoma...........................saa tatu asubuhi hii bunge laanza mchakato wa kumchagua spika na hawa waheshimiwa inabidi waende huko kutekeleza majukumu yao.............................
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Zitto ajibu hoja kama ifuatavyo........................aliomba bunge hili kumchagua spika kwa kutanguliza masilahi ya utaifa badala ya masilahi binafsi au mapenzi ya vyama ambavyo wabunge wanatoka..................................
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Zitto Kabwe apinga hoja za Aden rage kuhusiana na sifa za Marando........................Mabare marando ni mwanasheria na kazi ya spika ni kutafsiri sheria na kanuni za bunge.......................na hata spika aliyetangulia Bw. Sitta ilibidi akasomee sheria ili aweze kumudu majukumu ya bunge.........................
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,615
728,447
Kabwe aendelea kufafanua ya kuwa katika bunge la Afrika ya Mashariki ambapo Kinana ndiye aliyekuwa Spika wake wa kwanza kila mara alipokuwa safarini alikuwa anamwachia mabere marando uspika kutoka na umahiri wake wa kiutawala na kwenye nyanja za sheria..........
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom