Zitto Kabwe: ACT itaendelea kumheshimu mzee Sumaye na hawatasita kuomba ushauri wake itakapolazimu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,761
141,626
Kiongozi mkuu wa ACT wazalendo mh Zitto Kabwe amesema chama chake hakijafanya mazungumzo yoyote na mzee Sumaye kuhusu Waziri mkuu mstaafu huyo kujiunga na chama chao.

Zitto amesema mzee Sumaye ameweka wazi msimamo wake wa kupumzika siasa za vyama na kwamba atabakia kuwa mshauri kwa vyama vyote bila kujali itikadi.

Zitto amesisitiza kuwa wataendelea kuuthamini mchango wa mzee Sumaye kwani huo ndio utamaduni wa ACT wazalendo kuwaenzi wastaafu na kwamba watamwendea kwa ushauri itakapobidi.

Source ITV habari!
 
IMG-20190629-WA0000.jpeg
 
Zitto bana!

Kama utaratibu wa ACT-Wazalendo ni kuwaenzi wastaafu kwa nini anatudanganya kuwa kama ACT-Wazalendo itashika dola lazima wamshitaki mahakamani Rais Magufuli?

Huwezi kuwatofautisha wanasiasa na unafiki!
 
Atamshtaki Rais Magufuli kwa kutumia katiba gani?!
 
But wazee wapo wengi Tz, ila Sumaye ni mmojawapo!, huu upepo unaelekea kupita hivyo...
 
Back
Top Bottom