Zitto hawezi kuja kanda ya Ziwa na hasa Musoma kwa kuwa nimemweka mfukoni -N.Mkono

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Jana alizikwa Kiongozi wa Chama cha CUF ndugu Julius Masaka anayesemekana kupewa sumu kwa sababu za kisiasa jimboni hapa .katika mazishi haya yaliibuka malalamiko ya kwa nini Zitto ambaye amengojewa sana kanda ya Ziwa na hasa Musoma na Buzwagi kwenyewe hajafika kuwaelezea kilicho mfika Bungeni .Watu walianza kusema Zitto safi ana tetea Taifa lakini wanashangaa kwa nini haji Musoma , Buzwagi na Tarime kuliko machimbo .

Ndipo wakaja watu wanaodai kuwa na ushahidi juu ya Zitto kusemekana kapewa kitu kidogo na mkono kwamba asifike huku . Nikiwa hapo msibani nilisimama makaburini na kuelezea kwa jinsi navyo mjua Zitto yuko busy na Musoma na kwinginek atafika .

Nilitaka kuuawa pale maana wanasema Mkono na wana CCM wote wanasema Zitto hatakuja maana wamesha malizana naye . Kwa kuwa mimi si msemaji wa Zitto , na kwa kuwa hapa ndipi tunako kata issues nimeona nije hapa kutoa habari hii ili Zitto ajibu tuhuma hizi.Kwa kifupi wanakata tamaa for a long waiting ya wewe ndugu Zitto kufika huku na wanaanza kushangaa kwa nini wakati wote wana madini na wanataka kujua ukweli wa yaliyo kupata ukiwa Bungeni .Ujumbe nimesha ufikisha kwako tafadhali wasiliana na watu wa Musoma na kanda ya Ziwa wanaelekea kuto kuelewa kwa nini Chadema hawafiki kuelezea mambo haya .
 
Thats Lunyungu at his best! u can foul some people sometimes, but not all people all the time... teh teh teh....
 
Mkono asilete longolongo hapa,anafahamu fika wakazi wa Mara huwa ni watu wenye msimamo mkali,tena wepesi kufanya changes katika nyanja ya kisiasa,kumbukeni uchaguzi wa 1995,majimbo ya Bunda,Musoma vijijin,Mwibara na Ryorya yalichukuliwa na upinzani.Mbunge wa sasa wa Tarime ni wa Chadema,hata halmashauri ya Tarime inaongozwa na Chadema.Musoma mjini uchaguzi wa 2000 na 2005,Bwana Wandwe huwa anafanyiwa rough mbaya sana na CCM,binafsi nilishuhudia uchaguzi wa 2000 musoma mjini,upinzani ilishinda lakini matokeo yalibadilishwa,muulizeni Wandwe.

Zitto tunakuomba ukipata nafasi tembelea Mara,kule kuna wanamapinduzi wengi tu,hawataki michezo michafu,pia usisahau wakazi wa Buzwagi wanakuhitaji sana.
 
Mwenyekiti wa kamati ya mazishi ya Julius Masaka alikuwa Chacha Wangwe mbunge wa Tarime. Kama kulikuwa na mtu mwenye maswali hayo angemuona mbunge huyo ambaye yuko karibu na Zitto. Hata hivyo penye wengi pana mengi, na mimi pamoja na kuwa miongoni mwa umati mkubwa uliomsindikiza ndugu yetu huyu, nashangaa kuyasoma haya hapa.
 
Nimetokea Mugumu leo masaa mawili yaliyopita, kwa wachache niliyoongea nao kwa siku 5 nilizokuwepo kule wamechoshwa na ccm labda wako tayari kusikia wapinzani wana yapi ya kusema? hivi kwa nini hawa wapinzani wasijaribu kuona kuna nini huko na waende kwa umoja na sio kichama chama.
 
Back
Top Bottom