Zitto & Co: Zimebaki Siku 3 tu Kumg'oa Waziri Mkuu, Nini Kinaendelea?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto & Co: Zimebaki Siku 3 tu Kumg'oa Waziri Mkuu, Nini Kinaendelea??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Donyongijape, May 4, 2012.

 1. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Zimeshapita siku takribani siku 11 tangu tarehe 23/04/2011, siku ambayo Mh. Zitto aliwasilisha hoja ya Kumg'oa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Na kimsingi zimebaki siku tatu tu kabla ya kwisha siku 14 zinazotambuliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hoja iliyotimiza masharti kuwasilishwa.

  Watanzania tumeachwa njia panda mpaka sasa hatujui nini kinaendelea kuhusu hoja hii. Je spika ametoa mwongozo gani?. Je dharura iliyoombwa kupitisha hoja hii imekuwaje?

  Je, kamati kuu ya CCM kuahidi kufanya mabadiliko Baraza la Mawaziri imeondoa uhalali wa hoja iliyoko bungeni??. Na kama waliosaini wamekubali hoja hiyo (ya CCM na JK) kwa nini hawaiondoi bungeni (ku-retreat) na UMMA ukajulishwa??

  Au Bwana Zitto&Co. wamefreeze kusubiri temper ya uteuzi wa mawaziri wapya wa JK?? May be wanaogopa kuchokonoa hili wakiogopa Bwana Mkubwa asije 'akawawaweka kando'?.

  Je Ikitokea JK akamrudisha huyu huyu Waziri mkuu ambaye kimsingi walitaka kumg'oa kwa utendaji wake mbovu, tena baada ya hizi siku kumi na nne kuwa zimekwisha ITAKUWAJE?.

  Nawatakia siku njema wapiganaji wote mlioasaini, huku nikitegemea majibu yangu (na ya wenzangu walio njia panda kuhusu hili).

  Donyongijape.
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  hapo tu mkuu inabidi uanze upya kwa kuwa Zitto hajawasilisha hoja bali taarifa.
   
 3. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hapana Mkuu, taarifa ni ile aliyoitoa siku ambapo aliomba wabunge wamuunge mkono kwa kusaini ikiwa ni kusudio la kuwasilishwa Bungeni. Iliyopo Bungeni sasa ni HOJA ambayo inasubiri kujadiliwa bungeni. Naomba Majibu tafadhali.. nini kinaendelea?
   
 4. F

  Freshbrain Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naamini watakuja wenyewe kukupa majibu, au hata humu humu utapata majibu. This is JF, 'Ukweli na Uhakika'. Lol
   
 5. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ndio maana nikaileta hapa.
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hoja imeungwa mkono bila kupingwa!
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  53A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 51 ya Katiba hii,
  Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na
  Waziri Mkuu endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo na
  ikapitishwa kwa mujibuwa wa masharti ya ibara hii.
  (2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja
  yoyote ya kutaka kupitisha kura ya kutokuwa na imani na Waziri
  Mkuu haitatolewa Bungeni endapo-
  (a) haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya Waziri
  Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 52 ya Katiba hii, wala
  hakuna madai kwamba Waziri Mkuu amevunja Sheria
  ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
  (b) haijapita miezi sita tangu alipoteuliwa;
  (c) haijapita miezi tisa tangu hoja ya namna hiyo
  ilipotolewa Bungeni na Bunge likakataa kuipitisha.
  (3) Hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu
  haitapitishwa na Bunge isipokuwa tu kama-
  (a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa
  mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya
  Wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku angalau kumi
  na nne kabla ya siku inapokusudiwa kuwasilishwa
  Bungeni;
  (b) Spika atajiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili
  ya kuleta hoja yametimizwa.
  (4) Hoja iliyotimiza masharti ya ibara hii itawasilishwa Bungeni
  mapema iwezekanavyo kwa mujibu wa Kanuni za Bunge.
  (5) Hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa tu
  iwapo inaungwa mkono na Wabunge walio wengi.
  (6) Endapo hoja ya kura ya kutokuwa na imani kwa Waziri
  Mkuu itaungwa mkono na Wabunge wengi, Spika atawasilisha
  azimio hilo kwa Rais, na mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote
  vile ndani ya siku mbili tangu Bunge lilipopitisha azimio la hoja ya
  kura ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu
  atatakiwa ajiuzulu, ................................
   
 8. Biohazard

  Biohazard JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,002
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  Topic closed
   
 9. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  News za uhakika ni kuwa kisemeo, aka SPEAKER bi kiroboto yuko mtwaraaa.
   
 10. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
 11. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,124
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Zimeshatimia
   
Loading...