Zitto aweka pingamizi Mahakamani kuzuia Kikao cha Kamati Kuu kujadili rufaa yake kesho

Status
Not open for further replies.

ithangaledi

Member
Jun 4, 2011
84
70
Wana Jf,

Taarifa ambazo zimenifikia hivi punde ni kuwa Zitto Kabwe ameweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kesho.

Hoja yake ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.

Anadai anataka mahakama iagize kamati kuu kutojadili suala lake mpaka baraza kuu likae kuamua rufaa yake.

Wanasheria wa Chama wakiongozwa na Tundu Lissu wanaenda Mahakamani kusikiliza pingamizi hilo ambalo litakuwa limeenda kwa hati ya dharura.

Nitawaletea kinachoendelea.

Ithangaledi

Update,

1. Wakili wa ZZK ni Alberto Msando.

2. Mawakili wa pande zote wapo Mahakamani.

3. Msando ndiyo ameruhusiwa kuanza kuwasilisha.

4. Jaji Utamwa ndiye anayesikiliza pingamizi hilo

============
Itaendelea KESHO:
- Imetolewa interim order kuwazuia CHADEMA kujadili suala hili mpaka kesho ili wajibu hoja zao baada ya objections zilizowasilishwa na mawakili wa chama kukataliwa.
Mahakama imeamua kamati kuu iendelee baada ya mwanasheria wa Zitto kuweka pingamizi kuzuia Kamati Kuu Kesho

Pia Mahakama imeamua kuwa mashtaka dhidi ya viongozi waliovuliwa madaraka ambao wana mashtaka Dr.Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba yaendelee kujadiliwa Kesho na kamati kuu bila kizuizi chochote

Aidha,Kesho asubuhi Mahakama itatoa uamuzi juu ya pingamizi lililowekwa na Zitto Kabwe juu ya kamati kuu kujadili suala lake
 

MWAKISALU

Senior Member
Nov 1, 2013
100
225
ndugu wanachama wa chama cha democrasia na maendeleo nakuombeni tulieni. mahakama itatoa rulling on monday. nilikuwepo mahakamani kuanzia mwanzo mpaka mwisho. nimesikiliza hoja za pande zote mbili yaani plaintiff vs defendant.

kiukweli kama judge atafuata principle of law na judgement zake zika-base kwenye facts and arguments za pande zote mbili, zzk is likely to loose the case. kikawaida duniani kote ili uwe na base ya kukimbilia mahakamani kwa shauri ambalo lina katiba yake basi ni lazima uwe ume-meet all local remedies na uhakikishe kuwa hakuna tena mahara pa kukata rufaa kwa mujibu wa katiba ya chama chako ndipo utakuwa na locus stand ya kutafuta msaada wa mahakama. someni kesi ya mtikila vs republic na baadaye akafungua kesi mahakama ya africa mara baada ya kushindwa kupata haki yake ktk mahakama za ndani

huwezi ukawa malaika wa kubashiri eti kamati kuu itaamua kunivua uanachama, how did u know this?.

nawashukuru mawakili wote wamefanya kazi yao vizuri ktk kutetea wateja wao.

lakini ndugu zangu kusema ukweli kwa dhati ya moyo wangu namhurumia sana zzk. what i know is that mambo ya kichama mahakama si mahala pake. sijawahi kuona mtu wa ccm hata kama ameonewa akakimbilia mahakamani, kama kamati kuu imekuvua uongozi thanks god kwamba imekupunguzia mzigo wa majukumu. uongozi ni mzigo ndugu zangu, muda wote unaumiza kichwa.

kama zzk ingetokea aniombe ushauri i could frankly tell him kwamba kubali kustep down pumzika endelea na ubunge wako tu maana kwa kufanya hivyo angepunguza majukumu na kupata muda mwingi wa kuwahudumia watu wake waliomchagua kuliko kuwa naibu katibu mkuu wa chama mara pac n.k. wanachama wote jifunzeni kwamba mambo ya chama mara zote humalizwa ndani ya chama si mahakamani tena.

hoja nyingine ya msingi ni kwamba mnapokuwa mnapigania jambo fulani kutaka kuleta mabadiliko kwa kutoriziashwa na system iliyopo kwa sasa huwa hatugombanii mimi nipate cheo gani, huwa tunaangalia namna ya kufikia kwanza adhma yetu ya kuondoa system hiyo ndipo mambo mengine yafuate.

mke na mume wakigombana ndani ya matrimonial house yao na wakawa hawaongei wanachukiana kwelikweli, mara ikatokea kibaka kaingia ndani mwao, watu hawa wataungana kumpiga kibaka watasahau tofauti zao kwa kuwa lengo lao ni moja la kumuondoa mvamizi ndani mwao, wakifanikisha hili baadaye suala la kutatua tofauti zao litafuata wakiwa ktk mazingira ya amani. vyama fuateni mfano huu.

zzk jifunze kufuata mfano huo hapo juu japo ni haki yako kikatiba kuomba msaada wa mahakama, lakini suala la muda gani kuomba msaada wa mahakama ni jambo la msingi sana. zaidi ya yote napenda chama kiendelee kukua maana maendeleo huletwa na utofauti wa kifikra ambazo ni positive na siyo negative tena kama ilivyo ktk suala hili. asnateni sana ndugu zangu. tambueni kuwa tz ni muhimu zaidi ya maisha yetu.
 

Mfichua siri

Senior Member
Jun 19, 2012
135
0
Duu!! kuna matatizo gani ya kisheria kayastukia mpaka anaenda ku-challenge kukaliwa kwa kikao? Tupe updates ukizipata basi.
 

Maswala

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
560
225
Wana Jf,

Taarifa ambazo zimenifikia hivi punde ni kuwa Zitto Kabwe ameweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kesho.

Wanasheria wa Chama wakiongozwa na Tundu Lissu wanaenda Mahakamani kusikiliza pingamizi hilo ambalo litakuwa limeenda kwa hati ya dharura.

Nitawaletea kinachoendelea.

Ithangaledi

Kama hili ni kweli sasa ZZK amejianika! Sasa ni dhahili kuwa ana matatizo!
 

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,298
2,000
Wana Jf,

Taarifa ambazo zimenifikia hivi punde ni kuwa Zitto Kabwe ameweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kesho.

Wanasheria wa Chama wakiongozwa na Tundu Lissu wanaenda Mahakamani kusikiliza pingamizi hilo ambalo litakuwa limeenda kwa hati ya dharura.

Nitawaletea kinachoendelea.

Ithangaledi

Anazuia kikao au maamuzi ya kikao? Si angesubiri akawekea pingamizi maamuzi ya kikao? Au keshadodoswa ajenda nini?
 

Mbundumale

Senior Member
Dec 30, 2013
150
0
Kama ni kweli,ZITTO hatufai kwenye chama. Najiuliza anapata wapi ujasiri wa kuzuia kamati kuu wakati anajua kwamba maamuzi ya hatma yake na utetezi wake ndio utakaotolewa maamuzi.


Sasa anaweka pingamizi mahakamani kufanyika kwa kikao cha kamati kuu ili iweje??? Hatma ya jambo hili litamalizikaje????


Mimi nadhani angeweka pingamizi mahakamani baada ya maamuzi kufanyika na si kabla. Mfano,kama maamuzi yamefanyika kwamba avuliwe uanachama wake ndio angekwenda mahakamani kupinga kama anaona kaonewa.

ZITTO hakitakii mema CHADEMA, Tumpuuze.
 

Tumaini Makene

Verified Member
Jan 6, 2012
2,619
1,500
Kikao Maalum cha Kamati Kuu kesho, 3 Januari 2014, Jijini Dar Es Salaam kitakuwa na ajenda kuu tatu:

Mosi; Mchakato wa Katiba Mpya

Pili; Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka 2014

Mpango Kazi wa chama ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chama wenye dhima ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya chama na taifa.

Tatu; Kupokea utetezi wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao na

Kuhusu Wanachama watatu walishajulishwa makosa yao kwa maandishi na wamewasilisha utetezi wao wa maandishi. Wataitwa kwenye kikao kwa kuzingatia matakwa ya kanuni 6.5.2 (b) na 6.5.2 (d), kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.

 

Maswala

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
560
225
Wana Jf,

Taarifa ambazo zimenifikia hivi punde ni kuwa Zitto Kabwe ameweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kesho.

Wanasheria wa Chama wakiongozwa na Tundu Lissu wanaenda Mahakamani kusikiliza pingamizi hilo ambalo litakuwa limeenda kwa hati ya dharura.

Nitawaletea kinachoendelea.

Ithangaledi

Hivi si alisema anajiamini, kuwa anapendwa? Sasa si aache chama kiamue na akubaliane na maamuzi ya chama? ZZK atamwongoza nani, wakati hawamtaki?

Anafata nyayo za Rashi na Kafulila! Wako wapi leo?
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom