Zitto Kabwe acha unafiki wa kutumika, hesabu yenu na CCM kuhusu Mbowe tunaijua

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
176
970
Zitto huu unafki hsutakufikisha popote Wallah nakuapia. Ulisema mwenyewe kua hukumaanisha kwamba ulimuombea Mbowe msamaha kwa Rais isipokuwa CHADEMA walikuelewa vibaya, halafu leo unapigilia msumali kua ulimaanisha? Ipo siku utajutia tabia yako hii.

Nia yako ni kutaka Mbowe ajinyenyekeze kwa Rais aombe Msamaha ili aachiwe kwa msamaha jamii iseme kuwa alikuwa Gaidi kweli ndiyo maana meomba msamaha. Halafu kisha baadaye wewe na CCM muanze kukiita CHADEMA Chama cha Magaidi mkipake chama matope, kufungiwa na msajili wa vyama vingi ili chama chako cha ACT kunufaika na kufutwa kwa CHADEMA. Huu mtego wako na CCM twaujua na hatuwezi kunasa kamwe.

Wewe ni Mwislamu usijue kabisa kwamba kuomba msamaha kama huna kosa ni dhambi? Acha tamaa kupitia maisha ya wengine. Achana na Mbowe siyo nduguyo, ungekuwa unampenda ungemsaidia msaada wa kisheria kwa kuongeza idadi ya mawakili.

Unafikiri Mbowe ni muoga muoga kama wewe ambaye mlikubaliana kwa pamoja kuwa hamuutambui uchaguzi kisha nyuma mkageuka kuunda serikali ya umoja wa kitaifa?

Ndiyo maana wenzako wanahangaika na Katiba mpya watengeneze mifumo ya nchi, wewe unadai tume huru ili ushinde ubunge mpate ruzuku kuendesha chama chenu. CHADEMA ni kina kirefu achana nao huwezi kushindana nao, waulize CCM pamoja matumizi yote ya dola wamekiua?
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom