WINGER_TEREZA
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 242
- 450
Akiongea mapema leo asubuhi katika kipindi cha Joto Kali la asubuhi kinachorushwa na vyombo vya habari vya TVE na Efm Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe, ameongea mambo mengi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii na ameichambua bajeti kuu ya Serikali iliyowasilishwa week iliyopita Bungeni.
Kwa upande wa kuanzishwa kwa chama chake amesema chama chao kilianzishwa kutokana na mchango mkubwa wa Professor Kitila Mkumbo (ambaye amesema ndiye mwandishi wa katiba ya ACT-WAZALENDO), yeye mwenyewe (Zito) na Mwanaharakati mmoja mwenye jinsia ya kike ambaye aligoma kumtaja!.
Zito alijibu hivyo baada ya kuulizwa swali na muongozaji wa kipindi hicho, Jeradi Hando, alilomuuliza ni vipi chama kiliathirika baada ya viongozi wakuu wa chama chao kuteuliwa kushika nafasi mbalimbali serikalini katika awamu ya tano. Miongoni mwa viongozi alikuwa ni Anna Mgwira, ambaye alikuwa mwenyekiti wa chama, aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Pia kuna Kitila Mkumbo(Phd), alikuwa mshauri mkuu wa chama, aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya maji na umwagiliaji. Zito aliamini hakukuwa na ulazima kwa Kitila Mkumbo kuondoka katika chama alichokianzisha yeye mwenyewe na kwenda CCM badala yake angefanya kazi zake za Serikali ilihali akiwa bado mpinzani.
Swali langu ni, kwanini Zito aliogopa kumtaja huyo Mwanaharakati wa kike? Na anaweza akawa ni nani? Au Fatma Karume aka Shangazi, maana kuna kipindi alikuwa karibu na ACT - Wazalendo ata kwenye mkutano wao mkuu Shangazi alionekana ku-engineer mambo fulani fulani katika harakati za kutafuta kuingia "White House".