Janjaweed
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 13,157
- 10,655
Kimsingi sikubaliani na majumuisho ya jumla na dhanifu kuwa review hii ya mikataba inayotayarishwa na Prof Muhongo ni populist in nature.
Pamoja na mchango huu mzuri maudhui ya mchango wenyewe ni kwamba kwa vile pro active stance ya kurekebisha kasoro za mikatba hiyo inatoka kwenye serikali ya CCM, basi zoezi lenyewe ni naught.
Kuna watu waliojijengea mioyoni mwao kuwa na mtazamo hasi kwa kila kitu kinachofanywa na serikali ya CCM, hata kama ni kwa faida ya wananchi waliowengi.
Prof zmuhongo( na ndg Maswi) wamepigwa vita sana pale Wizara ya Nishati na Madini, vita ya wazi wazi na hata kisiasa kupitia Wabunge.
Siyo siri kuwa mikataba hii mibovu imetayarishwa na wanasiasa ambao baadhi wananufaika nayo hadi leo hii.
Ndiyo maana tulio wengi tunashangaa sana kuwa at last kapatikana mtu mwenye kuthubutu kuchambua the pandora box ya uchafu wa mikataba ya kifisadi, watu kama Zitto wanakuja juu.
Kwa msimamo huu, je CDM ni just an idler katika gurudumu la masahihisho ya mikataba hiyo?
Kulaumu tu from a safe distance?
Mimi nachelea kukubaliana na misimamo isiyo na misingi.
Tungependa vile vile Mzee Mwanakijiji kupata maoni yako ya kisera juu ya mikakati potofu na kifisadi kwa suala la Meya wa Moshi na safari ya masomo Kigali.
Zaidi ya maneno matupu sitegemei zaidi toka wenzetu wa CDM.
Kwani kanuni za mapitio, marejesho na mabadiliko ya mikataba, makubaliano ya hiyari na mikataba ya upendeleo inaruhusu waziri kufanya hizi decisions?