Uchaguzi 2020 Zitto: Ilani ya Uchaguzi ya CCM inafanana sana na Thesis ya PhD ya Mafuta ya Korosho

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Mar 26, 2019
2,338
5,263
Inawezekana Mwandishi ni mmoja..
IMG_20200901_104806.jpg
 
Tangu ilivyodanganya ajira mara milioni 7 Mara 8. Nikaona tunazugwa. Huyu jamaa anahangaika na ndege za mizigo. Mizigo gani hiyo kama sio akina Mr Slow
 
Kwa sababu sijaisoma siwezi bisha. Ila kuna mijitu haijasoma inambishia Zitto. Daaah akili za wapi sijui
 
Kwahiyo kumbe mpaka ilani ya chama iliandikwa na yule bwana mfupi mwenye kipara kutoka mapolini chato.
 
Hata kama ingekuwa na pages 1000 bila kutuambia ya 2015 ilitekelezwa kwa % ngapi yatabaki kuwa makelele tu
 
Inawezekana Mwandishi ni mmoja..
View attachment 1555232
Hiyo inaongea facts.

Kikubwa kilichoandikwa, serikali iliwajibika vipi kwa kuonyesha matokeo halisi. Ni matokeo makubwa sana lazima Ilani iwe kubwa.

Kisha inaonyesha mikakati na ahadi za matokeo makubwa zaidi. Ni ilani ya kisayansi na uhalisia. Msanii kama Zito lazima atamke ni boring, sababu anapenda kurubuni watu na fancy words kama "Kazi na bata".

Nilitegemea akosoe yaliyomo kwa hoja badala ya lugha za kubeza. Na ukiona hata Zito mzee wa kudanganya watu kwa tafsiri fake za takwimu ameshindwa kufanya hivyo, ujue Ilani imeandikwa kitaalamu, tena na serikali yenye uzoefu wa utendaji.
 
Back
Top Bottom