Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,278
- 25,846
Imeripotiwa kuwa Wabunge kadhaa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemwandikia barua Spika wa Bunge kujiuzulu ujumbe wao wa Kamati za Bunge. Wabunge hao ni pamoja na Zitto Kabwe,Hussein Bashe na Sixtus Mapunda wa Kigoma Mjini,Nzega Mjini na Mbinga Mjini. Wanadai Kamati zao zimetuhumiwa kwa rushwa.
Naziona barua zao na lengo lao kama usanii uliopindukia wa kisiasa. Kwanza,hakuna kanuni yoyote ya Bunge waliyoitaja au inayoruhusu kujiuzulu kwao. Pili,kila Mbunge ni Mjumbe wa Kamati mojawapo ya Bunge. Kanuni za Bunge haziruhusu Mbunge kuwa bila Kamati. Sasa hata wakijiuzulu,watabaki vipi bila Kamati?
Wabunge hawa pamoja na wenzao waliofanya au watakaofanya hivyo-kujiuzulu ujumbe wa Kamati wanafanya usanii. Kama Wabunge hao wameguswa na tuhuma zao na wanalenga kuonekana wazalendo,wajiuzulu Ubunge wao moja kwa moja. Kimsingi,barua zao ni ujanja na usanii wa kutaka kubadilishiwa Kamati.