Zitto awazindua Wasanii: 153 wameshasaini kuvunja mkataba

ukiisoma vizuri yaonesha imeandikwa na mtu wa mtaani tu we toka lini hao wasanii 153 wakasaini kwa pamoja hiyo mikataba na mitandao ya simu?

Mbona anae wawakilisha wasanii hajasaini hiyo taarifa?

Je tuamini kuwa walikuwa na mkataba na hao wasanii,kama kweli inakuwaje wanauvunja kihuni?
Mbona huo mkataba haujawasilishwa ili tuweze judge kama ni kweli?

Je kuna umoja wa wasanii hapa tz unaoshirikisha waimba nyimbo za dini na bongo flavor?
Cosota wako wapi kuwatetea hawa wasanii hadi wajitetee wenyewe?
Naomba msaada hapa
 
Zitto si ndio kawafunguwa macho? hata Sugu alikuwa halijui hilo na yeye ni mbunge na msanii wa hali ya juu, msanii kweli kweli tena.
 
kwani wasanii wa nyimbo za dini nao wanataka haki gani wakati ring tone zinaeneza ujumbe wa neno la mungu? kwa maoni yangu muziki wa dini ni sadaka na si biashara ,kwahiyo kuwazuia makampuni ya simu ni sawa na kuweka makwazo kwa neno la mungu!

Ili neno lienee zaidi lazima malipo yafanyike ili msanii aweze kurekodi ujumbe mpya!, ndio kazi hasa ya sadaka. hata viongozi wa dini wanalipwa kutoka ktk sadaka ili na kesho wahubiri tena.
 
Kile kinachoonekana ni hali ya ukomavu na kujiamini,Mbunge wa kigoma kaskazini amekuwa ndiye njia ya kuwafuta machozi wa sanii nchini mara baada ya kuafanikiwa kuwaelewesha na kuwafumbua macho wasanii nchini juu ya wizi unaofanywa na mitandao ya simu.

Leo wasanii wa mziki wa dini na wakidunia wameungana kusikiliza wito wa Mh.zitto wa kuwataka wakubali kuungana kwa kusaini partition maalumu kwaajili ya kusitisha mikataba yao juu ya CALLERTUNE za mitandao ya simu.

Hii ni mara baada ya Mbunge huyu kutambua kuwa wasanii wanaibiwa na kunyonywa juu ya malipo halali ambayo waliatakiwa walipwe kutokana na huduma hiyo.

Jana mbunge huyo licha ya kuwa na mtikisiko wa wa kuhusishwa na rushwa alikuwepo jijini dar es salaam kuongea na wasanii juu ya kusitisha mikataba yao juu mitandao ya simu.

Mh.zito kabwe kupitia utendaji huu wa kazi ni dhahili amezamilia kuujulisha umma kuwa yeye ni mchapa kazi,na mtetea haki za wanyonge.

Mtandao wa Tigo unamarumbano makubwa na zitto mara baada ya Mbunge huyu kufichua uozo wa tigo kwamba hawalipi kodi hata cent moja kwenye bunge lililopita. Serikali imekuwa kimya kujibu tuhuma hizi.

JF nawasilisha
 
Usipotambua na Usipodai haki yako mwenyewe usitegemee mtu atakusimamia. Ndo maana madaktari, walimu, wana-NSSF nao wanasimama kudai haki yao. makampuni mengi sana nchi ni wezi na hata kodi ninawasiwasi kama wanalipa vizuri.

Kutwa nzima ni promotions na kamari. imefikia kipindi sasa waTz tunaishi kwa kutegemea promotion na kamari za makampuni ya simu badala ya kufanya kazi.

Hii inatokana na sera hafifu za serikali kuyabana makampuni haya badala ya kupromote unzinzi na ulevi sasa wangegeuzia kwenye elimu, afya na kilimo maana nchi yetu bado masikini.

Kwa ujumla nimeipenda sana hii muvu ya wasanii kama watasimama kidete kuyabana makampuni (wezi) basi nina uhakika watafaidika na kazi zao.
 
Hahaaaa yaani kila kitu Zitto tu! Kaazi kweli kweli.

Sitashangaa keshokutwa walimu nao wakianza kumlaumu Zitto.

Zitto aliongea hili suala bungeni last 2 weeks nadhani ndo maana wanamuhusisha.lakini huwezi kujua inawezekana CHADEMA ni kampni ya simu maana wajasiriamali hawa...
 
good move kwa wasanii, ila sio zitto aliyefichua hii issue ni Citizen magazine na zitto alidandia tu hoja kama kawaida yake, wasanii wanaibiwa na watu wengine simo makampuni ya simu, hii mada imepotoshwa sana by the way nawasikitikia sana wasanii maana wanaruka mkojo wanaenda kukanyaga mavi,! kwasasa wanaingia mkataba na company ya ruge, business as usual
 
Msimpaishe hivyo Zito Gt walileta hiyo kitu hapa jamvini hata kabla Zito ajaitoa Bungeni nafikiri yy kaitoa humu ikiwa vilevile alivyoipresent
 
Msimpaishe hivyo Zito Gt walileta hiyo kitu hapa jamvini hata kabla Zito ajaitoa Bungeni nafikiri yy kaitoa humu ikiwa vilevile alivyoipresent

Correct!!!! hata mimi nilianza kuisoma humu jf kabla bwana zzk hajairusha bungeni.
 
PRESS RELEASE:
YAH: KUFUTA MIKATABA NA KUSIMAMISHA KUUZA MUZIKI WA BONGO FLEVA,GOSPEL,DANSI NA TAARABU KWENYE MITANDAO YA SIMU.
Husika na kichwa cha habari hapo juu,
Kwa ujumla wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya muziki wa Gospel, Rhumba , Taarabu pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agzio kwenu la kusimamisha mauzo ya kazi zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na Callertunes katika mitandao ya simu ya Vodacom, Zantel,Tigo na Airtel na kufuta mkataba tuliosaini kati yetu sisi Wasanii na Kampuni yako mpaka hapo tutakapokaa sisi kama wasanii, nyinyi kama wasambazaji wa muziki wetu, pamoja na Mitandao ya simu ili kuzungumzia namna mpya ya sisi na nyinyi tutakavyofanya kazi.

Sababu ya sisi Wasanii kusimamisha na kufuta mikataba kati yetu na wanaofanya biashara ya kuuza maudhui yetu ni pamoja kampuni husika kushindwa kuweka wazi taarifa za mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda husika kama ilivyoanishwa katika mikataba husika.
Sababu ya pili ni mitandao ya simu kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni asilimia themanini ya mauzo yote ya maudhui yetu, jambo hili linatuumiza na limetufanya tuendelee kuishi kwa kutegemea aina moja ya pato toka kwenye shoo.

Hivyo tumeziagiza kampuni zote zinazofanya kazi ya kuuza maudhui yetu kutoa maelekezo kwenye mtandao husika kuwaelekeza kusimamisha mauzo ya kazi zetu za sanaa ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 30/07/12 ikiwa pamoja na kusimamisha matangazo yote yanayotangaza mauzo ya kazi zetu kwa njia ya Television , Radio , blogs, website, Magazeti na Ujumbe Mfupi wa maneno mpaka hapo tutakapofikia muafaka.

Jumla ya wasanii 153 wameshasaini barua hizo na wengine wanaendelea kusaini.
Mwisho tunawashukuru kwa ushirikianao wenu, na tunaambatanisha sahihi zetu ili kuonyesha uthibitisho wa umoja wetu katika jambo hili.

Asante.


NAAAM! KUMEKUCHA!

Sasa hizi ndio harakati zinazotakiwa! Hakuna tena danganya toto! Wizi sasa basi!
 
Wakati wanaingia mikataba, wameingia kimya kimya na kila mtu kivyake....mbona wanataka kutoka kwa kelele na kama kundi? Hii press release ina nguvu gani ya kisheria hasa ukizingatia uwepo wa mikataba...isije ikawa ni kupoteza muda na rasilimali (hasa kama watakubali kutumika kwa manufaa ya wanasiasa bila kuwa makini na kuwa na uhakika wa kile wanachikipigania).

Mikataba yao inasemaje kuhusiana na kuvunja/kuvunjika? Kwa kuwa muziki ni biashara, je suala hili wanamuziki linaendana vipi na sheria ya ushindani wa kibiashara (The Fair Competition Act, 2003)? Ni vema wasanii wakawa makini katika masuala haya yahusuyo mikataba ambayo inaweza ku-back fire kwa individual musicians na sio kwa group (maana sio group la hao wanamuziki 153 lilioingia mkataba na makampuni ya simu)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom