mr.dominick
JF-Expert Member
- Jun 21, 2012
- 244
- 28
hivi nchi wahisani wakiona mambo yanayofanyika kama haya hivi wanatuonaje
hivi hii nchi inakwenda kwa nguvu za nchi wahisani ??? Halafu tuendelee kuikumbatia Zanzibar !!!! ngoma tunayo
hivi nchi wahisani wakiona mambo yanayofanyika kama haya hivi wanatuonaje
Haikuingii akilini? Inakuingia wapi? Du! Mzee dhaifu kaleta mambo ya Cameroon naona yamekunogeaHaiingii akilini kwa binaadam yeyote mwenye fikra japo kidogo, eti Serikali wakuchukuwe, wakupige, wakutupe Mabwepande halafu waje haki za binaadam kukuota.
serikali ya ccm inatakiwa itafakari.. Je baada ya kumuua sokoine ufisadi/uhujumu uchumi uliwafikisha wapi, je ndo ulikuwa na manufaa au ndo laana inayoitafuna serikali hadi leo,je hali ya uhujumu uchumi imefikisha wapi taifa, je kama sokoine angebaki hai hali ingekuwa hivi????
Walipomuuwa kolimba, je kupoteza dira kwa ccm kumefikia wapi? Je kwa kuumua ndo walipata dira au ndo walipotea njia na kutokea hapa walipo? Je ccm iliimarika baada ya kumuuwa au ndo ilizidi kuyumba???
Walitarajia wamwmuua dr ulimboka, je wanafikiri kwa kufanya hivyo ndo wataimarisha huduma za afya? Je ndo migomo itaisha? Maslahi ya madaktari hayatadaiwa?
pole sana dr. Ulimboka. Tunakuombea kwa mungu akupe nguvu ya uponyaji haraka.
Kwa wale wanaofikiria watazima vuguvugu la kujikomboa kwa mtanzania kwa kumteka na kumuumiza dr. Ulimboka wajue ya kwamba wameweka petroli kwenye moto. Ole wao, siku zao zimefikia mwisho.
Kwa wanaokumbuka historia ya ufaransa, binti mfalme marie-antoinette hakuelewa kwa nini watu walikuwa wanaandamana, akamuuliza mama yake malkia kwa nini wanaandamana. Alipojibiwa 'wanaandamana kwa kuwa hawana mikate', marie-antoinette alijibu 'si wale keki?'
hii inadhihirisha viongozi wa tanzania hawazijui shida za walalahoi wanaolala chini kwenye hospitali zetu, wanaokufa kila siku kwa kuwa hospitali hazina vifaa kama x ray, hakuna dawa, hakuna hata bandage za kufunga vidonda. Madaktari wanachodai ni mazingira bora ya huduma za afya na vitendea kazi. Kwa kifupi wanataka serikali iwakumbuke watanzania wanaoteseka bila huduma za afya ambazo ni haki yao ya msingi, wakati viongozi na familia zao wanakimbizwa afrika ya kusini, india na hata ulaya kupata matibabu. Badala ya kutafuta ufumbuzi wa madai haya, serikali inawajibu kwa vitisho na hata kufikia kumteka kiongozi wa madaktari.
Familia ya kifalme ufaransa iliondolewa madarakani na marie-antoinette pamoja na wenzake walielewa maana ya nguvu ya umma. Hatuhitaji keki, tunaomba haki yetu tupate huo mkate!
Mpaka kieleweke!
kumbe mabwe pande imeachwa na serikali kuwa sirikali ya mauaji, basi msitu ule upigwe moto kwani hauna faida zaidi ya mauaji. Watu wanakosa viwanja wao wanaujaza damu za watu wasio na hatia.
Haikuingii akilini? Inakuingia wapi? Du! Mzee dhaifu kaleta mambo ya Cameroon naona yamekunogea
Serikali inapokuwa inahusishwa na vitendo vya kinyama kama hivi ni hatari sana..ila kila lenye mwanzo halikosi mwisho
Haiingii akilini kwa binaadam yeyote mwenye fikra japo kidogo, eti Serikali wakuchukuwe, wakupige, wakutupe Mabwepande halafu waje haki za binaadam kukuota.
Serikali IELEZE NINI?
TUPATE MAELEZO YA LHRC KWANZA, Wao walijuajejuaje kuwa Majeruhi yuko Mabwepande
kwa hiyo wewe unaishi na kufanya mambo ili wahisani wakuone? ishi kama utakavyo ili mradi usizuie wala kuingilia haki na mipaka ya wenzako........ usiwe mtumwa wa wahisani..hivi nchi wahisani wakiona mambo yanayofanyika kama haya hivi wanatuonaje