Zitto Kabwe Achangia Bima Ya Afya Ya Mjane Wa Mwangosi Na Wanawe Kupitia NSSF

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
KATIKA siku ya mwisho ya harambee ya kumchangia mjane wa marehemu Daud Mwangosi, Ndugu Zitto Kabwe amejitolea kumchangia mjane wa marehemu kwa kumlipia ada ya uanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Kijamii (NSSF) kwa kila mwezi na kwa miaka mitatu mfululizo.

" Nimeona nami niunge mkono harambee hii.Pamoja na michango ya fedha iliyotolewa kumsaidia mjane kuanzisha mradi wa kujikimu, mimi naona ni muhimu pia mjane akawa na hakika ya huduma ya afya yake na watoto wake wanne. Hivyo, mchango wangu utakuwa ni kwenye eneo hilo Bima ya Afya na kwa miaka mitatu." Anasema Zitto Kabwe alipoongea na Mjengwablog.com, mtandao wa Kijamii ulioratibu harambee ya mjane wa Daud Mwangosi.

Hii ni mara ya pili kwa Ndugu Zitto Kabwe kuchangia kwenye masuala ya kijamii kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com, mara ya kwanza ni alitoa mchango wake pale Mtandao wa Mjengwablog.com ulipoendesha harambee ya kuwachangia watoto wa Somalia waliokuwa katika hatari ya kufa kwa njaa.

Katika harambee iliyomalizika Jumapili ya Septemba 30 mwaka huu na iliyochukua kipindi cha mwezi mmoja,zaidi ya shilingi milioni tano na nusu zimekusanywa.

Mchango huo wa Ndugu Zitto Kabwe una maana mjane wa marehemu ataweza kuwa na hakika ya yeye na watoto wake wanne kupata huduma za afya bila kufikiria malipo kwa kipindi cha miaka mitatu. Baada ya hapo,michango ya mjane huyo ya kila mwezi kwa mfuko huo wa hifadhi ya kijamii ( NSSF) ambayo atakuwa akilipiwa na Ndugu Zitto Kabwe itakuwa ni malimbikizo ya akiba yake ambayo mjane atakuwa na uwezo wa kuichukua kama akipenda. Kwa sasa mjane wa Daud Mwangosi hayuko kwenye utaratibu wowote wa Bima ya Afya, kwake yeye na wanawe.

Harambee ya mjane wa Daud Mwangosi iliyoendeshwa kwa uwazi kwa njia ya MPESA, TigoPesa, Airtel Money, NMB Mobile na Western Union ilimwezesha mchangiaji kuliona jina lake na mchango wake kwenye orodha ya wachangiaji iliyokuwa ikiwekwa mtandaoni kila siku. Michango ilikuwa ni hiyari, hakuna aliyeombwa kutoa na utaratibu haukuruhusu ahadi za kuchangia, bali, mwenye nacho alitoa na hapo hapo kuorodheshwa kama mchangiaji. Utaratibu haukuruhusu pia michango iliyofungamana na siasa za vyama.

Hatua hiyo ya uwazi na kutanguliza ubinadamu na si itikadi kwenye uchangiaji imechangia kupelekea Watanzania wengi wa kada zote, kwa namna moja au nyingine kushiriki kwenye kuchangia. Kuna waliochangia shilingi elfu moja na kuna waliochangia mpaka shilingi milioni moja.

Ari hii ya Watanzania kujitolea kusaidiana kwenye hali kama iliyomkuta mjane wa Daud Mwangosi imedhihirisha umoja na upendo tulionao kama Watanzania, na pia imeonyesha jinsi tunavyoijali amani yetu na hivyo jamii, kupitia michango hii, imeonyesha pia kwa vitendo, dhamira ya kulaani kwao vitendo vya maovu na vinavyotokana na matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima kama kile kilichomtokea mwandishi Daud Mwangosi.

Baadhi ya watu maarufu katika jamii waliojitokeza kwa hiyari yao kumchangia mjane wa Daud Mwangosi kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com ni pamoja na Shy- Rose Bhanji, Ananilea Nkya, John Bukuku ( Mmiliki wa Fullshangwe.blog) na Ndugu Mobhare Matinyi aliyepata kuwa mhariri wa gazeti la Majira.

Michango kwa mjane wa Daud Mwangosi itaingizwa kwenye akaunti ya mjane ya CRDB, Iringa leo alhamisi, Oktoba 4, 2012. Vielelezo vya kibenki vitawekwa kwenye mtandao wa Mjengwablog.com kwa kila mmoja kuona jumla iliyowasilishwa kwa mjane na orodha ya majina ya wachangiaji.

Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765, 0754 678 252
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
 
ubarikiwe ndugu zitto...nimefurahi kuwa hukuitisha press conference kutangaza nia hiyo..
 
Nawapongeza wote waliojitolea kumuwezesha huyo mama na familia yake. Mungu awabariki

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hongera ZZK, hongera sana ndg.Mjengwa kwa kuanzisha harambee hii ambayo umeifanya kwa ukweli na uwazi mkubwa. MUNGU wangu AKUBARIKi!
 
Mjane Wa Mwangosi: Michango Yote Imeingizwa Kwenye Akaunti Ya Mjane Leo Alhamisi...
1. Chris Cremence 100,000
2. Anonymous 500,000
3. Maggid Mjengwa
100,000
4. Raymond Kasoyaga 20,000
5.Edward Mgogo 10,000
6.Joachim Kiula 5,000
7.Libory Muhanga 5,000
8.Geofrey Kagaruki 10,000
9.Sadiki Mangesho 10,000
10. Edwin Namnauka 40,000
11.Daud Mbuba 10,000
12. Anonymous 200,000
13.Mikidadi Waziri 6,000
14. Bungaya Mayo 5,500
15. Abraham Siyovelwa 50,000
16. Godfrey Chongolo 22,222
17. Jacob Mwamwene 51,000
18. Denis Bwimbo 153,683
19. Zanzibar Ni Kwetu 150, 464
20.Felex Mpozemenya 10,000
21.Rweyendera Ngonge 11,000
22. Festo Temu 10,000
23. Azaria Mulinda 10,000
24.Khatibu Kolofete 5,000
25. John Bukuku 25,000
26. Abel 10,000
27. Hafidh Kido 10,000
28. George Mtandika 16,000
29. Shy-Rose Bhanji 200,000
30. Raymond Nkya 52,000
31. Maganga Sambo 10,000
32. Felix Mwakyembe 10,000
33. Abdul Diallo 5,000
34. Newton Kyando 20,000
35. Galanos Myinga 20,000
36. Anonymous ( 200 Euro) 497,000
37. Yasinta Ngonyani 50,000
38. Prosper/ Willy ( Japan) 314,000
39. Nuru Mkeremi 131,000
40. Anonymous 50,000
41. Josephine Mahimbo 50,000
42. Anonymous 150,000
43. Heladius Macha 30,000
44. Emma Malele 10,000
45. Anonymous 60,000
46. Hendry Mlay 35,000
47. Hosea Ngowi 10,000
48. Athuman Zuber 5,000
49. Hyancinth Komba 7,500
50. Edson Kihongole 11,500
51. Godfrey Emmanuel 20,500
52. Deus M 27,000
53.Sigisto Amon 10,000
54.Issa Kubonya 10,000
55. Richard Dalali 6,000
56.Fadhili Mtanga 20,000
57. Polycarp Ngowi 5,000
58. Salehe Mfaume 10,000
59. Deodatus Balile 20,000
60. Moses Ringo 15,000
61. Dr Rukoma 100,000
62. Mobhare Matinyi 100,000
63. Humphrey Simba 16,000
64. Fredrick Kyambile 10,000
65.John Mwakyusa 20,000
66. Abdul Njaidi 40,000
67. Fidelis Francis 10,000
68.Mutachumwa Mukandala 10,000
69. Augustino Lukosi 12,500
70. Goodluck Arobogast 20,000
71. Lusajo Mwasaga 15,000
72. Carolina Reynolds 5,500
73. Rugenamu Kawa 30,000
74. Innocent Kimario 5,000
75. Jumuiya Ya Watanzania UK 1,000,000
76. Josephat Mwagala 150,000
77. Sara Mawere 5,000
78. Deograsias Hyasini 15,000
79. Anonymous 10,000
80. Said Kambi 20,000
81. Cassian Mayega 10,000
82. Mary Glad 5,000
83. David V 153,000
84. Anonymous 100,000
85. Lingson Adam 21,500
86. Augustus Fungo 25,000
87.Seka Henjewele 5,000
88.Deusdith Bishweko 5,000
89.Robert Clemens 10,000
90.Isak Kabingo 10,000
91.Irene Massawe 10,000
92. Oliva Bujulu 11,000
93. John Lemomo 10,000
94. Joseph Rocket 500
95. Prosper Simon 5,500
96 Andy Mwakibete 2,000
97. Ramadhani Kasonso 20,000
98. Anonymous 11,000
99. Jenga Ngalawa 200,000
100.Stanslaus Nnyari 5,000
101.Luth Twissa 75,000
102. Mdodi Mlelwa 2,000
103. Hatibu Kiobya 5,000
104. Benjamin Mkalava 5,000
105. Manfred Mjengwa 11,000
106. John Malanilo 12,000
107. Lutgard Kokulinda Kagaruki 20,000
108. Kazikupenda Chale 25,000
109. Boniface Sechuma 10,000
110. Edmund Temu 5,000
111. Edwin Moshi 5,500
112. Syldion Semazina 5,000
113. Pastoc Shelutete 50,000
114. Ananilea Nkya 50,000
115. Lucy Bwana 21,000
116. William Genya 25,000
117. Anonymous 300,000
118. Adam Bakari 21,000
119. Gilbert Mkindi 5,000
120. Meriki Kinuno 5,000
121. Samuel Nguyaine 25,000
122. Josephat Godfrey 15,000
123. Anold Mturi 1,500
124. Gadiel Malisa 5,000
125. Ebenezer Mshana 11,000
126. Mussa Kopwe 1,000
127. Emmanuel Kitomari 6,000
128. Stella Kisale 2,000
129. Kahitwa Bishaija 20,000
130. Lucy Massawe 1,000
131. Valentini Temba 10,000
132. Victor Lucas 2,000
133. Irene Mdami 5,000
134. Killey Mwitas 10,000
135. Godwin Mushi 2,000
136. Adinani Madawili 2,000
137. Bryson Munisi 20,000
138. Sarah Beckham 50,000
139. Chrispin Modestus 11,000
140. Luiham Ringo 11,000
141. Marko Gideon 5,000
142. Peter Msuya 2,000
143. Maria Mvula 5,000
144. Safina Mbwelei 15,000
145. Sebastian Ivambi 15,000
146. Jackson Minja 1,000
147. Joseph Swai 5,000
148. Albino Simbila 8,000
149. David Sheshe 21,000
150. Nichs Kutumiwa 1,500
151. Mwanaidi Swedi 5,000
152. Mwajuma Abdalla 2,500
153. Richard Azrikamu 20,000
154. Mahafudh Nassoro 10,000
155. Anonymous 50,000
156. John Maboja 2,000
157. Asajile Mwalukasa 10,000
158. Solomon Rwangabwoba 100,000
159. Daniel Majalla 11,000
160. Anonymous 2,000
161. Lucas Olomi 2,000
162. Gloria Daudi 3,000
163. Fulgence Massawe 25,000
164. Godfred Mbanyi 50,000
165. Anna Mghwira 20,000
166. Vedasto Msungu 30,000

Jumla: 5,635,000 ( Shilingi Milioni Tano Na Laki Sita Na Thelathini Na Tano Elfu )

Mjengwablog, na kwa niaba ya Itika Mwangosi, mjane wa marehemu Daud Mwangosi inawashukuru kwa dhati wale wote waliojitolea kwa hiyari zao kumchangia mjane wa marehemu ili aweze kupata mtaji wa kuanzisha shughuli za kujikimu uweze kumsaidia yeye na watoto wake wanne. Na kama alivyotamka mjane wa marehemu; " Mungu ndiye atakayewalipa".

Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
http://mjengwablog.com/ 1.jpg
 
[h=2][/h]04/10/2012
0 Comments

KATIKA siku ya mwisho ya harambee ya kumchangia mjane wa marehemu Daud Mwangosi, Ndugu Zitto Kabwe amejitolea kumchangia mjane wa marehemu kwa kumlipia ada ya uanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Kijamii (NSSF) kwa kila mwezi na kwa miaka mitatu mfululizo.

"Nimeona nami niunge mkono harambee hii.Pamoja na michango ya fedha iliyotolewa kumsaidia mjane kuanzisha mradi wa kujikimu, mimi naona ni muhimu pia mjane akawa na hakika ya huduma ya afya yake na watoto wake wanne. Hivyo, mchango wangu utakuwa ni kwenye eneo hilo Bima ya Afya na kwa miaka mitatu." Anasema Zitto Kabwe alipoongea na Mjengwablog.com, mtandao wa Kijamii ulioratibu harambee ya mjane wa Daud Mwangosi.

Hii ni mara ya pili kwa Ndugu Zitto Kabwe kuchangia kwenye masuala ya kijamii kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com, mara ya kwanza ni alitoa mchango wake pale Mtandao wa Mjengwablog.com ulipoendesha harambee ya kuwachangia watoto wa Somalia waliokuwa katika hatari ya kufa kwa njaa.

Katika harambee iliyomalizika Jumapili ya Septemba 30 mwaka huu na iliyochukua kipindi cha mwezi mmoja,zaidi ya shilingi milioni tano na nusu zimekusanywa.

Mchango huo wa Ndugu Zitto Kabwe una maana mjane wa marehemu ataweza kuwa na hakika ya yeye na watoto wake wanne kupata huduma za afya bila kufikiria malipo kwa kipindi cha miaka mitatu. Baada ya hapo,michango ya mjane huyo ya kila mwezi kwa mfuko huo wa hifadhi ya kijamii ( NSSF) ambayo atakuwa akilipiwa na Ndugu Zitto Kabwe itakuwa ni malimbikizo ya akiba yake ambayo mjane atakuwa na uwezo wa kuichukua kama akipenda. Kwa sasa mjane wa Daud Mwangosi hayuko kwenye utaratibu wowote wa Bima ya Afya, kwake yeye na wanawe.

Harambee ya mjane wa Daud Mwangosi iliyoendeshwa kwa uwazi kwa njia ya MPESA, TigoPesa, Airtel Money, NMB Mobile na Western Union ilimwezesha mchangiaji kuliona jina lake na mchango wake kwenye orodha ya wachangiaji iliyokuwa ikiwekwa mtandaoni kila siku. Michango ilikuwa ni hiyari, hakuna aliyeombwa kutoa na utaratibu haukuruhusu ahadi za kuchangia, bali, mwenye nacho alitoa na hapo hapo kuorodheshwa kama mchangiaji. Utaratibu haukuruhusu pia michango iliyofungamana na siasa za vyama.

Hatua hiyo ya uwazi na kutanguliza ubinadamu na si itikadi kwenye uchangiaji imechangia kupelekea Watanzania wengi wa kada zote, kwa namna moja au nyingine kushiriki kwenye kuchangia. Kuna waliochangia shilingi elfu moja na kuna waliochangia mpaka shilingi milioni moja.

Ari hii ya Watanzania kujitolea kusaidiana kwenye hali kama iliyomkuta mjane wa Daud Mwangosi imedhihirisha umoja na upendo tulionao kama Watanzania, na pia imeonyesha jinsi tunavyoijali amani yetu na hivyo jamii, kupitia michango hii, imeonyesha pia kwa vitendo, dhamira ya kulaani kwao vitendo vya maovu na vinavyotokana na matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima kama kile kilichomtokea mwandishi Daud Mwangosi.

Baadhi ya watu maarufu katika jamii waliojitokeza kwa hiyari yao kumchangia mjane wa Daud Mwangosi kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com ni pamoja na Shy- Rose Bhanji, Ananilea Nkya, John Bukuku ( Mmiliki wa Fullshangwe.blog) na Ndugu Mobhare Matinyi aliyepata kuwa mhariri wa gazeti la Majira.

Michango kwa mjane wa Daud Mwangosi itaingizwa kwenye akaunti ya mjane ya CRDB, Iringa leo alhamisi, Oktoba 4, 2012. Vielelezo vya kibenki vitawekwa kwenye mtandao wa Mjengwablog.com kwa kila mmoja kuona jumla iliyowasilishwa kwa mjane na orodha ya majina ya wachangiaji.

Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765, 0754 678 252
mjengwablog.com

Source:
http://www.wavuti.com/#ixzz28LUdd5ce
 
Hivi kweli sirikali imemkaukia kabisa yule mjane kweli??siamini hii sirikali ni dhalimu kiasi hiki,2015 wataenda kwa wananchi kuwaambia aliuawa bahati mbaya hii ni serikali inayowajali wananchi wake!!!kwelii?????nashindwa kuelewa wanaenda misikitini na makanisani kufanya nini na unafiki wao hivi!!
 
Back
Top Bottom