Zitto: CCM hawaaminiani wala kuthaminiana

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,681
2,000
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe, amesema utitiri wa wagombea urais kupitia CCM kunaonyesha dalili ya wao wenyewe kutoaminiana, kutothaminiana na kimepoteza hazina ya viongozi.

Aidha, alisema kazi ya urais ingekuwa inachukuliwa kwa uzito wagombea wa CCM wasingefikia 10 badala yake imeonekana nikazi nyepesi na imerahisishwa na CCM.

Kabwe alisema sifa 13 pekee za wagombeawa CCM ni nyepesi ndio maana kila mmoja anajiona anaweza kuwa kiongozi wa nchi.

Akizungumza jana mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, Kabwe alisema moja ya sifa ya chama cha ACT-Wazalendo ni wagombea kufuata masharti kwa kutangaza mali na madeni ikiwamo kufuata miiko ya viongozi iliyotangazwa na Azimio la Tabora.

Kabwe aliwataja viongozi hao kuwa ni wa kitaifa wa chama, rais, mawaziri, wabunge na madiwani watakaotokana na chama hicho.

Aliongeza kuwa ili kubomoa mfumo wa kinyonyaji na kifisadi miongoni mwa viongozi, chama hicho kimeamua kurejesha miiko ya uongozi na kuishia ambayo imehusishwa kutokana na Azimio la Arusha."Chama kinamtaka kiongozi katika uongozi wa umma asiwe mkurugenzi katika kampuni au shirika la umma, awe wazi na vyanzo vyake vya mapato, mali alizonazo kwa kuzingatia utaratibu wa sheria ya nchi na kanuni za mwenendo na maadili ya viongozi," alisema Kabwe.

Pia, alisema kiongozi anatakiwa asiwe mfanyabiashara wa aina yoyote katika chama na serikali anapokuwa kwenye nafasi ya uongozi.

Alisema tangu wagombea hao waanze kutangaza nia hakuna mgombea urais aliyetamka neno miiko isipokuwa Samuel Sitta pekee, licha ya kuahidi kupambana narushwa pamoja na ufisadi."Nitolee mfano nchi ya Canada, Uingereza, Marekani wana miiko lakini Tanzania tunageuza uongozi kuwa kichaka cha wezi kwa kutupa miiko pembeni," alisema Kabwe.

Chanzo:
NIPASHE
 
mtAkI360

Member
Nov 10, 2014
96
95
Maneno ya zito huwa yana uzito na yaliyopangiga kwa mifano dhahiri na ndio kiongozi unastahili kuwa hivyo. Tanzania inapaswa tubadili mfumo wa uongozi kabisa.
 
Masonjo

JF-Expert Member
Aug 8, 2010
2,724
1,195
Hii ni hoja ya msingi sana, uongozi ni lazima uanzie kwanza kwenye maadili,ni lazima tuondoe hii kasumba ya kuufanya uongozi kuwa ni msingi mzuri wa kupiga deal za kibiashara.
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
107,505
2,000
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe, amesema utitiri wa wagombea urais kupitia CCM kunaonyesha dalili ya wao wenyewe kutoaminiana, kutothaminiana na kimepoteza hazina ya viongozi.

Aidha, alisema kazi ya urais ingekuwa inachukuliwa kwa uzito wagombea wa CCM wasingefikia 10 badala yake imeonekana nikazi nyepesi na imerahisishwa na CCM.

Kabwe alisema sifa 13 pekee za wagombeawa CCM ni nyepesi ndio maana kila mmoja anajiona anaweza kuwa kiongozi wa nchi.

Akizungumza jana mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, Kabwe alisema moja ya sifa ya chama cha ACT-Wazalendo ni wagombea kufuata masharti kwa kutangaza mali na madeni ikiwamo kufuata miiko ya viongozi iliyotangazwa na Azimio la Tabora.

Kabwe aliwataja viongozi hao kuwa ni wa kitaifa wa chama, rais, mawaziri, wabunge na madiwani watakaotokana na chama hicho.

Aliongeza kuwa ili kubomoa mfumo wa kinyonyaji na kifisadi miongoni mwa viongozi, chama hicho kimeamua kurejesha miiko ya uongozi na kuishia ambayo imehusishwa kutokana na Azimio la Arusha.“Chama kinamtaka kiongozi katika uongozi wa umma asiwe mkurugenzi katika kampuni au shirika la umma, awe wazi na vyanzo vyake vya mapato, mali alizonazo kwa kuzingatia utaratibu wa sheria ya nchi na kanuni za mwenendo na maadili ya viongozi,” alisema Kabwe.

Pia, alisema kiongozi anatakiwa asiwe mfanyabiashara wa aina yoyote katika chama na serikali anapokuwa kwenye nafasi ya uongozi.

Alisema tangu wagombea hao waanze kutangaza nia hakuna mgombea urais aliyetamka neno miiko isipokuwa Samuel Sitta pekee, licha ya kuahidi kupambana narushwa pamoja na ufisadi.“Nitolee mfano nchi ya Canada, Uingereza, Marekani wana miiko lakini Tanzania tunageuza uongozi kuwa kichaka cha wezi kwa kutupa miiko pembeni,” alisema Kabwe.

Chanzo:
NIPASHE

Hivi ile kampuni ya lekadutigite zzk yeye siyo mkurugenzi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom