Zitto Awabana Mawaziri

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
976
48
Zitto awabana mawaziri

na Salehe Mohamed, Dodoma


MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) Zitto Kabwe, amewalaumu mawaziri na baadhi ya viongozi wa serikali kwamba wamechangia kuyaua mashirika ya umma kwa kuchagua wakurugenzi wasio na uwezo.

Shutuma hizo alizitoa juzi bungeni, alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi kwa mwaka wa fedha wa 2008/2009.

Alisema kamati ya kukagua hesabu za mashirika ya umma, imekumbana na mambo mengi katika mashirika hayo lakini kubwa zaidi ni wakurugenzi wasio na uwezo ambao wamepata vyeo hivyo kwa misingi ya udugu na urafiki.

“Cha kusikitisha zaidi ni uteuzi wa wakurugenzi, unaofanywa na mawaziri bila kuihusisha Ofisi ya Msajili wa Hazina ambayo kimsingi, ndiyo inayopaswa kujulishwa na kuratibu shughuli za mashirika ya umma,” alisema.

Alisema Ofisi ya Msajili wa Hazina, ina mali zenye thamani ya zaidi ya sh trilioni 5, lakini ukiangalia uwezo wake ni mdogo na imekuwa haiangaliwi kwa kiwango kinachotakiwa

“Mawaziri mnaofanya uteuzi wa wakurugenzi wasio na sifa katika mashirika ya umma, ndio mnaoua mashirika hayo, pale hawaendi kusimamia masilahi yenu bali ya umma, sasa kwa nini msichague wakurugenzi wenye uwezo?” alihoji Zitto.

Aidha Zitto, aliitaka serikali kuingia katika Soko la Hisa la Dar es Salaam, kupitia baadhi ya mashirika yake ya umma ikiwamo TSN, Twiga Bancok, Celtel (Zain) na mengineyo, angalau itoe asilimia 25 za hisa zake ili ziweze kununuliwa na Watanzania.

Alisema hakuna maana kama serikali itakuwa ikiendelea kuimba wimbo wa Watanzania kumiliki uchumi wa nchi, kama itaendelea kuwa na hisa nyingi katika mashirika hayo bila kuziingiza katika soko la hisa ili Watanzania wazinunue.

Aidha, mbunge huyo pia amepinga wabunge kuwamo katika bodi za wakurugenzi wa mashirika mbalimbali ya umma, kwa madai kuwa hali hiyo inaweza kusababisha mgongano wa kimaslahi, linapofika suala la kuwawajibisha viongozi na wajumbe wa bodi wa shirika ya umma.

Alisema ni vema wabunge wanaotaka kuwamo katika mashirika ya umma, wakaachana na shughuli za kisiasa ili wayatumikie vema mashirika hayo kuliko ilivyo sasa.

Alisema kamati yake ya Hesabu za Mashirika ya Umma, imeshapeleka waraka kwa Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Fedha na Uchumi na viongozi wengine, ili jambo hilo liweze kupitishwa na kuwazuia wabunge kuwa wajumbe wa bodi hizo.

Aidha, Zitto alisema upinzani nchini unafanya kazi nzuri ya kuwaumbua viongozi na watendaji wanaoshiriki katika vitendo vya ufisadi, licha ya wabunge wa CCM kukerwa na kelele hizo.

Alisema kuibuliwa kwa suala la EPA ni kiashirio tosha cha kazi nzuri inayofanywa na wapinzani, ambao wako mstari wa mbele kuhakikisha watendaji na viongozi wanafuata maadili kulingana na kiapo walichokula wakati wanapewa nafisi hizo.
 
Hao Mwaziri kazi zao wenyewe zimewashinda unadhani wataweza kuchagua wakurugenzi bora maana a fool can not lead a fool!Wizara zao ni shaghala baghala!
 
Corporate governance kwa TZ ni tatizo. Hao wajumbe wa board inatakiwa wachaguliwe kwa kuangalia uwezo wao na pia kuongeza ujuzi kwenye board. Unapochagua mtu wa kwenda kukaa tu kule na kusubiri posho, hapo ndio mwanzo wa matatizo yote.

Hata mimi sioni sababu za wabunge kuwa wajumbe wa boards mbalimbali, wanatoa wapi huu muda? Mara bungeni, mara kamati za bunge, mara safari, je wanakuwa majimboni kwao muda gani?

Kuna haja ya kufanya research na kutambua wabunge wanakaa siku ngapi jimboni kwao kwa mwaka?
 
Bodi members ni kero kwa mashirika ya umma wala hawasaidii kwa lolote watendaji wa mashirika hayo.

Wanasiasa na mawaziri ni kero kwa mashirika ya umma kwasababu wanafanya kama ni sehemu za kuponea pale wanapokuwa na matatizo yao.
 
Back
Top Bottom