Zitto awa makini au apata kigugumizi?

Lukwangule

Senior Member
May 25, 2009
157
2
Leo ilikuwa siku ya mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutangaza wapi anawania kati ya majimbo matano aliyokuwa ameyataja mwanzo. Majimbo hayo ni Kahama, Geita, Kinondoni, Kigoma Mjini na Kigoma Kaskazini.

Hata hivyo katika mkutano wa Geita ambao alisema kwamba atatamka amewaomba watanzania kumpatia muda wa wiki mbili ili kukamilisha utafiti wake.

Zitto alisema kutokana na utafiti wa awali waliofanya wataalamu wake aliowapa kazi ya kuangalia jimbo analokubalika ameyaondoa majimbo mawili kati ya matano aliyoyataka na kubakiza matatu.

Majimbo aliyoyaondoa ni ya kinondoni na kahama na kubakiza ya Geita, Kigoma mjini na Kigoma Kaskazkini.
 
Tatizo anataka kwenda bungeni au anataka kusaidia watu?

Nadhani tatizo sio kwenda bungeni kwa kuwa nafasi ya kushinda ni kubwa. Kwa mtizamo wangu anachojaribu ni kujenga mtandao mpana zaidi ikiwa ni kuwawezesha wengine kupitia kwenye nyayo zake kuufika bungeni ikiwa ni kuongeza uwakilishi wa upinzani bungeni. Ni mtizamo wangu tu
 
umegonga penyewe mkuu
 
waswahili wanasema kuchamba kwingi............ dogo atulize ball
 
waswahili wanasema kuchamba kwingi............ dogo atulize ball

Mkutano wake ulikuwa mkubwa na watu wengi japo Polisi walimgomea Kibali cha kufanyia Geita mjini (katikati ya mji), mvua iliyokuwa imenyesha karibu siku nzima ya jana, bado alikuwa na watu wengi, ......walikuwa wakimlilia agombee Geita. Tizama jinsi ambavyo alikuwa akigombewa na umati huo katika picha hii.

zittokabwe.jpg

Nadhani tatizo sio kwenda bungeni kwa kuwa nafasi ya kushinda ni kubwa. Kwa mtizamo wangu anachojaribu ni kujenga mtandao mpana zaidi ikiwa ni kuwawezesha wengine kupitia kwenye nyayo zake kuufika bungeni ikiwa ni kuongeza uwakilishi wa upinzani bungeni. Ni mtizamo wangu tu

Atatangaza Geita huyu ninavyomuona amegundua inamlipa

47648527.jpg
 
Mbona huyu dogo mwenzangu ana kigeugeu? Alishawahi kusema kuwa hatagombea mwaka huu anaenda kusoma Ujerumani, leo anafanya mchanganuo wa jimbo lipi agombee. Naona hii haiko sawa.
 
Lazima anajipanga vizuri, wakati ukifika atangaza kwa hiyari yake..mchango wake bado unaitajika bungeni
 
Back
Top Bottom