Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Zitto amehoji kwa kirefu juu ya kupanda kwa gharama hizo katika ukurasa wake wa facebook na pia amegusia gharamaa za pasi za kusafiriia za kielekroniniki na kudai kuwa huko teundako kuna giza kuliko tutokako.
=========
Gharama za kitambulisho cha Taifa yapanda kutoka TZS 17,000 mpaka TZS 26,000
Mwaka 2016 Serikali ya awamu ya 5 iliwashitaki watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ( NIDA ) kwa sababu gharama za kutengeneza kitambulisho zilikuwa kubwa mno.
Kamati ya PAC imekuta kwamba menejimenti mpya iliyopewa kazi ya baada kuwatumbua kina Dickson Maimu iliingia mkataba mpya na mkandarasi na kupandisha bei ya kitambulisho kwa shilingi 9,000 zaidi hadi kufikia TZS 26,000 kwa kitambulisho kimoja.
Mbunge wa Tarime vijijini ndg. John Heche ameibua jambo hilo Bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani hakuweza kutoa majibu ya kutosheleza.
Ni dhahiri juhudi za kuficha madudu ya Serikali ya awamu ya 5 hazitafanikiwa na kashfa za ufisadi za Serikali ya awamu ya 5 zitakuwa na madhara makubwa kwa Serikali kuliko inavyofikiriwa.
Jana Zimezinduliwa pasi mpya za kusafiria ambazo tunaambiwa zimeokolewa zaidi ya shilingi 250 bilioni zilizotaka kupigwa. Taarifa kutoka ndani ya Kamati ya PAC inaonyesha kuwa e-passport ni eneo moja tu la mradi wote na hiyo gharama ya USD 57m ni ya eneo moja tu. Kwamba maeneo mengine kama ya e-visa, e-immigration services, e-border nk yana gharama zake. Nataraji CAG atafanya ukaguzi wa manunuzi ya mradi huu wa pasi za kusafiria.
Huko tuendako, kuna giza zaidi kuliko tutokako