Zitto awazindua Wasanii: 153 wameshasaini kuvunja mkataba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto awazindua Wasanii: 153 wameshasaini kuvunja mkataba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by lodrick, Jul 31, 2012.

 1. l

  lodrick Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  PRESS RELEASE:
  YAH: KUFUTA MIKATABA NA KUSIMAMISHA KUUZA MUZIKI WA BONGO FLEVA,GOSPEL,DANSI NA TAARABU KWENYE MITANDAO YA SIMU.
  Husika na kichwa cha habari hapo juu,
  Kwa ujumla wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya muziki wa Gospel, Rhumba , Taarabu pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agzio kwenu la kusimamisha mauzo ya kazi zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na Callertunes katika mitandao ya simu ya Vodacom, Zantel,Tigo na Airtel na kufuta mkataba tuliosaini kati yetu sisi Wasanii na Kampuni yako mpaka hapo tutakapokaa sisi kama wasanii, nyinyi kama wasambazaji wa muziki wetu, pamoja na Mitandao ya simu ili kuzungumzia namna mpya ya sisi na nyinyi tutakavyofanya kazi.

  Sababu ya sisi Wasanii kusimamisha na kufuta mikataba kati yetu na wanaofanya biashara ya kuuza maudhui yetu ni pamoja kampuni husika kushindwa kuweka wazi taarifa za mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda husika kama ilivyoanishwa katika mikataba husika.
  Sababu ya pili ni mitandao ya simu kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni asilimia themanini ya mauzo yote ya maudhui yetu, jambo hili linatuumiza na limetufanya tuendelee kuishi kwa kutegemea aina moja ya pato toka kwenye shoo.

  Hivyo tumeziagiza kampuni zote zinazofanya kazi ya kuuza maudhui yetu kutoa maelekezo kwenye mtandao husika kuwaelekeza kusimamisha mauzo ya kazi zetu za sanaa ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 30/07/12 ikiwa pamoja na kusimamisha matangazo yote yanayotangaza mauzo ya kazi zetu kwa njia ya Television , Radio , blogs, website, Magazeti na Ujumbe Mfupi wa maneno mpaka hapo tutakapofikia muafaka.

  Jumla ya wasanii 153 wameshasaini barua hizo na wengine wanaendelea kusaini.
  Mwisho tunawashukuru kwa ushirikianao wenu, na tunaambatanisha sahihi zetu ili kuonyesha uthibitisho wa umoja wetu katika jambo hili.

  Asante.
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Sasa Zitto anahusikaje na mauzo ya muziki kwenye simu? Nadhani yeye ni Mbunge na naibu katibu mkuu wa CHADEMA: je naye ana kampuni ya simu?
   
 3. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,973
  Likes Received: 6,605
  Trophy Points: 280
  Hii hapa ni nzuri lakini lazima baadhi ya wasanii watasaliti tu. Mia
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Jul 31, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hahaaaa yaani kila kitu Zitto tu! Kaazi kweli kweli.

  Sitashangaa keshokutwa walimu nao wakianza kumlaumu Zitto.
   
 5. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,973
  Likes Received: 6,605
  Trophy Points: 280
  Hii hapa ni nzuri lakini lazima baadhi ya wasanii watasaliti tu. Mia
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  zitto alichofanya ni kuwatetea wanamuziki......
   
 7. l

  lodrick Member

  #7
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Zitto amehusika sana kuwashtua wasanii kwa jinsi wanavyoibiwa mapato ya kazi zao, nafkiri wote tuliskia hotuba yake bungeni. Makampuni ya simu hayakaa kimya, tusubiri tuone kitakachofuata.
   
 8. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,478
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Kwanza suala hili halihusiani na siasa umeamua kutaja jina la Zitto ili kuiingiza humu, humu sio mahala pake peleka kwingine
   
 9. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  kichwa cha habari na taarifa uliyotoa haviendani kajipange upya
   
 10. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  let me guess!!! labda kwa vile zitto aliwatetea bungeni..labda kawafungua wamejua wanaibiwa na makampuni ya simu...
   
 11. l

  lodrick Member

  #11
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  you are a great thinker
   
 12. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Linahusiana sana, limeongelewa juzi tu hapa na Zitto. Jamani kama hamkusikia siku hiyo msibishe, ZZK amewashtua wasanii usingizini kuwaambia kwamba ringtone zinazotumia nyimbo za wasanii zinanufaisha makampuni ya simu kwa asilimia kubwa compared to msanii mwenyewe. Hakuishia ktk nyimbo tu, kuna adverts nyingi tu zinatumia sanaa, iwe ya ngoma, uchoraji etc. Hawa wasanii wamekurupushwa na kauli ya ZZK, hakuna ubishi kwa hilo.
   
 13. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,296
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Usituhamishe CD, linalomhusu Zitto kwa sasa ni kashfa ya rushwa.
   
 14. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,398
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Kama vile haijakaa sawa! Hii Press Release imetolewa na nani? Haina address ya Mtoaji wala signature ya mtoaji wake (kwa niaba ya hao wanaojitoa) Haitoshelezi kusema wasanii 153 wameshasaini na wegine wanaendelea kusaini. Ama PR hii imeletwa kwa hati ya dharura?
   
 15. l

  lodrick Member

  #15
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Zitto anahusika kwa 110% kwa kinachoendelea hadi kufanya wasanii kufikia hatua waliofikia. Pili ishu hii iliibuka bungeni, hapa ndo mahala pake haswaa.
   
 16. l

  lodrick Member

  #16
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hizi taarifa zimethibitishwa na Mwana Fa na ndo topic kwenye kila redio kwa sasa. unaweza pia kuipata www.millardayo.com
   
 17. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Na usaliti always muradi wake hua ni njaa !
   
 18. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  kwani wasanii wa nyimbo za dini nao wanataka haki gani wakati ring tone zinaeneza ujumbe wa neno la mungu? kwa maoni yangu muziki wa dini ni sadaka na si biashara ,kwahiyo kuwazuia makampuni ya simu ni sawa na kuweka makwazo kwa neno la mungu!
   
 19. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Ok tutaona km kweli wana umoja
   
 20. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Zitto go.........................!
   
Loading...