Zitto: Dk. Dau huwezi kujikagua, jiondoe

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
MWENYEKITI wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe, amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau, kutokuwa katibu wa kamati ya ukaguzi wa hesabu za ndani wa shirika hilo.

Zitto alitoa agizo hilo jana jijini Dar es Salam wakati watendaji wa shirika hilo walipokuwa katika mahojiano na kamati hiyo na kushauri kutafutwa mtu mwingine awe katibu wa kamati hiyo.

“Nafikiri yalikuwa yanafanyika makosa makubwa, mkurugenzi mkuu kuchukua nafasi ya katibu wa kamati ya hesabu za ndani na kujikagua mwenyewe … sasa ninaagiza kwamba aondoke ichukuliwe na mfanyakazi mwingine,” alisema Zitto.

Zitto alisema hakuna sheria na si haki kwa kiongozi yeyote kutumia nafasi yake au kuchaguliwa kujichunguza, bali kazi hiyo inapaswa kufanywa na wafanyakazi wengine.

Katika hatua nyingine, Zitto aliitaka NSSF kuielimisha jamii na kuboresha huduma ya mafao ya bima ya afya ambayo yalianza miaka michache iliyopita.

Aliwataka kuwatumia wasanii kuzunguka nchi nzima kutoa elimu ya namna ya kujiunga na kueleza namna mafao ya afya yanavyotolewa.

Pia, Zitto aliitaka NSSF kuangalia namna ya kutengeneza kadi za wanachama tegemezi (watoto), ili kuondoa usumbufu unaojitokeza pale wanapotaka kupatiwa matibabu.
 
Namuunga mkono zitto kwa hili! Lisiishie NSSF tuu bali kwa mashirika yote ya umma.
 
Amemfumbia macho swahiba wake!au danganya toto?maana hao wote(kila mmoja) ni first right handman wa JK.Wenyewe kwa wenyewe;
 
MWENYEKITI wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe, amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau, kutokuwa katibu wa kamati ya ukaguzi wa hesabu za ndani wa shirika hilo.

Zitto alitoa agizo hilo jana jijini Dar es Salam wakati watendaji wa shirika hilo walipokuwa katika mahojiano na kamati hiyo na kushauri kutafutwa mtu mwingine awe katibu wa kamati hiyo.

"Nafikiri yalikuwa yanafanyika makosa makubwa, mkurugenzi mkuu kuchukua nafasi ya katibu wa kamati ya hesabu za ndani na kujikagua mwenyewe … sasa ninaagiza kwamba aondoke ichukuliwe na mfanyakazi mwingine," alisema Zitto.

Zitto alisema hakuna sheria na si haki kwa kiongozi yeyote kutumia nafasi yake au kuchaguliwa kujichunguza, bali kazi hiyo inapaswa kufanywa na wafanyakazi wengine.

Katika hatua nyingine, Zitto aliitaka NSSF kuielimisha jamii na kuboresha huduma ya mafao ya bima ya afya ambayo yalianza miaka michache iliyopita.

Aliwataka kuwatumia wasanii kuzunguka nchi nzima kutoa elimu ya namna ya kujiunga na kueleza namna mafao ya afya yanavyotolewa.

Pia, Zitto aliitaka NSSF kuangalia namna ya kutengeneza kadi za wanachama tegemezi (watoto), ili kuondoa usumbufu unaojitokeza pale wanapotaka kupatiwa matibabu.

hapo sasa ndio naona lengo la Zitto la kuwatumia wasanii toka kigoma (Leka dutigite) ili wamfanyie promo ya urais 2015 kwakua eti wasanii hao wanakubalika karibia wote na vijana..hapa analazimisha wasaniii wale wale (Diamond, Alli Kiba, chege) waonekane influencial kwa jamii ili iwe rahisi kwake..the chap ni mjanja sana huyu!..Yanini Kuvalia Tenite Mimba ya Jirani??!!
 
ni mjanja kwel ila kuna wajanja zaid yake na wameshastukia styles zake za kuwa2mia wasanii kujenga jina for 2015 target lol! Akil kumkichwa.
 
ni mjanja kwel ila kuna
wajanja zaid yake na wameshastukia styles zake za kuwa2mia wasanii
kujenga jina for 2015 target lol! Akil kumkichwa.

atoe msimamo wa kamati kuhusu fao la kujitoa...aache kujiumauma....
 
Badala ya kusema watutumie sisi tusio kuwa na ajira anasema wawatumie wasanii!
 
hapo sasa ndio naona lengo la Zitto la kuwatumia wasanii toka kigoma (Leka dutigite) ili wamfanyie promo ya urais 2015 kwakua eti wasanii hao wanakubalika karibia wote na vijana..hapa analazimisha wasaniii wale wale (Diamond, Alli Kiba, chege) waonekane influencial kwa jamii ili iwe rahisi kwake..the chap ni mjanja sana huyu!..Yanini Kuvalia Tenite Mimba ya Jirani??!!

Ndivyo alivyosema?
 
mimi namsubiri ataje walioficha pesa uswisi kwenye bunge kama alivoahidi asipofanya hivo nitaaanza kumhesabu nae ni mmoja wa walioficha pesa uswisi!
 
Amwambie pia sisi wafanyakazi tunataka hela yetu
Kikwete na wenzie watajua wapi watatoa hela za kujenga kigamboni na kampeni zao 2015
 
Back
Top Bottom