Zitto awasilisha mapendekezo kuhusu namna bora ya kukabiliana na virusi vya Corona

Hayo yote uliyoongea nayaelewa ila point yangu ni kusema ana 'hutubia taifa' ndio ninachopinga mkuu. Rais au anaemkaimu ndio mwenye mamlaka ya kulihutubia taifa.


Taifa ni nini??, ni wanyama au watu??!!, corona inawahusu wanyama na vitu au inawahusu watu/wananchi??
 
Ni kweli ugonjwa ni siri ya daktari na mgonjwa. lakini covid 19 ni ugonjwa wa ajabu sana maana unaweza kutembea nao bila kujijua na ukawambukiza wengine na wenyewe wasijijue kuwa wameambukizwa. Ugonjwa huu ni janga kwa dunia nzima.sasa kama mgonjwa atagundulika ameambukizwa halafu ikawa siri kwa jamii hatuoni kuwa ugonjwa huu utaendelea kuenea kwa kasi?

kwa maana kama mgonjwa huyu angejulikana wako watu ambao wamekaa na mgonjwa huyu kama wakisikia ndugu yao au rafiki yao alikuwa na ugonjwa huu aidha watajitenga wenyewe(kama alivyofanya Mh mbowe)au wataripoti wenyewe hospitali bila ya kutafutwa.

Gharama ya kuwatafuta contacts wa mgonjwa yaweza kuwa kubwa kuliko kama mgonjwa angekubari atangazwe .labda kinachotakiwa ni kuomba kibari kwa mgonjwa ili jina lake litangazwe lakini kwa kutangazwa sidhani kama ni kumyanyapaa au kumvunjia heshima.

Ugonjwa huu haupatikani kwa kufanya matendo maovu kama vile magonjwa ya ngono,ukimwi hivyo tusioni aibu kujitangaza .ukijitangaza ni njia bora ya kuwakinga ndugu jamaa na marafiki na taifa kwa ujumla .pili ukijitangaza unatupa muda mzuri wa kukuombea ili upone haraka.

haya ni maoni yangu sipingani na waziri au maadili ya madaktari.
 
Back
Top Bottom