Zitto hana chama, chama ni cha Wapemba na wafuasi wa Maalimu Seif

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
ACT - Wazalendo haina wanachama wala jengo la ofisi inalomiliki Bara. ACT inategemea nguvu ya wanachama kutoka Zanzibar wengi wakiwa ni wale waliokuwa wafuasi wa CUF- Maalimu Seif.

ACT -Wazalendo haina Jengo la Chama kwa maana ya umiliki, jengo walilopewa na Maalimu Seif Foundation ni lile walilokuwa wanatumia waliokuwa Wabunge watiifu wa Maalimu Seif, linamilikiwa na familia ya Seif.

ACT Wazalendo haina mtandao Bara mtandao wake uko Zanzibar. Kwa mtu makini ataelewa hapa mwenye nguvu ya chama ni nani kati ya Zitto, Wazanzibari na familia ya Seif.

Siku wenye chama chao wakiamua kuondoka na jengo lao chama kitakufa Zitto atabaki na makaratasi ya Msajili wa vyama vya siasa tu. Jifunze kutoka kwa Lipumba na CUF yake.

Najua wafuasi wa Zitto hawapendi kusikia haya lkn, Ukweli ndio huo.

Zitto and others, Keep this short Thread you will thank me later.
 
Zitto inatakiwa akae kwa kutulia, lakini akivimbisha kichwa yatamkuta kama yaliyomkuta NAPE eti kuwa anaijua sana CCM kuliko yeyote na akaliwa kichwa akarudi kwa magoti.
 
Siasa zetu za kuchaguana kwa kuangalia sura na mengineyo haziwezi kumfanya Zitto aachiwe makaratasi ya msajili.

Naona huyu ana bahati ya kuachiwa urithi wa wafuasi wa Maalim Seif, hivyo ataendelea kutembea nao mpaka pale naye atakapomuachia kiongozi mwingine huo urithi.
 
Chama chenyewe alikikwapua kutoka kwa Lucas Kadawi Limbu na wenzake. Kisha akawafanyia roho mbaye wenzake akina Kitila na mama Mghwila, wakatimkia ccm. Ipo siku ukweli mchungu utakuwa dhahiri kwake
 
Makaratasi gani bwashee?

58E5854B-E2F8-43DA-A422-5A6C825DBE9F.jpeg
 
Back
Top Bottom