Zitto: Inawezekanaje Serikali ikasaini mkataba wa shilingi Trilioni 7 kujenga Reli na vifaa vyote vikatoka Uturuki?


Francis12

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Messages
7,020
Likes
18,808
Points
280
Francis12

Francis12

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2016
7,020 18,808 280
Anaandika Mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe.

Jambo moja linanisumbua sana. Nisaidieni tafadhali

Inawezekanaje Serikali ikasaini mkataba wa shilingi Trilioni 7 kujenga Reli bila kuweka vifungu vya kufungamanisha na sekta nyengine nchini? Yani kweli hata misumari ( screws) nchi hii haiwezi kutengeneza mpaka iagizwe kutoka Uturuki?

Yani hata kampuni ya kuchimba kokoto itoke Uturuki? Hivi Viwanda vya Chuma nchini vinafanya kazi gani sasa? CTI, TPSF nielezeni hili, hamuwezi kuzalisha kitu chochote kulisha ujenzi wa Reli ya Kati ya SGR? Katika BOQ ya Mradi wa SGR, hamna muwezalo? Serikali iliwapa BOQ mkashindwa? Ukiwauliza watu wa Wizara hawana majibu, wanasema Mkataba ali negotiate Rais mwenyewe. Inawezekana kweli? Siwezi kumwuliza Rais. Anasema sisi kazi yetu kukosoa tu. Amekasirika. Siwezi kumwuliza mtu aliyekasirika, tena Amiri Jeshi Mkuu.

Wakati wa Mdororo wa Uchumi Asia mwaka 1997-1998 Waziri Mkuu wa Malaysia Tun Mahathir Mohammed alifanya miradi mikubwa sana ikiwemo kujenga Mji Mpya, barabara kubwa na Jengo la Petronas. Kwanini? Ili kuingiza fedha kwenye uchumi na kuchochea shughuli nyengine za uchumi na kukuza mahitaji ( aggregate demand). Malaysia ikawa nchi ya kwanza kuibuka kutoka Asian Financial Crisis.

Sisi Watawala wetu wamekwenda madarasa tofauti na kusoma vitabu tofauti vya Uchumi? Unajenga Reli kwa pesa yako ( inavyodaiwa), kwa hiyo unakusanya kodi kutoka kwa watu wako, unanunua US$, unamlipa Mkandarasi. Mkandarasi ananunua kila kitu kutoka nchini kwao Uturuki, mataruma ya Reli, Chuma, Screws na Misumari na hata mchimba kokoto Mturuki. Kwenye uchumi hii inaitwa leakages. Uchumi wetu unahitaji more inflows.

Unajengaje Reli kwa kutumia Chuma kutoka nje the wakati una hazina ya chuma Ludewa? Unamwaga TZS 7 Trilioni bila kuhakikisha offsetting? Natamani kuiona hiyo BOQ ya Reli ya Kati.

Hili linanisumbua sana. Siamini kuwa watawala waliokwenda shule na wenye uzoefu Serikalini hawakuona faida kubwa ya offsets. Baraza la Mawaziri limejaa PHDs, kweli wameshindwa kuona hili? Fedha zetu wenyewe tunatengeneza ajira nje? Kwamba sisi tuwe vibarua tu na wagonga reli? Trilioni 7 zingechochea sana uchumi ( multipliers).

Tunaambiwa sisi tupo negative mno. Hebu watetezi wa Serikali, mnaojua kuitafsiri Serikali, nisaidieni.

Hili mnaona lipo sawa?
 
I

ikigijo

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Messages
581
Likes
539
Points
180
I

ikigijo

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2017
581 539 180
ZOTE zilizoandikwa humo ni point tupu lakini inategemea na mkataba unasemaje, hakuna aliyeuona. Huenda moja ya makubaliano ni hayo na namna ya kulipana nk hivyo siwezi kuhukumu bila kujua mkataba wa kujenga hiyo Reli umesemaje.

Na mkataba una mambo mengi sio kujenga tu kuna mpaka namna ya kulipana, wafanyakazi nk

I will remain neutral, no comment kwasababu sijui upande mwingine wa Mkataba ukoje...
 
Job K

Job K

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Messages
8,207
Likes
4,346
Points
280
Job K

Job K

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2010
8,207 4,346 280
Ukanda wa kati Singida, Dodoma, tabora, shinyanga hadi mwanza kuna mawe ya kutosha. Kwanini kampuni za ndani zisifanye kazi ya kuzalisha kokoto ?
Tena siyo hivyo tu Mkuu, TRC wenyewe wakikuwaga na mashine zao za kuponda kokoto! Basi hata kama hizo zao zimekufa kwanini wasimpe hata Nyanza contractors akawauzia hizo kokoto? Wachumi wetu wachumia tumbo wanaogopa kuhoji na kushauri wasije wakatumbuliwa! Nimkojoleeeee naaaaaniiiiii?
 
Mushi92

Mushi92

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Messages
3,598
Likes
2,158
Points
280
Age
28
Mushi92

Mushi92

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2013
3,598 2,158 280
Ndugu peleka hii hoja bungeni. Nadhan hamjaidhinisha hyo fedha Bali katoa as if ananunua mboga ya familia. No negotiations at all. Anasemea tuu kwenye mikutano.
Peleka bungeni ikibidi mumwekee mipaka. Maana mambo mengi haanzii bungeni.
 

Forum statistics

Threads 1,235,412
Members 474,534
Posts 29,221,235