Zitto, Hongera kwa kuchokonoa KIA na Mengineyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto, Hongera kwa kuchokonoa KIA na Mengineyo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPadmire, Jul 1, 2009.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Leo Mh Zitto Kabwe ameanza hotuba vizuri, kwa kusema kuwa barabara hazijengwi kwa hela za chama chochote cha siasa bali kwa kodi za wananchi.

  Pia Zitto ameongelea suala la KADCO ambao wanaendesha Kilimanjaro International Airpoirt (KIA). Ni aibu sana kwa wageni wengi wanaokuja kutembelea Tanzania kupitia Nairobi. Sio siri wageni wengi wanaotembelea Tanzania wanapitia Kenya. Sababu kubwa wageni kupitia kenya ni nauli kubwa kwa wageni kama wakitua KIA ukilinganisha na wakitua Nairobi.

  Mfano, Kama mgeni akisafiri kutoka Amsterdam akitua KIA atalipa dola 1305 EURO ROundtrip wakati akitua kenya ni 600 Euro Roundtrip. Na ni kwa KLM (Royal Dutch Airlines). Sidanganyi, Naomba ucheck kwenye KLM.COM website na uangalie hizo nauli mwenyewe.

  Huo ni mfano rahisi, angalia ndege nyingine kama virgin Atlantic, na mandege mengine mengi.

  Wageni wakifika nairobi wanalala night moja na kesho yake wanakuja na daily bus shuttles. kama wadau mnataka kuhakikisha nendeni Arusha pale Namanga border, shuttles BOBBY Shuttle, River side, DAVANU, OTTA, n.k Hawa wote wana mabasi mengi na wastani wa mabasi 4 kwenda nairobi na 4 kuja Arusha.

  Kwa hiyo hoteli za Kenya zinafaidi, curio shops, national parks, beaches.

  Landing fee KIA ni tatizo; landing fee ni 5000 US $ per day. Wakati KADCO wanalipa 1000 US $ per year.

  Mie ninashaka KADCO ina mikono ya VIGOGO wa CCM. Please nendeni BRELA muwaanike hapa tujue.
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  KADCO ni sooo sana wanatuibia live.... lakini sio hapo tu kila kona hii nchi inatakiwa ipigwe chini utawala wa kiraiaa maana naona uhuru wao wanautumia vibaya hata wanachafua geshi na ufisadi huku pesa wamepiga wao wanasiasa ni aibu sana hata kwa geshi letu..........
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ndiyo maana nampinga Zitto kujiondoa kuto kugombea tena hata kama uamuzi ni wake, maana Bunge litakosa uzito wa Zitto. Issue ya KADCO inafahamika na hakuna wa kuigusa ila utasikia rais anasema visa zipungue. Visa hazisaidii wageni kuja. Waache longo longo.

  Hongera Zitto wacha tuone Pinda atakuvaa kwa lipi tena.
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Duu, yaani hadi mwakani tutasikia sana. Halafu Pinda alikuwa akijisifu kuwa Serikali imejenga, wakati huo wao ndiyo wanasaidia kuiba Tanzania iibiwe vyanzo vyake vya pesa. Yaani Kilimanjaro IA inakosa ndege hadi wakaikodisha eti kwa dola 1,000/ Huu ni upuuzi wa hali ya juu. Wanakomba Bandarini, TRC, TANESCO, DAWASCO, BoT, NBC, kwenye madini, mbuga za wanyama, hadi airport.... Na sasa hata Dar Aiport itauzwa hivi karibuni. Wanafanya uzembe ili ionekane tumeshindwa kuendesha na baadaye wanaziuza kwa bei chee au kuuziana wenyewe. Wee Mkapa miaka yote umekuwa mtu wa ofisini na leo eti unakuwa MFANYABIASHARA wa kiwanda cha Makaa ya mawe na kufua umeme, hihiiiii Mjasilimali my A**. Yaani hadi unapata raha. Ngoja nikimbie maana ntaandika kabila langu hapa ili nimtukane Mmakonde, na Masatu atakuja na maneno kuwa ninam-boa.....
   
 5. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii ni hatari sana kwa Taifa letu kama tunakuwa na gharama kubwa sana katika viwanja vya Ndege, na Kijographia, Kilimanjaro ipo sehemu nzuri zaidi ya Kenya na ndio maana Kenya wanatumia nafasi hiyo kusema kuwa Milima Kilimanjaro upo Kenya.
   
 6. A

  August JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hii inafaa wabunge wapande zote washirikiane tumjue mchawi wetu alikuwa nani na ni nani mpaka sasa hivi. na hatua zifaazo zichukuliwe dhidi ya hao waliotuingize mkengee au tutaambiwa na masuala ya Jeshi/usalama wa Taifa?
   
 7. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama kweli tunataka maendeleo ya kweli utafanya mambo ya kuongeza support kwa wale makamanda wa vita yani ni Chadema
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nafurahi kwamba Zitto na Slaa siyo wana ccm maana kama wangelikuwa huko tungekuwa tushawazika loong time.

  Serikali inataka kusifiwa wakati ndiyo kinara cha kuvunja sheria nchini.
  Tukianzia ubadhirifu = viongozi wa serikali,
  maadili yaliyoooza = viongozi wa serikali,
  dili chafu za ukwapuaji kodi za wananchi = viongozi wa serikali
  kuisaliti nchi (ugenishaji) = viongozi wa serikali
  uonevu wa raia kupitia vyombo vya dola = viongozi wa serikali
  UBAKAJI wa uhuru wa kupata habari = viongozi wa serikali
  majibu ya kebehi kwa maswali magumu = viongozi wa serikali
  ahadi za uongo kupitia bajeti = viongozi wa serikali
  kujilimbikizia mali za umma = viongozi wa serikali
  mabilionea wa kutisha = viongozi wa serikali
  wizi wa kura = ccm

  Kama serikali inataka kusifiwa inapaswa kupangusa tongotongo kwanza ijiangalie kwenye kioo ndipo itagundua kwamba worms wanaimaliziamalizia.

  Aaaaaaargh!!! naogopa kuongea kwa ukali nisije nikafungiwa bureee.
   
 9. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu wangekuwa wanalijua hilo tusingefika hapa tulipo, the sad news is, majibu ya hovyo yatatolewa na waziri husika, halafu wataishia kugonga meza CCM, CCM, and thats it!

  I think 2010 inabidi kifanyike kitu, hata kama ni noma na iwe noma!
   
 10. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Haiwezekani! Yaani KADCO wakusanye maelfu ya dola kwa siku halafu wao walipe dola 1,000 tu kwa mwaka? No no no no no no! Hivi inaingia akilini kweli hii? Hata kama ni wizi jamani hii sasa is too much. Jamani CCM wanaimaliza hii nchi. Ama kweli TZ ni shamba la bibi. Eeee MUNGU wa mbinguni ikumbuke Tanzania na mafisadi wakujue wewe ili nchi yetu ipone.
   
 11. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu haijalishi iwe Chadema au nani. Yoyote anaye pigania maendeleo ya nchi na wananchi wa kawaida anastahili support yetu sisi. Nchi haijengwi na mtu au chama kimoja. Kwenye maslahi ta taifa hakuna huyu CCM au huyu Cuf. Hakuna huyu Mzanzibar wala huyu Mbara. When it comes to our dear country kuna huyu Mtanzania mwenzangu and that's all that matters.
   
 12. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  You seem to underestimate mafisadi mkuu wangu. Unakumbuka wale walio kuwa wakitulia milioni 150 kwa siku?
   
  Last edited: Jul 2, 2009
 13. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tatizo uongozi Bongo hauangalii mbali sijui? Kwa sababu watu wanaangalia mapato ya Airport badala ya kuangalia ya hao watalii kulala, kula na kutembelea sehemu zetu (Vivutio) maana ilibidi tuwe tunajifunza kutoka hata kwa hao Wakenya kwamba ni njia gani wanapata watalii zaidi yetu, yaani inabidi tutumie Any means necessary kuhakikisha watalii wanatua na kulala hapa hapa Tanzania.
   
 14. S

  Sandra Member

  #14
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  As far as airline pricing strategies are concerned, it makes sense for KLM to charge more for flights into KIA than they do to NIA. It is obvious that a lot of people going through KIA would be proceeding to either tourist expeditions in Moshi/Ngorongoro/Manyara/Arusha or Arusha town, therefore a direct flight (to a point closest to their destination) would be more expensive than when the airline has to take you round through another destination (on the same carrier or their partners). That is why a ticket is always cheaper if you are roureted via different destinations.

  As for KLM's case, they have a high demand for flights into TZ especially KIA therefore their prices have to reflect such. Also, important to note is that they own part of KQ (Kenya Airways) therefore they can afford to have a price war with them and they may have some agreement in place with the government for some fees (the governement owns a small share of KQ, will have to confirm have much exactly).

  Another reason for Jomo Kenyattas relatively lower landing fees as compared to our TZ airports is that Nairobi is considered a hub of East Africa, with Ethiopia vying for a close second. There are more airlines landing in Nairobi than at Tanzania's airports therefore JKIA is able to charge lower landing fees bcese they have the advantage of volumes which our airports do not, especially KIA which except for KLM, have FEW major airlines landing (ET, SA, some few seasonal european flights...and i standto be corrected coz i have not been monitoring this for a few months)... And note that landing fees are charged per type/weight of the aircraft landing or whether the flight is domestic or international (depending on country & airport) so when an airport has most Precision Air/Zanair/Coastal (small, propeller a/c & domestic flights) at its airports it is bound to charge higher for the bigger a/c since they are so few. Some PW/Zanair landings cost as less as $ 200 or less!

  What we need to do is remind our government that we need to improve our (air) transport infrastructure, overhaul our country's civil aviation authority and promote our country as preferred hub of East Africa.(remember IATA had to suspend TC's license even though TCAA had previously declared them airworthy. TCAA only declared them un-airworthy after ICAO audited them (TCAA) and found that wanawabeba sana TC.) Airport experts tell me that Dar is actually a better ideal airport than JKIA bcse we r at sea level whereas Nairobi is slightly higher, so if from the beginning we had facilitated , built and promoted the infrastructure, Dar would have been a bigger hub than JKIA
   
  Last edited: Jul 2, 2009
 15. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu,
  Hapa una hoja lakini inabidi ukae chini utengeneze hoja nzito yenye data za kutosha baada ya hapo rephrase hiyo post. Ninayasema haya I hope una nondo au access ya nondo.
  Kwa mfano, unaweza ukatafiti rate za landing fees kwa type za ndege na country of registration.
  Pia unaweza ukatafiti kupata ukweli wa malipo ambayo KADCO wanalipa serikalini.
  Kwa kuongezea, unaweza kutafiti matumizi ya ile hangar pale ambayo ninajua ilihamishwa kutoka katika umiliki wa ATC kwenda kwa serikali moja kwa moja na hivyo kukabidhiwa KADCO.
  Unaweza kutafiti, hadi sasa KADCO wameendeleza kwa kiasi gani Uwanja na facilities zingine kwa mujibu wa Mkataba wa ukodishaji wa miaka 25 walioingia na serikali.
  Ukiweza kufanya haya na mengine mengi, utakuwa umesaidia watanzania na hasa wabunge (bila ya kujali itikadi za kisiasa). Nina hakika wabunge wengine hawana taarifa muhimu siyo tu za KIA bali za maeneo mengi sana ya Tanzania.
   
 16. M

  Magezi JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kama CCM wameshindwa na wanaona bora wauze nchi kwa nini tuwafikirie tena??
   
 17. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Zitto hana lolote!he is playing ith people's minds to cleaneth himmself!

  Zitto an njaa tu kama wapinzani wanao hama hama!ndomaana aliitetea final episode ya DOWANS kwa nguvu zake zote

  Zitto is very selfish!

  ZITTO SHOULD STEP DOWN!HE LOOKS LIKE AN ACADEMICIAN,NOT A POLITICIAN
   
 18. M

  Magezi JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Bora yeye anazungumzia mambo ambayo angalau watu tunaelewa. Wewe unalipi na mchango gani kwa umma? Au unamchukia tu, hakuna binadamu asiyekuwa na ubinafsi ila tunatofautian kiwango. Issue ya Dowans kila mtu alishangaa kwa maelezo yaliyotolewa na zitto lakini alivyojitetea kama ni kweli basi huenda msimamo wake ulikuwa tofauti na matarajio yetu. Lakini kuna mambo mengi amesaidia kuelimisha umma mfano buzwagi n.k.

  Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.....!
   
 19. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  1-Tuliwachagua wawakilishi wetu ili kuwe na utaratibu wa kuzungumza,au kutoa madukuduku yetu,SIO KILA MTU AONGEE!

  2-Mategemeo yetu wapiga kura ni wawakilishi hawa kukiwwasilisha kile kinachotokea maeneo tunayoishi walipa kodi,AND NOT OTHERWISE

  3-Kuelimisha buzwagi n.k kama unavyosema ITA HAD TO HAPPEN ANYWAYS.it was the matter of time and opportunity!Zitto ilimkuta hivyo opoortunity akia kwenye form,ofcourse he is honoured!Zitto hakuzaliwa ili aelimishe buzwagi,anybody cn do it!NI SWALA LA EXPOSURE.na zitto anapo pakusemea,na ana nafasi ya kusemea.

  So far,tunao wataalamu wazuri zaidi ya zitto humuhumu jf

  4-Mzimu wa 'dowans' UTAMMALIZA Zitto!uzuri yeye mwenyewe ameshasoma dalili za nyakati.ndo maana anafikiria kupumzika kugombea!sijui wewe mshabiki wake mwenye imani kwamba Zitto alishushwa na mungu kwa ajili ya buzwagi unaamini nini......................
   
 20. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu all I meant to say is that we need to support whoever is against ufisadi without looking at party affiliations. Sawa CCM kuna mafisadi but it will be very unfair to say that anyone and everyone who is CCM ni fisadi. It will be like saying anyone who is in the oposition is against ufisadi. If a person is genuinely against ufisadi I don't care what party they are from but they have my support.
   
Loading...