Zitto: Deni la Taifa kwa miaka 4 limeongezeka sawa na uongozi wote wa JK kwa miaka 10

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Serikali ya Awamu ya 4 ilipoingia Madarakani Deni la Taifa la Nje lilikuwa USD 8 billions ( Novemba 2005 )
Wakati Serikali ya Awamu ya 4 inaondoka madarakani miaka 10 baadaye, Deni la Nje lilikuwa limefikia USD 15 bilioni ( Novemba 2015 )

Serikali ya Awamu ya Tano imefikisha Deni la Nje USD 22 bilioni ndani ya miaka 4 tangu iingie madarakani. Maana yake ni kuwa, Serikali ya Rais John Magufuli katika miaka 4 imeliingiza Taifa katika Deni la USD 7 bilioni sawasawa na Deni lote lililokopwa katika miaka 10 ya Rais Jakaya Kikwete.
FB_IMG_1569578603995.jpg
 
Ungechambua ilo deni liloongezeka awamu ya tano limetumika kiholela(matumizi ya hovyo) au limeenda kwenye mambo ya msingi(maendeleo)?

Pili unge analyse au kufanya comparison kwamba awamu ya nne na ya tano baada ya kuchukua mikopo, je awamu ipi hiyo mikopo ilienda kwenye maendeleo na kwa asilimia ngapi? Je kukopa kwa ajili ya maendeleo ni dhambi?

Mwisho najua jamaa mchumi mbobezi kama anavyojipambanua apunguze kuja na vitu ambavyo havina NONDO za kutosha au kama anatafuta political mileage aseme tu.
 
"Tutembee kifua mbele ni pesa zetu za ndani", sijawahi kuwa na kiongozi wa nchi niliye na mashaka naye akifungua kinywa Kama magufuli.
 
Yani Zitto nae anataka simple popularity. Kwani yeye hajui miradi inayofanyika ktk nchi ya Tz kweli?
Mbona tunaambiwa yote yafanyikayo ni pesa zetu wenyewe,au MABEBERU yanatufanyia figisu?
 
Ungechambua ilo deni liloongezeka awamu ya tano limetumika kiholela(matumizi ya hovyo) au limeenda kwenye mambo ya msingi(maendeleo)?
Hatutaki kiongozi anayetia shaka akinyanyua mdomo....Kama umenielewa hewala!
 
Back
Top Bottom