Mkuu nakubaliana na hoja zako, lakini kwa jinsi ninavoijua Zimbabwe na interest za Uingereza na US kwa nchi hiyo, nalazimika kusema kwamba ni heri Mugabe akaendelea kuitawala nchi hiyo hata kwa miaka minne zaidi.
MUNGU IBARIKI ZIMBABWE.
Mkuu hapo tupo pamoja swala la zimbabwe linaweza kusubiri tumalize kwanza ya kwetu yanayotuumiza vichwa. kwa kutoa angalizo tu ni kwamba Serikali yetu ifunge ubalozi wetu kule kama wao na itoe tamko kwa watanzania wanaoishi zimbabwe warudi kwanza nyumbani mpaka hapo hali itakapotulia. KODI wanayosaga wabunge pale Dom kwa siku inatisha wakiongeza tena siku kwa swala la ZIMb mmhh!! itatuumiza. Kama wao wamemwondoa balozi wao kwenye nchi ya amani sisi tunachelea nini kumtoa wa kwetu kwenye nchi ya Vurugu???
Mkuu hapo tupo pamoja swala la zimbabwe linaweza kusubiri tumalize kwanza ya kwetu yanayotuumiza vichwa. kwa kutoa angalizo tu ni kwamba Serikali yetu ifunge ubalozi wetu kule kama wao na itoe tamko kwa watanzania wanaoishi zimbabwe warudi kwanza nyumbani mpaka hapo hali itakapotulia. KODI wanayosaga wabunge pale Dom kwa siku inatisha wakiongeza tena siku kwa swala la ZIMb mmhh!! itatuumiza. Kama wao wamemwondoa balozi wao kwenye nchi ya amani sisi tunachelea nini kumtoa wa kwetu kwenye nchi ya Vurugu???
And unto the angel of the church of the Laodiceans write; These things saith the Amen, the faithful and true witness, the beginning of the creation of God; I know thy works, that thou art neither cold nor hot: I would thou wert cold or hot. So then because thou art lukewarm, and neither cold nor hot, I will spue thee out of my mouth. Because thou sayest, I am rich, and increased with goods, and have need of nothing; and knowest not that thou art wretched, and miserable, and poor, and blind, and naked: I counsel thee to buy of me gold tried in the fire, that thou mayest be rich; and white raiment, that thou mayest be clothed, and [that] the shame of thy nakedness do not appear; and anoint thine eyes with eyesalve, that thou mayest see. As many as I love, I rebuke and chasten: be zealous therefore, and repent.
Revelation 3:14-19 (KJV)
nadhani Term Ya Uraisi Zimbabwe Ni Miaka 7 Unless Wamebadili Hivi Karibuni
balozi ameenda kwa masuala muhimu ya uchaguzi na si RECALL
Kwa hiyo unataka kusema Mh. Zitto ametudanganya wananchi na Bunge???
JAMBO LA DHARURA
kanuni ya 47 na 48 ya Kanuni za Bunge
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kanuni ya 47 na 48 ya Kanuni za kudumu za Bunge Toleo la mwaka 2007, ninaomba kuwasilisha hoja kuwa Bunge liahirishe shughuli zake ili kujadili jambo la dharura.
Mheshimiwa Spika, jambo hili linahusu Zimbabwe.
Mheshimiwa Spika, Mara baada ya Mawaziri wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika SADC kukutana na kujadili hali tete ya Zimbabwe na mara baada ya kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mheshimiwa Bernard Camillius Membe (Mb) kwamba uchaguzi wa Zimbabwe hautakuwa huru na haki, Serikali ya Zimbabwe imechukua hatua ya kumwondo Balozi wake nchini.
Katika shughuli za Kidiplomasia, hatua ya nchi kumwondoa Balozi wake kufuatia matamko ya nchi mwenyeji ni sawa na kutangaza mgogoro wa Kidiplomasia.
Mheshimiwa Spika, mpaka hapa ninapowasilisha hoja hii, Serikali ya Tanzania bado haijachukua hatua yeyote kuhusu Balozi wetu aliyepo huko Harare. Mtanzania huyu tuliyemtuma kumwakilisha Rais na nchi yetu nchini Zimbabwe aweza kuwa katika hali ya hatari.
Mheshimiwa Spika, Zimbabwe na watu wa Zimbabwe ni marafiki zetu wa siku nyingi. Tanzania imeisaidia sana Zimbabwe katika juhudi zake za ukombozi na chama kilicholeta ukombozi nchini humo na Chama cha TANU na baadae CCM ya Mwalimu Nyerere walikuwa na urafiki wa kindugu. Kwa kweli hali ya sasa ya Zimbabwe haivumiliki na ni aibu kwa Umoja wa Afrika.
Mheshimiwa Spika, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mheshimiwa Wilson Masilingi na Mheshimiwa Anna Abdallah (Mb) wamezungumza humu Bungeni kuhusu hali tete ya Zimbabwe na kuunga mkono kauli ya Serikali yetu.
Mheshimiwa Spika, chama cha MDC chini ya Kiongozi wake ndugu Morgan Tsvangirai wamejitoa katika uchaguzi na hivyo kusababisha hali ya Zimbabwe kuwa tete zaidi. Vitendo anavyofanya Robert Mugabe vya uvunjifu wa makusudi wa haki za binaadamu na kanuni za demokrasia lazima vilaaniwe kwa nguvu zote. Kama Robert Mugabe na chama chake cha ZANU PF hawawezi kuachia madaraka wakishindwa uchaguzi na kwamba wapo tayari kuingia vitani, ni kwanini waliitisha uchaguzi. Viongozi kama akina Mugabe ambao walikuwa na heshima kubwa na Mfano wa kuigwa kwa viongozi vijana wa Afrika, wanapofanya vitendo kama anavyofanya sasa wanatutia aibu na kulichafua bara la Afrika.
Mheshimiwa Spika, natoa hoja sasa kwamba Bunge lijadili kwa ufupi hali ya Zimbabwe na kwamba Balozi wa Tanzania aliyepo Harare arudi nyumbani mara moja ili kuionesha Zimbabwe, Afrika na Dunia kwa ujumla kwamba Tanzania ipo thabiti katika kulinda demokrasia na haki za binaadamu.
Naomba kutoa hoja,
Kabwe Zuberi Zitto (Mb)
Kigoma Kaskazini.
BALOZI MWENYEWE (na sio zitto) ANASEMAJE KUHUSIANA NA KURUDI KWAKE ZIMBABWE....!