mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,307
- 6,514
RAIS John Magufuli ameshauriwa kuchukua uamuzi mgumu wenye kuibua muafaka wa kudumu kwa mgogoro wa kisiasa Zanzibar, bila kujali uamuzi huo utawafurahisha wengi ama la, uamuzi utakaohusisha kusimamisha Katiba ya Zanzibar na kuunda serikali ya mpito.
Akizungumza na Raia Mwema baada ya mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, kutoa maelezo ya kina kuhusu mazungumzo yanayoendelea baada ya kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar, Jumatatu wiki hii jijini Dar es Salaam, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema suluhisho la mgogoro huo ni kuunda serikali ya mpito ya watalaamu (Technocratic Government) ambayo itafanya kazi ya kutafuta muafaka wa kijamii kwa watu wa Zanzibar na kuandaa uchaguzi.
Alisema kuwa kwa hali ilivyo sasa haoni ni kwa namna gani CCM watakubali matokeo wa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana yatangazwe na pia hawaoni CUF wakikubali kuingia katika uchaguzi wa marudio.
“Kwa maoni yangu iundwe serikali ya mpito ambayo haitahusisha wanasiasa na ifanye kazi ya kuleta mabadiliko ya Katiba, kuunda Tume huru ya Uchaguzi, iongozwe na wataalamu wasiofungamana na vyama vya siasa ili mchakato wa kuleta maridhiano ya kijamii na kutibu makovu yote tangu Mapinduzi ya mwaka 1964,” alishauri Zitto.
Alieleza kwamba maafikiano ya kisiasa ambayo yamekuwa yikifikiwa katika visiwa hivyo yamekuwa yakihusisha wanasiasa ndiyo maana hakuna suluhisho la kudumu, na kwamba kazi ya serikali hiyo ya mpito ambayo anashauri iwepo madarakani kwa kipindi cha miaka mitano, mpaka 2020, iwe ni kutafuta muafaka wa kijamii.
Kuhusu namna ya kuunda serikali hiyo alisema; “Katiba ya Zanzibar isimamishwe pande zote zihusishwe katika uamuzi huo, na kwa kuwa wabunge wa Zanzibar wa Bunge la Jamhuri ya Muugano walitangazwa, pale ambapo mambo ya kisheria yanapotakiwa kufanyika katika serikali hiyo ya mpito, wabunge hao wanakaa kama Baraza la Wawakilishi,” alisema na kuongeza; “Hatuna namna, ni lazima tufanye maamuzi magumu sana kuhusu Zanzibar ili tupate suluhisho la kudumu.”
Kuhusu majukumu ya msingi ya serikali hiyo ya mpito, alisema itakuwa ni kufanya uchambuzi wa kina kuhusu matatizo ya Zanzibar, na kuunganisha jamii ya Wazanzibari ambapo wataalamu hao kwa kusaidiana na mabaraza ya wazee, yatakayoundwa na serikali hiyo, waendeshe marekebisho ya jamii ya Wazanzibari bila kuruhusu vyama vya siasa kuwa na mkono wake.
Amtwisha mzigo Rais Magufuli
Katika kuhakikisha kwamba serikali hiyo inaundwa, Zitto, ametoa wito kwa Rais John Magufuli, kusimamia mchakato wa kuiunda na akifanya hivyo kwa nia njema ataweza kuumaliza kabisa mgogoro wa kisiasa visiwani humo.
“Rais Magufuli ndiyo Mkuu wa Nchi, kwa mazingira ya dharura ndiye peke yake anaweza kuisimamisha Katiba ya Zanzibar, mamlaka haya hayako kwa mtu mwingine,” alisema.
Alifafanua kuwa Rais anayo nafasi kubwa kuingilia kati na kumaliza mgogoro huo kwa kuwa pande zote zinazosigana katika mgogoro huo bado zina imani naye.
Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari aliyoitoa juzi, Maalim Seif alisema kwa hali ilipofikia, inabidi Rais Magufuli aongoze juhudi za kuleta muafaka katika mgogoro huo.
“Rais alipozugumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na mimi Ikulu, Dar es Salaam, alisisitiza haja ya kukamilisha mazungumzo kwa kulipatia ufumbuzi wa haraka, tunaona wakati umefika yeye mwenyewe aongoze juhudi zenye lengo la kufanikisha hatua zilizopendekezwa (na CUF),” alisema Maalim Seif.
Baadhi ya hatua zilizopendekezwa na CUF ni pamoja na kusimamishwa kazi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanazibar (ZEC), Jecha Salum Jecha, ZEC kutangaza matokeo ya majimbo tisa yaliyohakikiwa na kumalizia kuhakiki matokeo ya majimbo 14 yaliyobaki na kutangaza matokeo, vyama vya CCM na CUF kufanya mazungumzo na kukamilisha taratibu za kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kurekebisha mfumo wa uchaguzi Zanzibar.
Suluhu ya kudumu inawezekana Z’bar?
Katika andiko lake, The Zanzibar Conflict: A search for Durable solutions, Professa Gaundence Mpangala, wa Chuo Kikuu cha Dra es Salaam, anasema kuwa suluhisho la kudumu la mgogoro wa Zanzibar linapaswa kushughulikiwa katika ngazi ya chini na ya juu (micro and macro levels) na kuchukua hatua za kujenga jamii ya kidemokrasia iliyoendelea.
“Katika ngazi ya chini Muafaka I na II lazima utekelezwe pamoja na mapendekezo mengine. Wadau wengi wanaona muafaka II umetekelezwa kikamilifu, lakini hiyo haitoshi kuhakikisha suluhisho la kudumu kwa mgogoro wa Zanzibar na kujenga amani ya kudumu. Hii ni kwa sababu muafaka huo ulijikita katika masuala ya uchaguzi zaidi. Jamii ya Zanzibar lazima itazamwe kwa uhalisia na kwa upana zaidi. Suluhisho lazima litazamwe kuhusisha masuala kama Muungano, uongozi, utawala wa sheria, elimu, ikiwemo ya uraia, na hali ya maendeleo ya kiuchumi,” inasema sehemu ya andiko hilo.
Njia nyingine ya kumaliza mgogoro
Katika mahoajiano yake na Raia Mwema, Zitto amesema namna nyingine ya kumaliza mgogoro huo ni kwa pande mbili kukubaliana kuongoza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kugawana vipindi vya miaka miwili na nusu kila chama.
“Maana yake hii ni kwamba matokeo ya wawakilishi yaheshimiwe, kwa sababu yalikwishatangazwa, na tume haina mamlaka ya kufuta matokeo yaliyotangazwa, Wawakilishi wakubaliane katika hili na iitishwe referendum (kura ya maoni) na wananchi waridhie, baada ya hapo CUF waongoze miaka miwili na nusu na CCM hali kadhalika,” alisema.
Hata hivyo alisema hilo litakuwa suluhisho la muda tu kwa kuwa litakuwa suluhisho la wanasiasa kama ambavyo imezoeleka, lakini suluhu ya kudumu ya matatizo ya Zanzibar ni kutafuta suluhisho la jamii ya Wazanzibari.
Matumaini ya muafaka shakani
Yale matumaini waliyokuwa nayo Wazazibari kuhusu mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea kutafuta muafaka wa mgogoro wa kisiasa visiwani, yaliingia doa juzi baada ya Maalim Seif kujitokeza hadharani na kuweka msimamo wa chama chake kuhusu hali hiyo.
“Hoja ya kurudia uchaguzi haina uhalali, haina msingi na ni chachu ya kuiweka nchi katika utawala usiokuwa halali na kusababisha fadhaa kuwa kwa wananchi. Ni hoja ambayo inaweza kuzaa fujo na vurugu katika nchi na kupelekea mzozo mkubwa zaidi wa Kikatiba na kisheria,” alisema Maalim Seif.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Maalim Seif alimshutumu Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, kwa kuhujumu juhudi za utafutaji wa ufumbuzi wa haki na wana CCM Zanzibar kwa kauli zinazoashiria kujiandaa na uchaguzi wakati mazungumzo ya kutafuta muafaka yanaendelea.
Akijibu tuhuma hizo za Maalim Seif, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema chama chake kilihamasisha wanachama wake na wananchi kwa ujumla kujiandaa na uchaguzi kwa kuzingatia tangazo za ZEC la kufuta uchaguzi na kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio, huku akimshutumu Maalim Seif kuwa ameingia kwenye mazungumzo hayo siyo kwa nia ya dhati.
“Yako mambo hayasemwi, Seif alijitangazia ushindi akijua ni kinyume cha sheria, alipojua ameteleza akakimbilia kwenye mazungumzo ili kuepuka kushtakiwa,” alisema Vuai alipozungumza na Shirika la Utangazaji la Ujerumani mapema wiki hii.
Hatua hiyo ya Maalim Seif, inairejesha Zanzibar katika hali tete ya kutojua hatma ya muafaka wa mgogoro huo wa kisiasa visiwani humo, baada ya uchaguzi wa Oktoba 25 kufutwa.
Source: Raia Mwema