Zitto: Inawezekanaje Serikali ikasaini mkataba wa shilingi Trilioni 7 kujenga Reli na vifaa vyote vikatoka Uturuki?

Pia ni vizuri kujiridhisha na alichokizungumza huyo zitto..inawezekana kaamua tu kuongea.maana ndicho kilichobakia sasa..
Lakini hata ikiwa ni kweli basi ilikuwa vizuri kujua terms za mkataba..pengine hata suala la ubora wa malighafi limehusishwa..
Kama Magu alimzuia dangote kuagiza makaa ya mawe afrika kusini na badala yake atumie yaliyopo tz asingeshindwa kuzuia utumiaji wa malighafi inayotoka Nje ya Tanzania..kama ni kweli na kama hakuna terms zozote au sababu yoyote
 
Ndo maana mwlm nyerere alisema "mmenipa madaraka makubwa sana anaweza akatokea rais mwingine....."
Hakupewa hayo madaraka alijipa yeye na washauri wake na kituachia urithi wa hayo madaraka sasa ndo yamepata mtumiaji
 
zitto huwa hakosei ila the way avowasilisha hoja zake ndio inakuwa haina tija...kwa nin hakushauri kabla ya mkataba kuafikiwa....amesubir sasa ndo anakuja kusema akati alikuwepo toka awali...hapo ndipo nawachkia wanasiasa tu...yaan wapo tayar kukuacha ufanye vibaya sehem ili wataftiepo kiki.
 
Tunakusaidia, uliza swali kwa waziri mhusika BUNGENI , sisi uraiani HATUNA JIBU!

Kwa taarifa yako siku hizi mijadala huru iko huku mitandaoni. Huko bungeni ni kwenda kutekeleza taratibu tu. Huku ndio uchambuzi halisi hufanyika ukiachia vijembe na lugha za kejeli hapa na pale. Huku mitandaoni kuanzia rais, mawaziri; wabunge nk hushinda. Bungeni utasikia muheshimiwa waziri majibu kwa kifupi kutokana na muda!!

Huku mitandaoni ndio unapewa ukweli wako hata na wale unaodhani wanakuunga mkono. Wale wote wanaogopa kukosoa waziwazi huko kwenye baraza na bungeni ndio wanaofunguka huku mitandaoni.
 
Ndugu yangu zito kabwe hawawezi kukuelewa phd za makaratasi tu...mambo haya yanafanywa kisiasa tu ndugu zitto...labda tusubiri ajitokeze mtu wa serikal "alieelimika" akujibu hoja yako hii nzito
 
Back
Top Bottom