Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,162
Zitto Kabwe leo asubuhi amewasilisha hoja akitiliataka Bunge kuacha shughuli nyingine ili kujadili hali ya kisiasa na kidemokrasia inayotokea Zimbabwe kwa maelezo kuwa hiyo ni dharura.
Zitto amejenga hoja yake chini ya mambo yanayotokea nchini humo, an uamuzi wa Zimbabwe kumuondoa balozi wake nchini, siku chache baada ya membe kutoa msimamo wa nchi dhidi ya yanayofanywa na serikali ya Zimbabwe.
Amesema uamuzi wa Zimbabwe kumuondoa balozi wake ni sawa na kutangaza vita ya kidemokrasia na kuna uwezekano hata balozi wa Tanzania huko Zimbabwe akawa hatarini.
Amesema vitendo na Kauli ya Serikali ya Zimbabwe kwamba ZANU PF haiwez\i kuachia madaraka hata ikishindwa uchaguzi inaashiria shari na "viongozi kama akina Mugabe ambao walikuwa na heshima kubwa na mfano wa kuigwa kwa viongozi vijana wa Afrika, wanapofanya vitendo kama hivyo anavyofanya sasa wanatutia aibu na kulichafua bara la Afrika."
Kwa maana hiyo, Zitto alitoa hoja kuwa Bunge lijadili kwa ufupi hali hiyo ya Zimbabwe na kwamba balozi wa Tanzania aliyeko harare arudi nyumbani mara moja ili kuonyesha Zimbabwe, Afrika na Dunia kwa ujumla kwamba Tanzania ipo thabiti katika kulinda demokrasia na haki za binadamu.
Lakini, pamoja na kukiri kuwa hoja hiyo ni nzito, Spika alisema kuwa haitaweza kujadiliwa Bungeni moja kwa moja hivyo ameipeleka kqwenye Kamati ya Mambo ya Nje, ikajadiliwe huko kwanza kabla ya kuchukua hatua zaidi.