you are a great thinker
kichwa cha habari na taarifa uliyotoa haviendani kajipange upya
kwani wasanii wa nyimbo za dini nao wanataka haki gani wakati ring tone zinaeneza ujumbe wa neno la mungu? kwa maoni yangu muziki wa dini ni sadaka na si biashara ,kwahiyo kuwazuia makampuni ya simu ni sawa na kuweka makwazo kwa neno la mungu!
PRESS RELEASE:Husika na kichwa cha habari hapo juu,
YAH: KUFUTA MIKATABA NA KUSIMAMISHA KUUZA MUZIKI WA BONGO FLEVA,GOSPEL,DANSI NA TAARABU KWENYE MITANDAO YA SIMU.
Kwa ujumla wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya muziki wa Gospel, Rhumba , Taarabu pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agzio kwenu la kusimamisha mauzo ya kazi zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na Callertunes katika mitandao ya simu ya Vodacom, Zantel,Tigo na Airtel na kufuta mkataba tuliosaini kati yetu sisi Wasanii na Kampuni yako mpaka hapo tutakapokaa sisi kama wasanii, nyinyi kama wasambazaji wa muziki wetu, pamoja na Mitandao ya simu ili kuzungumzia namna mpya ya sisi na nyinyi tutakavyofanya kazi.
Sababu ya sisi Wasanii kusimamisha na kufuta mikataba kati yetu na wanaofanya biashara ya kuuza maudhui yetu ni pamoja kampuni husika kushindwa kuweka wazi taarifa za mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda husika kama ilivyoanishwa katika mikataba husika.
Sababu ya pili ni mitandao ya simu kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni asilimia themanini ya mauzo yote ya maudhui yetu, jambo hili linatuumiza na limetufanya tuendelee kuishi kwa kutegemea aina moja ya pato toka kwenye shoo.
Hivyo tumeziagiza kampuni zote zinazofanya kazi ya kuuza maudhui yetu kutoa maelekezo kwenye mtandao husika kuwaelekeza kusimamisha mauzo ya kazi zetu za sanaa ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 30/07/12 ikiwa pamoja na kusimamisha matangazo yote yanayotangaza mauzo ya kazi zetu kwa njia ya Television , Radio , blogs, website, Magazeti na Ujumbe Mfupi wa maneno mpaka hapo tutakapofikia muafaka.
Jumla ya wasanii 153 wameshasaini barua hizo na wengine wanaendelea kusaini.
Mwisho tunawashukuru kwa ushirikianao wenu, na tunaambatanisha sahihi zetu ili kuonyesha uthibitisho wa umoja wetu katika jambo hili.
Asante.
Kwanza suala hili halihusiani na siasa umeamua kutaja jina la Zitto ili kuiingiza humu, humu sio mahala pake peleka kwingine
Hivi kumbe mtu ukimshtua mwenzio kuwa anaibiwa unaweza kuingia matatizoni ee...? Sijapata logic...Zitto amehusika sana kuwashtua wasanii kwa jinsi wanavyoibiwa mapato ya kazi zao, nafkiri wote tuliskia hotuba yake bungeni. Makampuni ya simu hayakaa kimya, tusubiri tuone kitakachofuata.
Hivi kumbe mtu ukimshtua mwenzio kuwa anaibiwa unaweza kuingia matatizoni ee...? Sijaona logic...Zitto amehusika sana kuwashtua wasanii kwa jinsi wanavyoibiwa mapato ya kazi zao, nafkiri wote tuliskia hotuba yake bungeni. Makampuni ya simu hayakaa kimya, tusubiri tuone kitakachofuata.
kwani wasanii wa nyimbo za dini nao wanataka haki gani wakati ring tone zinaeneza ujumbe wa neno la mungu? kwa maoni yangu muziki wa dini ni sadaka na si biashara ,kwahiyo kuwazuia makampuni ya simu ni sawa na kuweka makwazo kwa neno la mungu!
Usituhamishe CD, linalomhusu Zitto kwa sasa ni kashfa ya rushwa.