Zitto/Filikunjombe wajitosa kuwatetea madereva wa wabunge Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto/Filikunjombe wajitosa kuwatetea madereva wa wabunge Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 24, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  SIRI nzito yaibuka sakata ya Madai ya madereva wa wabunge wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania,yadaiwa wabunge wanaoogoza kuwatimu madereva wao ni wa vyama vya upinzani kikiwemo cha cha Demokrasia na maendeleo ( Chadema) ambao baadhi yao wamekuwa wakijiendesha wenyewe na kushindwa kupeperusha bender ya bunge .

  Huku mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) na mbunge Zitto Kabwe ambaye ni waziri kivuli wa fedha na uchumi (Chadema) wakiibuka kuwatetea madereva hao kuwa pia wanapaswa kulipwa vizuri Kama ambavyo wabunge wenzao wamekuwa wakijitetea kuhusu maslahi mazuri Kwao wafanye hivyo hata kwa kupigania bungeni maslahi mazuri ya madereva wao badala ya kuwapunja haki zao. Filikunjombe ambaye amekuwa mbunge wa kwanza katika bunge hilo kufunguka kuguswa na malalamiko hayo ya madereva na hata kuwaunga mkono madereva hao kwa kuwataka kuondoa uoga katika kupigania maslahi yao. Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungunza na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na Madai hayo ya madereva na kudai kuwa amesikitishwa sana kuona madereva wakiendelea kupunjwa haki zao wakati kazi wanazozifanya za kuwaendesha wabunge hao ni kubwa zaidi na kuwataka wabunge wenzake kuwa na roho za huruma kwa madereva hao.

  Hata hivyo alishauri wabunge wenzake kujaribu kuwatetea madereva wa wabunge ili Kama inawezekana basi madereva hao waweze kulipwa kama madereva wa mawaziri badala ya posho na Mishahara yao kupitia kwenye akaunti za wabunge. " Mimi ninawsunga mkono madereva na nitaendelea kufanya hivyo hadi watakavyotendewa haki ...hoja ya madereva kuhusu ajali za Mara kwa Mara kwa wabunge wanaojiendesha wenyewe ni ya Msingi zaidi na wabunge wenzangu wanapaswa kuifanyia kazi kuacha kufanya kazi ya udereva hata Kama ni dereva"

  Kwa upande wake Mbunge Zitto Kabwe alisema kuwa madereva wanapaswa kuendeleza moto huo ambao wameuwasha bila kuchoka na kuwa tabia ya madereva hao wamekuwa wakianzisha suala hilo na kabla ya kufika mwisho wamekuwa wakiliacha hewani. Zitto alisema kwa safari hii ataungana nao kupigania maslahi yao na kuwataka madereva hao kuendelea kujenga hoja zaidi ili kuweza kutendewa haki bila ya kugombana na wabunge hao ambao ni mabosi wao. Alisema kuwa kuanzia mwezi ujao kila mbunge atapewa kiasi cha shilingi 170,000 kwa ajili ya kumlipa dereva wake kila mwezi na kuwa ni vema fedha hizo wabunge kuingia mikataba na madereva hao na mikataba hiyo Kusainiwa na katibu wa bunge ili iwe ya kisheria na fedha hizo kuingizwa moja kwa moja katika akaunti zao.

  Zitto alithibitisha Madai ya madereva hao kuwa ni kweli Kabisa wabunge wengi katika bunge hilo hawana madereva na wamekuwa wakila fedha ndogo ambavyo zimekuwa zikitolewa na bunge kwa ajili ya madereva. Alisema kuwa kwa kuwa mbunge amekuwa akilipwa kiasi cha shilingi 80,000 kwa siku kwa ajili ya posho ni vema kuwepo utaratibu wa kumlipa dereva wake nusu ya fedha hizo kwa kazi anayoifanya badala ya wabunge kuwalipa shilingi 20000 ama chini ya hapo Zitto alisema kuwa kazi ya madereva ni kubwa hivyo wabunge wanapaswa kuacha mchezo katika kutambua kazi ya madereva hao na kuachana na ubaili usio na maana katika kuwalipa haki stahiki . "Bwana Godwin nasema nitasimama kidete kutetea haki za madereva ili kuona nao wanatendewa haki ....suala hilo la madereva kulalamika juu ya maslahi duni kwa mara ya kwanza lilipoibuka zaidi ya miaka miwili sasa Mimi niliungana nao kuwatetea na sasa nitaendelea kufanya hivyo"

  Kuhusu Madai ya wabunge wengi wa Chadema kuongoza kutimua madereva na kujiendesha wenyewe na baadhi ya wabunge wa viti maalum kuendeshwa na waume zao ,Zitto alitaka wabunge hao pia kuhojiwa wenyewe badala ya kuwasemea yeye. Mbali ya wabunge wa majimbo kujiendesha kwa upande wa wabunge wa viti maalum wamekuwa wakiendeshwa na waume zao huku baadhi yao wakilala kitanda kimoja zaidi ya watatu imefahamika.

  Mmoja Kati ya wabunge wa viti maalum wa vyama vya upinzani amedokeza Siri nzito hiyo kwa wabunge na kudai kuwa wabunge hao wamekuwa wakifanya hivyo kwa kuishi maisha ya ghetto wawapo bungeni Kama njia ya kubana matumizi . Pia alisema kuwa mbali ya wabunge kushindwa kuwalipa vizuri madereva wao pia sehemu kubwa ya wabunge wameamua kuegesha mashangigi ya ubunge ambayo walikopeshwa na kutumia magari ya hari ya chini zaidi kutokana na mashangingi hayo kuonekana kutumia mafuta mengi zaidi. Kwani wamedai kuwa njia hiyo itawasaidia zaidi kujua umma kujua jinsi ambavyo wabunge hao wanavyoongoza kuwatetea wanyonge wakati wao wakiendelea kuwatendea ndivyo sivyo madereva wao.

  Madereva hao wamesema kuwa wabunge wamekuwa mbele kutetea madereva wanaofanya kazi hiyo hapa nchini kupewa mikataba wakati kwa upande wao wabunge hao wamekuwa wakiendelea kuwafanyia ufisadi kwa kutowalipa fedha zao wala kuingia mikataba ya kisheria. Uamuzi huo wa madereva hao kutaka kuwaanika katika vyombo vya habari wabunge hao umetolewa leo tena ikiwa ni siku mbili baada ya mtamdao mtandao wa
  Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima na gazeti hili la Jamboleo kuandika juu ya madai ya madereva hao kwa mabosi wao ambao ni wabunge.

  Mwenyekiti wa chama cha madereva wa wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Juvenille Joseph alisema kuwa wapo baadhi ya wabunge wachache wa CCM na wale wa vyama vya upinani ambao wamekuwa wakiongoza kwa kuwajali madereva wao . Ila alisema wapo baadhi ya wabunge ambao madereva wao hata kulala kwao na kula kwao wakiwa bungeni Dodoma ni shida na kuwa baadhi ya madereva wanaolipwa vizuri wamekuwa wakiwachangia fedha za kununua mihogo na maji

  Hivyo alisema kuwa uwazi wa madereva hao kwa kuanika majina ya wabunge wao ambao wamekuwa wakiwapunja haki zao itasaidia kupata haki yao badala ya kuendelea kuwa madereva wa majina na heshima wakati mfukoni hawana kitu. “mbali ya wabunge kufanya kazi nao bila mikataba ila baadhi ya wabunge wamekuwa wakilipa vizuri akiwemo bosi wangu Felista Bulla (CCM) mimi kiukweli analipa vizuri sana tofauti na wenzangu ila bado nitaendelea kupigania haki ya madereva wenzangu …. Mimi wakati bunge la mwaka 2005 alinipa milioni 3”

  Wabunge wengine waliotoa mkono wa ahsante kwa madereva wao ni pamoja na mbunge Stella Manyanya ( CCM) Milioni 5.5 Zitto Kabwe (Chadema) milioni 5.5 na mbunge mmoja wa viti maalum kutoka Zanzibar yeye alimpa dereva wake milioni 3 japo hakurudi bungeni. “Wabunge wetu wanaongoza kwa kuikosesha serikali mapato yake na ajira kwa vijana kupungua kutokana na baadhi yao kushindwa kutoa mikataba ya kazi wala kuwalipa mishahara ambayo serikali kupitia bunge ilipendekeza kwa ajili ya madereva wa wabunge toka mwaka 2008 .


  Hata hivyo alimpongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) kuwa ameonekana kuwa mbunge aliyeingia bungeni kwa kipindi hiki cha kwanza na kuwa mfano wa kumjali dereva wake. Madereva hao walisema kuwa sehemu kubwa ya wabunge hao wameanza kuendesha magari yao wao wenyewe baada ya kushindana na madereva waliokuwa wakiwaendesha awali baada ya kushindwa kuwalipa mishahara na posho zilizobainishwa kisheria na ofisi ya bunge. Hata hivyo walisema kuwa suala hilo la wabunge kushindwa kuwalipa vizuri madereva si kwa wabunge wa CCM pekee bali ni wabunge karibu wote wakiwemo wa vyama vya upinzani ambao baadhi yao kwa sasa wanajiendesha wenyewe baada ya kukimbiwa na madereva wao kwa kushindwa kuwalipa.

  Pia walisema matukio ya ajali kwa wabunge yamezidi kuongezeka kutokana na wabunge hao kushindwa kufanya kazi na madeva na kuishia kuifanya kazi hiyo wao wenyewe na matokeo yake kutokana na mawazo ama kuwa na mambo mengi kichwani wamekuwa wakishindwa kuyamundu magari yao na kuishia kusababisha ajali za barabarani ambazo baadhi ya ajali hizo zimekuwa zikisababisha vifo ama ulemavu kwa wabunge hao. “Leo ukitazama hapa bungeni Dodoma utaona idadi kubwa ya wabunge wanajiendesha wenyewe kama si mbunge kuwaendesha wenzake basi mbunge amekuwa akijiendesha mwenyewe na wapo wanaokuja na madereva hadi hapa Dodoma na baada ya hapo dereva amekuwa akipewa nauli ya kurudi jimboni na mbunge anaendelea kujiendesha mwenyewe kama njia ya kubana matumizi “ Aidha walisema kuwa miongoni mwa madereva waliokosa ajira ni pamoja na wale waliokuwa madereva wa mawaziri na manaibu mawaziri ambao hawakurejea tena baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza mabadiliko ya baraza la mawaziri hivi karibuni ambapo mawaziri hao kwa sasa wamegeuka kuwa madereva wenyewe.

  Makamu mwenyekiti wa chama cha madereva wa wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Adam Said alisema kuwa sababu ya wabunge wengi kukimbiwa na madereva ni kutokana na maslahi duni wanayoendelea kulipwa na kuwa hivi sasa baadhi ya wabunge baada ya kukimbiwa na madereva wamelazimika kuwatumia ndugu zao kama njia ya kukwepa kuwalipa mishahara. Pia alisema maisha ambayo madereva hao wamekuwa wakiishi mjini Dodoma ni heri ya omba omba kutokana na wabunge hao kuwalipa kiasi cha shilingi 50,000 ama chini ya hapo na kutaka kuitumia kwa muda wa wiki moja ama mwezi mzima jambo lililopelekea madereva hao kupanga vyumba mtaani na kuishi katika chumba kimoja zaidi ya watatu kama sehemu ya kubana matumizi.

  Mwenyekiti wa chama cha madereva wa wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Juvenille Joseph alithibitisha madaia ya madereva hao na kuwa tayari uongozi wake umefikisha malalamiko ya madereva hao katika ofisi ya chama cha wafanyakazi mkoa wa Dodoma pamoja na ofisi ya spika wa bunge Anne Makinda ili kushughulikia madai hayo. Alisema kuwa kwa sasa wanakusudia kuitisha mkutano wa dharura wa madereva wote wanaowaendesha wabunge ili kuweza kuwa na msimamo wa pamoja katika kupigania haki zao na baada ya hao watawatumia barua wabunge ambao wanajiendesha wenyewe ili waweze kujiunga na chama hicho cha madereva wa wabunge . Kwani alisema kuwa katika barua iliyotolewa na ofisi ya bunge Novemba 3 mwaka 2008 barua yenye kumbukumbu namba FA.155/206/01/70 ikiwa na kichwa yahusu posho ya ubunge Malimbikizo July –Octoba 2008 ilibainisha posho na mishahara hiyo.

  Joseph alisema kuwa posho ya mafuta lita 1000 kwa lita shilingi 2500 kwa wakati huo ilikuwa ni kiasi cha shilingi milioni 2.5 kwa mwezi , Matengenezo yagari asilimia 40 ya thamani ya mafuta ambayo ilikuwa ni milioni 1 kwa mwezi , posho ya dereva siku 10 kwa shilingi 30,000(vijijini ) ilikuwa ni shilingi 300,000 na posho ya mbunge siku 10 kwa kila atakazokuwepo kijijini kwa kila siku shilingi 45,000 ilikuwa ni shilingi 450,000 huku mshahara wa dereva kwa mwezi ulikuwa ni shilingi 100,000 na kufanya jumla kwa mwezi kuwa bajeti ya shilingi milioni 5,115,000 kwa wakati huo.

  Ila pamoja na sasa posho za wabunge kupanga ila bado wabunge wamekuwa wakiwalipa madereva wao kiasi cha shilingi 70,000 hadi 90,000 kwa mwezi fedha ambazo haitoshi kwa maisha ya sasa hivyo kutaka fedha za madereva kuingizwa katika akaunti zao na madereva wote wa wabunge kuwa na mikataba ya kazi badala ya kuendelea kufanya kazi kirafiki na kindugu.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  MADEREVA WA WABUNGE WAIBUKA KWA SURA MPYA ,SASA KUANIKA WABUNGE WAFISADI

  SAKATA la madai ya madereva wanaowaendesha wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania limezidi kuchukua sura mpya sasawadai watayaanika majina ya wabunge waliofukuza madereva wao na kuifanya kazi hiyo wenyewe pamoja na wale ambao wanawalipa madereva wao chini ya shilingi 50,000 na wanaolipa vizuri maderevawao. Kwani wamedai kuwa njia hiyo itawasaidia zaidi kujua umma kujua jinsi ambavyo wabunge hao wanavyoongoza kuwatetea wanyongewakati wao wakiendelea kuwatendea ndivyo sivyo madereva wao.

  Madereva hao wamesema kuwa wabunge wamekuwa mbele kutetea madereva wanaofanya kazi hiyo hapa nchini kupewa mikataba wakati kwa upande wao wabunge hao wamekuwa wakiendelea kuwafanyia ufisadi kwa kutowalipa fedha zao wala kuingia mikataba ya kisheria.
  Uamuzi huo wa madereva hao kutaka kuwaanika katika vyombo vya habari wabunge hao umetolewa leo tena ikiwa ni siku mmoja baada ya mtamdao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima na gazeti la Jamboleo kuandika juu ya madai ya madereva hao kwa mabosi wao ambao ni wabunge.

  Mwenyekiti wa chama cha madereva wa wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Juvenille Joseph alisema kuwa wapo baadhi ya wabunge wachache wa CCM na wale wa vyama vya upinani ambaowamekuwa wakiongoza kwa kuwajali madereva wao .
  Ila alisema wapo baadhi ya wabunge ambao madereva wao hata kulalakwao na kula kwao wakiwa bungeni Dodoma ni shida na kuwa baadhi ya madereva wanaolipwa vizuri wamekuwa wakiwachangia fedha zakununua mihogo na maji .

  Hivyo alisema kuwa uwazi wa madereva hao kwa kuanika majina yawabunge wao ambao wamekuwa wakiwapunja haki zao itasaidia kupata haki yao badala ya kuendelea kuwa madereva wa majina na heshimawakati mfukoni hawana kitu.
  "mbali ya wabunge kufanya kazi nao bila mikataba ila baadhi yawabunge wamekuwa wakilipa vizuri akiwemo bosi wangu Felista Bulla (CCM) mimi kiukweli analipa vizuri sana tofauti na wenzangu ila bado nitaendelea kupigania haki ya madereva wenzangu …. Mimi wakati bunge la mwaka 2005 alinipa milioni 3"

  Wabunge wengine waliotoa mkono wa ahsante kwa madereva wao ni pamoja na mbunge Stella Manyanya ( CCM) Milioni 5.5 Zitto Kabwe (Chadema) milioni 5.5 na mbunge mmoja wa viti maalum kutoka Zanzibar yeye alimpa dereva wake milioni 3 japo hakurudi bungeni.
  "Wabunge wetu wanaongoza kwa kuikosesha serikali mapato yake na ajira kwa vijana kupungua kutokana na baadhi yao kushindwa kutoa mikataba ya kazi wala kuwalipa mishahara ambayo serikali kupitia bunge ilipendekeza kwa ajili ya madereva wa wabunge toka mwaka 2008 .

  Hata hivyo alimpongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) kuwa ameonekana kuwa mbunge aliyeingia bungeni kwa kipindihiki cha kwanza na kuwa mfano wa kumjali dereva wake.
  Madereva hao walisema kuwa sehemu kubwa ya wabunge hao wameanza kuendesha magari yao wao wenyewe baada ya kushindana na madereva waliokuwa wakiwaendesha awali baada ya kushindwa kuwalipa mishahara na posho zilizobainishwa kisheria na ofisi ya bunge.

  Hata hivyo walisema kuwa suala hilo la wabunge kushindwa kuwalipa vizuri madereva si kwa wabunge wa CCM pekee bali ni wabunge karibu wote wakiwemo wa vyama vya upinzani ambao baadhi yao kwa sasa wanajiendesha wenyewe baada ya kukimbiwa na madereva wao kwa kushindwa kuwalipa.
  Pia walisema matukio ya ajali kwa wabunge yamezidi kuongezeka kutokana na wabunge hao kushindwa kufanya kazi na madeva na kuishia kuifanya kazi hiyo wao wenyewe na matokeo yake kutokana na mawazo ama kuwa na mambo mengi kichwani wamekuwa wakishindwa kuyamundu magari yao na kuishia kusababisha ajali za barabarani ambazo baadhi ya ajali hizo zimekuwa zikisababisha vifo ama ulemavu kwa wabunge hao. "Leo ukitazama hapa bungeni Dodoma utaona idadi kubwa ya wabunge wanajiendesha wenyewe kama si mbunge kuwaendesha wenzake basi mbunge amekuwa akijiendesha mwenyewe na wapo wanaokuja na madereva hadi hapa Dodoma na baada ya hapo dereva amekuwa akipewa nauli ya kurudi jimboni na mbunge anaendelea kujiendesha mwenyewe kama njia ya kubana matumizi "

  Aidha walisema kuwa miongoni mwa madereva waliokosa ajira ni pamoja na wale waliokuwa madereva wa mawaziri na manaibu mawaziri ambao hawakurejea tena baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza mabadiliko ya baraza la mawaziri hivi karibuni ambapo mawaziri hao kwa sasa wamegeuka kuwa madereva wenyewe.


  Makamu mwenyekiti wa chama cha madereva wa wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Adam Said alisema kuwa sababu ya wabunge wengi kukimbiwa na madereva ni kutokana na maslahi duni wanayoendelea kulipwa na kuwa hivi sasa baadhi ya wabunge baada ya kukimbiwa na madereva wamelazimika kuwatumia ndugu zao kama njia ya kukwepa kuwalipa mishahara .

  Pia alisema maisha ambayo madereva hao wamekuwa wakiishi mjini Dodoma ni heri ya omba omba kutokana na wabunge hao kuwalipa kiasi cha shilingi 50,000 ama chini ya hapo na kutaka kuitumia kwa muda wa wiki moja ama mwezi mzima jambo lililopelekea madereva hao kupanga vyumba mtaani na kuishi katika chumba kimoja zaidi ya watatu kama sehemu ya kubana matumizi.

  Mwenyekiti wa chama cha madereva wa wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Juvenille Joseph alithibitisha madaia ya madereva hao na kuwa tayari uongozi wake umefikisha malalamiko ya madereva hao katika ofisi ya chama cha wafanyakazi mkoa wa Dodoma pamoja na ofisi ya spika wa bunge Anne Makinda ili kushughulikia madai hayo.
  Alisema kuwa kwa sasa wanakusudia kuitisha mkutano wa dharura wa madereva wote wanaowaendesha wabunge ili kuweza kuwa na msimamo wa pamoja katika kupigania haki zao na baada ya hao watawatumia barua wabunge ambao wanajiendesha wenyewe ili waweze kujiunga na chama hicho cha madereva wa wabunge .

  Kwani alisema kuwa katika barua iliyotolewa na ofisi ya bunge Novemba 3 mwaka 2008 barua yenye kumbukumbu namba FA.155/206/01/70 ikiwa na kichwa yahusu posho ya ubunge Malimbikizo July –Octoba 2008 ilibainisha posho na mishahara hiyo.
  Joseph alisema kuwa posho ya mafuta lita 1000 kwa lita shilingi 2500 kwa wakati huo ilikuwa ni kiasi cha shilingi milioni 2.5 kwa mwezi , Matengenezo yagari asilimia 40 ya thamani ya mafuta ambayo ilikuwa ni milioni 1 kwa mwezi , posho ya dereva siku 10 kwa shilingi 30,000(vijijini ) ilikuwa ni shilingi 300,000 na posho ya mbunge siku 10 kwa kila atakazokuwepo kijijini kwa kila siku shilingi 45,000 ilikuwa ni shilingi 450,000 huku mshahara wa dereva kwa mwezi ulikuwa ni shilingi 100,000 na kufanya jumla kwa mwezi kuwa bajeti ya shilingi milioni 5,115,000 kwa wakati huo.

  Ila pamoja na sasa posho za wabunge kupanga ila bado wabunge wamekuwa wakiwalipa madereva wao kiasi cha shilingi 70,000 hadi 90,000 kwa mwezi fedha ambazo haitoshi kwa maisha ya sasa hivyo kutaka fedha za madereva kuingizwa katika akaunti zao na madereva wote wa wabunge kuwa na mikataba ya kazi badala ya kuendelea kufanya kazi kirafiki na kindugu.
  Wakati huo huo mbunge wa jimbo la Ludewa Filikunjombe amewatakaamefunguka kulizungumzia suala hilo na kuwataka madereva hao kuacha uoga na iwapo hawalipwi kweli kuwa wawazi na kuepuka uoga wa kuwataja kwa majina wabunge wao.

  Hata hivyo uchunguzi wa mtandao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima umebaini sehemu kubwa ya wabunge wa vyama vya upinzani na waliokuwa mawaziri na manaibu waziri katika baraza la mawaziri lililobadilishwa hivi karibuni ndiowanaongoza kwa kujiendesha wao wenyewe baada ya kushindwakuwalipa mishahara madereva wao.
   
 3. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Nawaunga mkono wabunge zito na deo, ni kweli hawa baadhi ya wabunge hawawatendei wema madereva wao. mifano hai tunao kuna mbunge mmoja inasemekana anakaba perdiem hadi alisababisha ajali na kusababisha vifo kwa ndigu zake.
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  nachukiaga habari ndefu zinazoelezea point ileile..niite mvivu
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kujiendesha mwenyewe wakati unapewa pesa ya kumlipa dereva ni ufisadi kama ufisadi mwingine wowote. Unashindwa kuyoa ajira kwa vijana unang'ang'ana kujiendesha badala ya kimtumia kija wewe ukae kushoto na kutafakari.

  Wabunge mna mambo mengi mara ufikirie kwamba Kimbunga ameonekana jimboni kwako na una wasiwasi kwamba anapiga jalamba la kukuengua 2015 huku unaendesha matokeo yake ni miajali isiyokuwa na mbele wala nyuma. Wabunge toeni ajira kwa vijana ikiwa ni sehemu ya kuisaidia serikali katika kutengeneza ajira.

  Acheni tamaa ya kukaba hadi penalti.
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mbona hiyo picha ya Juu namuona mzee wa mabomu aka Mzee wa Kwela aka Mzee.wa Ranchi kwani naye amejitosa kuwa tetea madereva au ni katika kikao chao cha uchimbaji chuma huko Liganga?
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono jitahada za madereva kudai haki zao. Hata hivyo nadhani kuna njia nzuri zaidi kwa Deo Filikunjombe na Zitto kusaidia hawa madereva including kuungalia utaratibu mzima wa bunge kuwa ndio mlipaji wa mishahara badala ya mbunge.

  Pia, kwenye point ya baadhi ya wabunge kujiendesha wenyewe au waume zao, ni vizuri Deo na Zitto wakawa very careful na hii hoja maana wapo wabunge wanaomua kufanya hivyo kwa sababu za 'kiusalama'. Ni vema wawili hawa wakatafuta namna bora ya kuwatetea madereva bila kuibua hisia zilizojengeka za kutumia madereva kwa maslahi ya kufanikisha mikakati ya kisiasa.

  Mwisho, sijaelewa ni nani anayepita kwenye vyumba wanavyolala wabunge na kuona kuwa baadhi wanalala watu kwenye chumba kimoja? Hii ni zaidi ya umbeya! Ndani ana-audit sleeping arrangement za watu wazima na utashi wao?
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kama unazoea kusoma vitabu na habari mbalimbali hapa ndio umefika. Wengine hatupendelei mipasho kwani huwezi kuona wazi nini kinaongelewa kwa ufafanuzi upi.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Sorry, lengo ni picha ambayo hawa wabunge wawili wanaonekana kuwa pamoja, vinginevyo ieleweke picha hiyo imetoholewa walipoenda Ludewa/Mchuchuma kuangalia madini kamati ya Zito.
   
 10. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Madereva? ... mimi sioni haja ya serikali kumlipia mbunge dereva.
  Madereva wanaostahili kulipiwa na serikali ni kuanzia ma-PS ,manaibu na mawaziri. Wengine sioni umuhimu wala sababu, tuache mambo ya kizamani.
   
 11. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Duh bongo noma.
   
 12. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hoja hapa siyo kwamba madereva wa wabunge walipwe ama wasilipwe; hoja ni kwamba bunge linatoa fedha za kuwalipa madereva linawapa wabunge na wabunge wanazitia ndani fedha za madereza wao. Hii ni dhuluma.
   
 13. J

  JokaKuu Platinum Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,069
  Trophy Points: 280
  ..kwenye nchi za wenzetu wabunge na mawaziri wanaendesha magari yao wenyewe.

  ..napendekeza wabunge wasipewe posho ya aina yoyote ile ya kuajiri madereva.

  ..wakiamua kuajiri madereva wawalipe kwa kutumia fedha zao wenyewe.

  ..pia tuna wabunge 200++ sasa ina maana bunge liandae mikataba ya madereva kwa wabunge wote hao??

  ..halafu tukianza na madereva wa wabunge, nini kitatuzuia kuandaa mikataba ya wapishi wa wabunge, madobi, walinzi, etc etc??
   
 14. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,112
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Sioni kosa kama mbunge anaweza kujiendesha mwenyewe. Ni sawa kabisa mbunge kujiendesha mwenyewe utakumbuka kuwa kwa sasa tunapigania viongozi wengi wakopeshwe magari ili waweze kuyanunua na kujiendesha wenyewe. Katika nchi zilizoendelea sio ajabu hata juzi juzi wazri mkuu wa Uk aliendesha mwenyewe weekend kwenda kupata chochote na familia yake. Ila kwa wale wabunge ambao hawajiwezi kuendesha na kuajiri dereva inabidi amlipe vizuri. Hivyo tusilete dhana ya kuwa CDM ndio wanaongoza kwa kufukuza madereva. Kama najiweza kwanini nimwajiri dereva. Kwa mfano niko jimboni kwangu mara nyingi natoka kwenda ofisini nisawasawa na mfanyakazi mwingine anaenda kazini.
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  kobello, bunge letu lina matumizi ya hovyo sana na tabia ya kazamani kama ulivyosema. Angalia wakati wa vikao, waziri au msemaji akiwa kwenye meza, ataletewa maji, na kumiminiwa kwenye glass!!! Hivi wabunge/waziri wanashindwa kujihudumia wenyewe? wanashindwa kubeba chupa ya maji mpaka waletewe?

  Si hivyo, zama hizi za science & technology mbunge anaandika kaujumbe kwenye karatasi anapeperusha juu, mhudumu atakuja na kumpelekea mbunge mlengwa! Ukweli ukiangalia bunge wakati wa vikao ni uzururaji mtupu umo kweli ndani wa wabeba chupa za maji ya kunywa na vikaratasi. Hawa wote wanatakiwa waondolewe ili kubana matumizi. Pia ni mfano mbaya sana wa mtu mzima kutaka umiminiwe maji, hapo unapayuka matumizi makubwa yasiyo na maana serikalini? yepi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #16
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Madreva poleni sana toeni pia siri wanavyolala mzungu wa 4 hapo Area C huku wakipanda majukwaani wakidai nchi inaliwa na mafisadi huku wakitaka posho kwao ziongezwe
  Sasa km wanalipwa night na hela ya dreva wanatia ndani nuu aibu
   
 17. Kingmairo

  Kingmairo JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 4,977
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Hichi unachokisema ni sawa wala hakuna ubishi lakini ishu hapa ni kwamba hawa ndugu wanapewa fedha za kuwalipa madereva wao na bunge sasa huoni huo ni wizi? Kama anapewa fedha halafu hana dereva si wizi huo? Ilipaswa asipewe hizo fedha kama hana dereva.
   
 18. Kingmairo

  Kingmairo JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 4,977
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Uongozi wa bunge unapswa kubeba lawama zote katika hili suala. Kwanini wawalipe madereva hawa kupitia akaunti za wabunge? Inasikitisha kuona taasisi nyeti kama bunge inatumia utaratibu mbovu namna hiyo katika kutoa haki kwa wasaidizi wa watumishi wake. Kwa maana nyingine unaweza kusema bunge ndo limehamasisha uporwaji wa haki za hao madereva badala ya kuhakikisha wanapatiwa haki zao. Huu ni ufisadi mkuu
   
 19. m

  mahoza JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,242
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na wewe siku hizi kila mtu anajiendesha mwenyewe unaomba kazi unaambiwa unaleseni ya udereva maana hakuna dereva. Ma PS na maundersecretary wanajiendesha kasoro Rais.
   
 20. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Kwanini wawe na madereva? Kama hawana fedha si wajiendeshe wenyewe?
   
Loading...