Zitto, hili swali lako ni zuri sana - lakini umeliuliza ukihitaji nani haswa alete ufumbuzi wake?

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Hapa chini ni swali ambalo Mh Zitto Kabwe ameuliza kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Sina uhakika amelilenga kwa nani lakini binafsi naona si sahihi kwa ACT, Chadema na/au vyama vingine serious vya upinzani kuuliza swali hili in the first place.

In fact, ni sisi wananchi ndiyo ambao kwa miaka kadhaa sasa (kama si miongo) tumekuwa tukiwauliza ninyi viongozi mnaotuwakilisha katika crusade hii na bado hatujapata jawabu.

Sasa wananchi tunaanza kuwa puzzled na kupata wasiwasi mnapoanza kuturudishia swali letu kihivi. Tulitegemea tupate sauti ya mkakati mahsusi kutoka kwenu inayotoa mwongozo wa haswa sisi wananchi tushiriki vipi kivitendo katika kuufanikisha mkakati mtakaouleta mezani.

Msiishie mathalani kutuhimiza tu kuwa tujitokeze kwa wingi sana kupiga kura October. Hiyo pekee haitoshi kama mkakati kwani kwa mfumo tulio nao, wanaoamua ni nani ashinde uchaguzi ni watangaza matokeo na si wapiga kura. Tunahitaji kusikia kutoka kwenu suluhisho la hii kitu na mwongozo wenu kwetu wananchi vile mwataka tufanye.

Tunahitaji tangible solution.

20200607_134133.jpg
 
Naungana na wwe! Upinzani wa kweli ndio wa kutoa majibu. Kwa Tanzania wananchi ni "takataka" hatuna jibu! na hasa katika msuli wa Jiwe aided by police, mahakama and bunge!
 
Kwani huo upinzani hautokani na wananchi?!
 
Hii mada pana sana.

Tatizo hasa linaanzia kwenye jamii, na ni tatizo la jamii yote kama Zitto alivyoandika hayo makundi hapo juu.

Watanzania tumegawanyika kulingana na kada zetu; kuanzia wasio na elimu mpaka wenye elimu. Halafu tena tunasogea mbele kuanzia wenye elimu ma jobless, mpaka wenye elimu wenye ajira.

Hivyo tatizo la kundi moja, linaonekana haliwahusu kundi jingine, kumbe hilo kundi jingine nalo lina tatizo lao tofauti, tuna ubinafsi fulani. Mfano. wakati walimu wanalia mishahara midogo, hawapandishwi madaraja, wakati huo huo kuna ma- jobless wanaolia hakuna ajira.

Mpaka siku tutakapoamua kuungana wote kwa pamoja, bila kujali matatizo yetu ambayo kimsingi hayafanani, tuache kila mtu kulilia shida yake binafsi na kupuuza ya mwingine, ndio tutapiga hatua kama taifa ya kumfukuza mkoloni mweusi nchi hii.

Mababu zetu waliungana kwa umoja wao kumfukuza mzungu, bahati nzuri kwao adui alikuwa mmoja, na hawakuwa na matabaka miongoni mwao kama sisi; -adui mzungu: sisi leo hii kila mmoja ana tatizo lake binafsi, lakini lililoletwa na adui mmoja- mkoloni mweusi.

Tuungane kujikomboa, kuwaachia viongozi wa upinzani peke yao watupiganie wakati matatizo zaidi ni ya kwetu, tunakuwa hatuwatendei haki hao viongozi kwa uchache wao, wala hatujitendei haki sisi binafsi kwa wingi wetu.
 
Platform ya kusema ukasikika wanayo wapinzani wa kweli.... kwa hali ya sasa wananchi wa kawaida ni vigumu.
Ukiishia kutaka kupewa nafasi ya kusema na kusikika tu bila kufanya kitendo chochote cha kuchochea wewe binafsi upewe ukitakacho hutakaa upewe unachotaka, kusema na kusikika hakutoshi tumesha prove hilo mara nyingi, we need to move to the next stage.
 
Dictators never heed to words! They need action and preferably mechanical ones!
 
Hapa chini ni swali ambalo Mh Zitto Kabwe ameuliza kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Sina uhakika amelilenga kwa nani lakini binafsi naona si sahihi kwa ACT, Chadema na/au vyama vingine serious vya upinzani kuuliza swali hili in the first place.

In fact, ni sisi wananchi ndiyo ambao kwa miaka kadhaa sasa (kama si miongo) tumekuwa tukiwauliza ninyi viongozi mnaotuwakilisha katika crusade hii na bado hatujapata jawabu.

Sasa wananchi tunaanza kuwa puzzled na kupata wasiwasi mnapoanza kuturudishia swali letu kihivi. Tulitegemea tupate sauti ya mkakati mahsusi kutoka kwenu inayotoa mwongozo wa haswa sisi wananchi tushiriki vipi kivitendo katika kuufanikisha mkakati mtakaouleta mezani.

Msiishie mathalani kutuhimiza tu kuwa tujitokeze kwa wingi sana kupiga kura October. Hiyo pekee haitoshi kama mkakati kwani kwa mfumo tulio nao, wanaoamua ni nani ashinde uchaguzi ni watangaza matokeo na si wapiga kura. Tunahitaji kusikia kutoka kwenu suluhisho la hii kitu na mwongozo wenu kwetu wananchi vile mwataka tufanye.

Tunahitaji tangible solution.

Jamii zetu ziko dhaifu sana katika kupambana kupata maisha bora. Hatujawekeza vya kutosha katika kujenga jamii imara zenye uwezo wa kukabili hali duni ya maisha. Kuna mambo mengi ya kuthibisha udhaifu huu mfano bidhaa nyingi za viwandani tunazotumia hapa kwetu kwa asilimia kubwa zinatoka nchi za nje na hakuna mpango thabiti wa kuweza kuzitengeneza wenyewe (hapo ndio chanzo cha ukosefu wa ajira)

Tumeshindwa kama taifa kuwajengea uwezo wananchi wake ili wawe wabunifu na wachapa kazi. Kwa kuwaacha wananchi walio wengi kuishi holela bila kuwa na mfumo jumuishi wa kiuchumi lazima umaskini utaendelea kutamalaki na kuzalisha taifa la mazuzu.

Elimu yetu mbovu, inaishia kufundisha watu kusoma na kuandika wala si kuwapa uwezo wa kuwa wabunifu wa kukabili matatizo yanayo zikumba jamii zao. Tuchunguze udhaifu wa elimu yetu na kuifanyia marekebisho.
Uhuru wetu ni wa maneno na si vitendo hivyo hauwezi kuzalisha raia wabunifu.
Land son Tz
 
Naungana na wwe! Upinzani wa kweli ndio wa kutoa majibu. Kwa Tanzania wananchi ni "takataka" hatuna jibu! na hasa katika msuli wa Jiwe aided by police, mahakama and bunge!
Hata police,mahakama na bunge nao ni watanzania,wote ni takataka maana madhira aliyoyataja jiwe nao yanawafika au kuwafika ndugu zao Ila wanapumbazwa na vimishahara vya laki tatu laki nne,Kama taifa tunashida kubwa sana
 
Kuna uhakika gani kwamba tukienda kupiga kura hazitaibiwa?

Baada ya uchaguzi mdogo ambao wapinzani waliugomea kwa sababu za kuwepo fouls za Tume ya Uchaguzi kwa kushirikiana na CCM, kuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika?
 
Watanzania wengi tumekatishwa tamaa na wanasiasa.
Wewe unakomaa kwelikweli na unajitoa kwa nchi yako na mshahara wa laki nne kwa mwezi, mwisho wa siku mbunge anataka aongezewe posho ya laki tatu kwa siku na asikatwe kodi (acha mengine). ghafla anamiliki hamma, hujatulia ana shamba la milioni mia saba mtwara
Niambie hapo utaanzia wapi kuungana naye akija kukushawishi mdai democrasia ya kuongea na kuandamana
 
Wananchi wan
Naungana na wwe! Upinzani wa kweli ndio wa kutoa majibu. Kwa Tanzania wananchi ni "takataka" hatuna jibu! na hasa katika msuli wa Jiwe aided by police, mahakama and bunge!
Wananchi wanaweza wakiwezeshwa kwa kupewa elimu ya uraia na kutambua thamani ya kura haya moja,kupiga kura kwa wing I kuwakataa wadhalimu,kuzilinda hadi kieleweke.Bila hivyo Mh.Zitto na wengine hawawezi peke yao bila support ya Wananchi wenyewe ambao ndiyo wahanga wa udhalimu.
Tukiamua tunaweza,Mimi sijawahi na sitaishi kuwapigia kura wakoloni weusi.Wewe je,unasimama upande gani?
 
Naungana na wwe! Upinzani wa kweli ndio wa kutoa majibu. Kwa Tanzania wananchi ni "takataka" hatuna jibu! na hasa katika msuli wa Jiwe aided by police, mahakama and bunge!
Hao wapinzani wakitoa matamko ya kukemea huo ukandamizaji hamuwaoni wanavyolundikiwa makesi ya uchochezi??
Huko bungeni wapinzani hamuwaoni wakikosoa huu utaratibu batili wa CCM tena muda mwingine hupelekea kufukuzwa bungeni na kuitwa kwenye vikao vya maadili tena wengine hotuba zao hufutwa na kunyimwa nafasi ya kuzisoma bungeni.

Je wananchi ambao ni wapiga kura wamechukua hatua gani???

Maandamano ya mara ya mwisho alijikuta mange mwenyewe akindamana ughaibuni wakati watanzania wanakenua meno mitandaoni.

Wapinzani wameplay part yao wameishia kufilisiwa, kubambikiwa kesi, kupotezwa nk.

Huu mzigo ni wa wananchi, mmewaachia wanasiasa wawasaidie kudai katiba mpya nyie mmelala usingizi wa pono.
 
Hapa chini ni swali ambalo Mh Zitto Kabwe ameuliza kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Sina uhakika amelilenga kwa nani lakini binafsi naona si sahihi kwa ACT, Chadema na/au vyama vingine serious vya upinzani kuuliza swali hili in the first place.

In fact, ni sisi wananchi ndiyo ambao kwa miaka kadhaa sasa (kama si miongo) tumekuwa tukiwauliza ninyi viongozi mnaotuwakilisha katika crusade hii na bado hatujapata jawabu.

Sasa wananchi tunaanza kuwa puzzled na kupata wasiwasi mnapoanza kuturudishia swali letu kihivi. Tulitegemea tupate sauti ya mkakati mahsusi kutoka kwenu inayotoa mwongozo wa haswa sisi wananchi tushiriki vipi kivitendo katika kuufanikisha mkakati mtakaouleta mezani.

Msiishie mathalani kutuhimiza tu kuwa tujitokeze kwa wingi sana kupiga kura October. Hiyo pekee haitoshi kama mkakati kwani kwa mfumo tulio nao, wanaoamua ni nani ashinde uchaguzi ni watangaza matokeo na si wapiga kura. Tunahitaji kusikia kutoka kwenu suluhisho la hii kitu na mwongozo wenu kwetu wananchi vile mwataka tufanye.

Tunahitaji tangible solution.

Zitto, kama viongozi wengine wa kisiasa, na hata wamiliki wa vyombo vya habari, hawawezi kutoa jibu kwa sababu ni tuhuma za uzushi ili wapate kusikiliwa na Mataifa ya nje.

Kama kuna mapungufu katika hayo aliyoyataja, ni mapungufu yatokanayo na Kikatiba, Kisheria, Kanuni na Taratibu. Zitto, kama mbunge, anapaswa kuwasilisha hoja ya mapitio ya Katiba, Sheria na hata Kanuni, zirekebishwe kukidhi mahitaji ya leo na kesho, na siyo kulalamika mitandaoni.

Najiuliza kwa sauti Je, iwapo hao viongozi wakipewa ridhaa na wananchi kuongoza nchi hii, hawataendeleza tabia ya kulalamika nchi ikiporwa au kukandamizwa na mataifa ya nje?
 
Rasimu ya katiba mpya ililetwa ili kuondoa huu upuuzi, CCM baada ya kuona hali yao ya utawala iko hatarini wakamtoa Spika Sitta wakamuweka Chenge alinde maslahi yao, matokeo yake lile bunge la katiba likafia pale.

Wewe sijui una mawazo ya wapi; habari ya mataifa ya nje hapa inaingiaje? hamjiamini, mmeshadumaza akili zenu kuwaza kila anaekemea uovu wa nchi hii anatumwa na mzungu!.mna mawazo mgando yasiyoelezeka.

Tatizo la ukosefu wa ajira, walimu kutopandishwa madaraja, uhuni wanaofanyiwa wapinzani, na mengine ni tuhuma za uzushi hizo? wake up man.
 
wanaoamua ni nani ashinde uchaguzi ni watangaza matokeo na si wapiga kura.
Watu wa Kituo fulani wakiamua kulinda kura zao na kuwa karibu wakati wa kuhesabu na kutangazwa matokeo,huwa hakuna mwizi atakayethubutu kutangaza kinyume cha kilichopo kwenye sanduku la kura.

Mkakati huu umezaa matunda kila pale wananchi wanapoamua kujitolea na kusimamia mabadiliko ya kweli.

mbona hili liko wazi? kila mwka na kila pahali wapinzani waliposhinda ,msuli ulituna dhidi ya wizi wa kura na kupindua matokeo.

Tujuwetuu sheria za Uchaguzi nakufuata kanuni na kuwa makini na IMARA ( Kichwa ngumu hadi kieleweke)
 
Back
Top Bottom