MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Msingi wa hoja yangu ni kupambana na Rais wa Tanzania Versus mafanikio ya kisiasa na kiuchumi kwa wanasiasa na wafanyabiashara kulingana na mzingira ya Tanzania.
Nimechagua watanzania wawili kama kielezo katika uwanja wa siasa na biashara nchini kutokana na historia na mafanikio yao kisiasa na kibiashara.
Mbowe ni mwanasiasa ambaye unaweza kumuita successful political entrepreneur. Mzee Mengi ni mfanyabiashara ambaye unaweza kumuita successful business entrepreneur.
Hawa Watanzania hawakuyafikia mafanikio yao kimakosa bali waliyafikia kutokana na kufahamu vizuri jinsi ya kuzicheza karata zao kutokana na mazingira ya kisiasa na kiuchumi nchini.
Mazingira ya kisiasa nchini hayaruhusu mwanasiasa yoyote au mfanyabiashara kuwa zaidi ya Rais wa Tanzania na kama mwanasiasa au mfanyabiashara anataka kudumaa au kupotea kisiasa/kibiashara basi njia iliyonyepesi ni kupambana binafsi (personal) na Rais wa Tanzania.
Mjuzi wa siasa za Tanzania kama Mbowe alishafahamu dhana ya madaraka ya Rais wa Tanzania ndiyo maana huwezi kumsikia akitoa tamko la yeye kupambana binafsi (personal) na Rais wa Tanzania.
Matamko ya Mbowe ya kisiasa huwa measured kwenye dhana ya taasisi na siyo dhaya ya mapambano binafsi. Mwanasiasa anayezijua siasa za Tanzania kama Mbowe huwezi kumsikia akisema Rais wa Tanzania ameenda kujifunza udikteta kwa Rais Kagame nchini Rwanda, CCM idhibiti udikteta wa Rais wa Tanzania na nitapambana na Rais.
Mbowe hutoa matamko ambayo yanakuwa na nafasi ya majadiliano kati yake na Rais wa Tanzania kwa sababu anafahamu nguvu alizonazo Rais wa Tanzania kwenye siasa, uchumi na kijamii. Matamko ya Mbowe kwa Rais wa Tanzania yanakuwa na dhana ya kujishusha na siyo kujikweza kwa sababu anafahamu kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Rais wa Tanzania ni kimbilio la mwisho kwa wanasiasa na wafanyabiashara .
Matamko ya Zitto hayana dhana zote ambazo anazitumia Mbowe kama anapingana na Rais wa Tanzania. Zitto anatoa matamko kama vile yeye ndiye Rais wa Tanzania. Matamko ya Zitto niya kujikweza badala ya kujishusha.
kwa mfano, Zitto kusema Kagame ni dikteta anaweza kujikuta yuko kwenye mahakama za Rwanda kujibu mashitaka baada ya extradition yenye mkono wa kitaasisi kati ya Rais wa Tanzania na Rais wa Rwanda.
Kwa upande wa Mzee Mengi. Kuna baadhi ya watu wamejenga dhana kuwa ukipambana na Mzee Mengi huwezi kushinda. Inawezekana kuna ukweli ndani yake lakini wanachoshindwa kukibaini au kukielezea ni jinsi ambavyo Mzee Mengi anatumia uelewa wake wa uwanja wa siasa za Tanzania katika kuchagua adui.
Huwezi kukuta Mzee Mengi anapambana na Rais wa Tanzania kwa sababu anafahamu madhara ya kuingia vita ya aina hiyo kutokana na nguvu alizonazo Rais wa Tanzania. Mzee Mengi kama akipingana na Rais wa Tanzania huamua kujishusha na kukaa kimya kwa sababu anafahamu faida ya kufanya hivyo katika uwanja wa kiuchumi nchini.
Mafanikio mengi ya Mzee Mengi katika vita vyake na wafanyabiashara au wanasiasa yamefanikishwa kwa kutumia mkono wa Rais wa Tanzania. Mengi anatambua umuhimu wa kuwa upande wa Rais wa Tanzania kutokana na nguvu alizonazo Rais wa Tanzania.
Zitto anatakiwa ajifunze kwa Mzee Mengi jinsi ya kuchagua adui na kupambana naye.
Watu wenye hekima na busara wanafahamu kuwa ujasiri wa mtu unapatikana kutokana na uwezo wa kuchagua adui/vita na siyo uwezo wa kupambana na kila adui/vita.
Zitto bado hajaondoa mapungufu yake ambayo yaliainishwa kwenye waraka wa mkakati wa Mabadiliko 2013 ulioandikwa na Prof. Kitila Mkumbo kuhusu udhaifu wa Zitto ambapo alisema;
''Maneno yake mara nyingine hayazingatii anayazungumza katika mazingira gani na hivyo kuwasha masikio ya wanataasisi jambo linalompunguzia kukubalika kwake taratibu. Kama ilivyo kwa maneno, kuna matendo pia ambayo mara nyingine huyafanya bila kuzingatia mazingira na wasikilizaji wake na hivyo kupunguza imani ya wana taasisi kwake''.
Ziito ana safari ndefu kuyafikia mafanikio katika uwanja wa kisiasa nchini.