Zitto: CHADEMA walifanya makosa haya ndiyo maana Lowassa akawakimbia, sisi hatutayafanya kwa Membe

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,224
113,554
Nimemsikiliza Zitto na sababu yake/ zake kwanini suala la Membe kuhamia kwenye chama chake halitokuwa kama ilivyokuwa kwa CHADEMA na Lowassa na Sumaye na wengineo.

Sababu zake kuu ni kwamba hao waliohamia CHADEMA kipindi kile hawakujiona au hawakuonekana kuwa ni sehemu ya ‘movement’.

Pia, eti hawakujiona au kuonekana kuwa walikuwa ni sehemu ya ‘familia’ ya CHADEMA.

Muda utazungumza tu. Ila Zitto inabidi awe mwangalifu na uchaguzi wa maneno yake.

Kwenye hili nadhani Bw. Zitto anaathiriwa na kuwa ‘prisoner of the moment’.

Natumaini yeye na ACT yake watakuwa na mipango baada ya uchaguzi ujao baada ya kushindwa.

Maana ushindi huwaunganisha watu na ushindwaji hugawanyisha.
 
Zitto anaongea tu, miaka yote ya utumishi wa Membe huko Serikalini aliwahi kumsikia Membe anaongea/kutetea chochote kwa maslahi ya wapinzani? Labda kuhusu tume huru,sheria mbovu za uchaguzi etc

Atakuja hapa atoe majibu ya siasa haina adui wa kudumu bla bla bla.

Membe ni Lowassa part 2 yule.
 
Thank you 🙏🏽 👊🏽👊🏽👊🏽 Huyo Zitto kaanza kuongea ujinga ujinga Chadema wamuangalie kwa umakini mkubwa sana.

Zitto anaongea tu miaka yote ya utumishi wa Membe huko Serikalini aliwahi kumsikia Membe anaongea/kutetea chochote kwa maslahi ya wapinzani?Labda kuhusu tume huru, sheria mbovu za uchaguzi etc.

Atakuja hapa atoe majibu ya siasa haina adui wa kudumu bla bla bla

Membe ni Lowassa part 2 yule.
 
Zitto anaongea upuuzi tu,miaka yote ya utumishi wa Membe huko Serikalini aliwahi kumsikia Membe anaongea/kutetea chochote kwa maslahi ya wapinzani?Labda kuhusu tume huru,sheria mbovu za uchaguzi etc

Atakuja hapa atoe majibu ya siasa haina adui wa kudumu bla bla bla.

Membe ni Lowassa part 2 yule.
Membe wakati akiwa mnufaika wa mfumo wa CCM aliwahi kweli kuhoji kuhusu u huru wa tume ya uchaguzi?

Au kaanza majuzi hapa baada ya kutimuliwa?
 
Zitto anajua fika kwamba Bara Chadema ni more popular kuliko chama chake lakini anafanya juu chini kutaka Membe ndiye awe mgombea wa Upinzani. Chadema wasikubali upuuzi wake. Anataka kuweka mgombea mmoja basi ni Lissu tu na si Membe.

Kabisa kabisa mkuu,na sasa hivi kila wakiongea Membe/Zitto ni lazima kusema inabidi kusimamisha mgombea mmoja.

Naona wana agenda yao wale.
 
Mahojiano mazuri, amefafanua vizuri Mh. Zitto Kabwe.

Upinzani lazima tushiriki ktk uchaguzi kuzuia nchi kurudi ktk mfumo wa 'chama kimoja' .

CCM Mpya pia imefanya makosa hayohayo na itawa gharimu ktk uchaguzi kwani hakuna anayepigiwa chapuo zaidi ya mtu mmoja mwenye serikali yake ndiyo anayegawa fedha kununua korosho, kuwabagua wanaCCM wa zamani.

Uchaguzi huru ndani ya chama

Breaking News !


Dr. Faustine Engelbert Ndugulile ashinda kura za maoni za ndani ya chama cha CCM jimbo la Kigamboni jijini Dar es Sakaam.

Kura za maoni za wajumbe halali zilikuwa 399 hakuna kura iliyoharibika na Dr. Faustine Engelbert Ndugulile amefanikiwa kupata kura 190 za wajumbe hao wa mkutano wa wilaya ya Kigamboni..

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kutumbuliwa kwa kilichoitwa 'tamaa' isiyokubalika ndani ya CCM Mpya Bw. Paul Christian Makonda amepata kura 122.
 
Na
Membe wakati akiwa mnufaika wa mfumo wa CCM aliwahi kweli kuhoji kuhusu u huru wa tume ya uchaguzi?

Au kaanza majuzi hapa baada ya kutimuliwa?
Lowasa naye alikuwa hivyo hivyo mpka yalipomkuta. Na walimyosha kweli kweli wakati mwingine nilifurahi kuukosa urais ili hata kama akifa na uzee wake aondoke na maumivu aliyowafanyia wengine kwa kushiriki na kubariki sheria kandamizi.
 
Zitto anajua fika kwamba Bara Chadema ni more popular kuliko chama chake lakini anafanya juu chini kutaka Membe ndiye awe mgombea wa Upinzani. Chadema wasikubali upuuzi wake. Anataka kuweka mgombea mmoja basi ni Lissu tu na si Membe.
Naunga hoja kwa 100% mkuu.
 
Back
Top Bottom