Zitto, Chukua posho za vikao peleka jimboni kwako!


Tulimumu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Messages
10,356
Likes
6,715
Points
280
Tulimumu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2013
10,356 6,715 280
Mh. Zitto Kabwe aliamua kuacha kuchukua posho za vikao vya bunge akipinga malipo hayo kuwa ni matumizi mabaya ya pesa za umma kwakuwa vikao vya bunge ni sehemu ya majukumu ya mbunge ambapo analipwa mshahara na posho mbali mbali nje ya vikao ndani ya bunge. Mimi ningemshauri Zitto kuchukua posho zote anazositahili kulipwa kama mbunge ambazo anaona si halali na kuzipeleka jimboni kwake zote katika huduma za jamii kama elimu, afya na hata kusaidia makundi maalumu ya wajane, walemavu, vijana na yatima ili kuonesha kwa vitendo kuwa posho zile zikipelekwa kwa wananachi zitawasaidia sana kujikwamua na ugumu wa maisha unao wakabili badala ya kuwalipa wabunge ambao tayari wana mishahara mikubwa, mikopo na posho mbali mbali nje ya posho ya vikao.

Mimi naona mh. ni kama mtu anayeuza ng'ombe ili kushinda kesi ya kuku. Sasa kuna faida gani? Wananchi jimboni kwake wanashida na hawapati huduma muhimu na yeye mh. kasusia posho. Suala la posho naona ni suala la kikanuni, kibajeti na kisheria.Maana yake ni kuwa Zitto kama hachukui posho anayostahili huenda posho yake ikarudishwa hazina au ikaliwa na wajanja kwakuwa tayari iko katika fungu la malipo. Anaonaje kama posho yake ingewasaidia wananchi wa jimboni kwake na au sehemu nyingine hapa nchini wenye shida kubwa. Mimi nadhani Mh. angeendelea kupokea posho yake halali huku akiipinga na kuonesha kuwa anaipinga angekuwa anatangaza moja kwa moja kuwa posho hizo si halali kwao na kuwa anazi[pokea na kuwarudishia wananchi kama nilivyoeleza hapo juu. Mimi najiuliza toka ameacha kuchukua posho hiyo sijui jumla yake sasa itakuwa imefikia milioni ngapi?(lada atatupa jibu) Na je akizichukua zote leo(maana ni haki yake) hazitoshi kumaliza tatizo la madawati katika shule mbili au tatu jimboni kwake? haziwezi kununua ambulance katka hospitali mojawapo huko jimboni kwake au mkoani? hazitoshi kutoa kama msaada kwa vikundi mbali mbali vya wajasilia mali jimbon kwake?, hazitoshi kulipia karo watoto wanaokosa karo jimboni? Hakika kuna mambo mengi ambayo mh. angeweza kuyafanya na kuyatolea taarifa hata bungeni ili kuonesha uzalendo wake na kuliamsha bunge kuwa linawadhulum wananchi. Mh. Kakusanye posho zako zote ulilzozisusia peleka jimboni kwako kwa maendeleo ya jimbo lako na wananchi kwa ujumla. Kama ni msimamo kisiasa umeshaeleweka.
 

Forum statistics

Threads 1,252,104
Members 481,989
Posts 29,795,473