Zitto Atufagilia CCM kwa utekelezaji wa ilani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto Atufagilia CCM kwa utekelezaji wa ilani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MkamaP, Apr 21, 2010.

 1. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Zitto Kabwe aipongeza CCM Send to a friend
  Wednesday, 21 April 2010 19:05

  Salim Said

  NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe ameifagilia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kufanikiwa kufanya uwekezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo kuliko nchi yoyote kusini mwa bara la Afrika.

  Zitto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (Nac), aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana alipokuwa akiwasilisha ripoti ya kamati yake kwa 2008/09.

  Akiwasilisha ripoti hiyo aliyoisoma kwa muda wa nusu saa, Zitto alianza kuusifia uwekezaji wa miaka mitatu wa mradi mkubwa uliomo ndani ya ilani ya CCM wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

  “Mheshimiwa Spika uwekezaji huu wa miaka mitatu wa Chuo Kikuu cha Dodoma unagharimu jumla ya Sh800 bilioni ni mkubwa sana kwa nchi yetu lazima tupongeze,” alisema Zitto.

  “Uwekezaji huu ni mkubwa kuliko uwekezaji wowote uliofanywa katika nchi zilipo kusini mwa bara la Afrika na ni zaidi ya uwekezaji wa miaka 10 kutoka nje,” aliendelea kusifu.

  my note:
  Lakini pamoja na kufagilia
  Sijaona jinsi ajira milioni kadhaa kwa vijana zilivyotekelezeka. Na pia sijaona maisha bora kwa kila mtanzania.
   
 2. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mimi nahofu tumekwisha poteza mpiganaji, mwanamageuzi. Hivi hizo fedha walizowekeza wamezitoa wapi? Huenda ndiyo Kagoda yenyewe! Sasa Zitto anasifu nini? Kutawalla nchi miaka 45 na kuwekeza hivyo vijisenti kunahitaji sifa kweli? Mimi nafikiri kuna kirusi fulani cha ubongo nchini Tanzania bado hatujakigundua na jina bado kupewa. Nawaomba radhi wana JF hili haliniingii kichwani.
   
 3. n

  nndondo JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  He is a sell out, a cheap politicians hajua hata kufanya analysis sijui hiyo shule anayosoma kwa sasa anasoma nini. hajua kwamba analysis hazifanywi kwenye process indicators you need impact indicators, hajui kwamba huo anaouita uwekezaji hau qualify kuitwa hivyo kwa milestone yoyote, hajasoma hata hizo strategic intention za sera ya uwekezaji akaangalia na matokeo yake na kuyakuta sio tu ni zero bali negative. Hajasikiliza hata report ya baraza la uwezeshaji la April 7 2010. Hapo ndipo unapoona kwamba kweli Zitto bila Chadema ni mtupu alibebwa akapata umaarufu kwa migongo ya wenzake. Anatafuta cheo kwa JK anasahau kwamba hata huo uenyekiti wa kamati critical kama hizo na scholarship za ujerumani alizipata akiwa kavaa ngozi ya kondoo kumbe ndani ni wolf. Huyo ndio zitto Kabwe swala la vijana wakitanzania kusukumwa kwenye umaskini uliokithiri sio hoja kwake anymore, kwa sasa anataka position 'too cheap'.

   
 4. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,090
  Trophy Points: 280
  tatizo la siasa za uongo na unafiki zitazidi kuturudisha nyuma. Mpinzani wako akifanya jambo jema unampongeza huo ndo ukweli. Wewe MkamaP na chama chako mnatakiwa pia kupongeza mazuri yanayofanywa na wapinzani. Nampenda kwa kuwa mkweli katika hili. Hii haimainishi kwamba CCM wamefanya vizuri hata wawe majasiri kwetu wananchi. Madudu ni mengi kuliko mafanikio, na hili ndo tatizo.

  Kikubwa ubovu unaanzia kwa Mhe. Rais. You can imagine, ndani ya mwezi mmoja yanatokea mambo mawili makubwa yanayoonyesha kuwa hawanazo:
  1. Rais amesaini sheria kwa mbwembwe nyingi, siku tu baadae inajulikana kuwa inamakosa na inarudishwa bungeni huku wakiomba radhi.
  2. Rais kasaini hati ya dharura ya kujadiliwa kwa mswada wa sheria ya madini. Kabla hata ya kujadiliwa bungeni wanaiondoa kwasababu inamakosa kibao.

  Can you say this President na Serikali yake are siyo wasanii waliopewa nchi kimakosa, makosa ya wananchi kutowajua vizuri kabla ya kuvote.
   
 5. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mie kama mwana CCM ulivyosema
  Sijaona Ilani iliyotekelezwa na chama changu, nafikiri huo ndo ukweli. Hasa ukizingatia ajira milioni kadhaa , vijana kuwezeshwa na masilahi bora kwa kila mtanzania hasa ukitilia maanani maisha yamekuwa je bora kama wafanyakazi tarehe 5 wanajiandaa kugoma kudai masilahi na je wakulima si ndo basi kabisa.

  Mimi michango yangu huwa sina itikadi na mtu ,huwa najadili kulingana na topic
   
 6. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Sifikiri kama anaongea hivyo akiwa na maana ya kumendea kitu kutoka serikalini, yawezekana na mtazamo wake
   
 7. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160

  Zitto anaweza kutoa reference kusimamia kile alichokisema hapo juu. Nchi zilizoko kusini mwa bara la Afrika ni pamoja

  na South Africa na Angola...........
   
 8. m

  miner Member

  #8
  Apr 21, 2010
  Joined: Dec 14, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sina uhakika kama ujenzi wa Chuo Kikuu Dodoma kama upo katika ilani ya CCM na umetamkwa bayana nakumbumka ilani ya Chadema ndio imetamka kuufanya mji wa dodoma kama kitovu cha elimu badala ya kuendeleza dhana ya makao makuu kutotekelezeka mwenye ilani karibu atusaidie
   
 9. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Huku kusini mwa jangwa la sahara kuna nchi zinafanya vizuri sana kama Gaboni,Namibia.
  Nafikiri japo sina uhakika wanasiasa badala ya kujenga hoja wamekuwa na mtindo wa kufanya reference kuhafanya hoja, mfano utasikia Tz imefanya vizuri sana ktk EAF.
  Na kama wamefeli kujenga hoja utasikia hapo inabidi wananchi wa vijijini wakaelimishwe. Kuna kasumba fulani ambayo imeanza kujengeka nafikiri sio nzuri sana maana hawatupi takwimu zinazozitahili.
   
 10. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #10
  Apr 21, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Wait!!!!, wakati zito anatoa hiyo ripoti bungeni alisema neno ILANI YA CCM??? AU ALISIFIA TU UWEKEZAJI??, we need to be careful here! !. Hilo moja

  Pili kama amesema CCM Imetekeleza ilani ya uchaguzi na reference yake imekuwa ni UDOM tu tatizo nini nini? NIKISEMA KUWA CCM KWA KUJENGA UDOM IMETEKELEZA ILANI YAO YA UCHAGUZI NDIYO NI SAWA NA NIMESEMA KUWA CCM WAMETEKELEZA ILANI ZOTE ZA UCHAGUZI?????????????????????? great thinker vipi?
   
 11. m

  matejoo Member

  #11
  Apr 21, 2010
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna watu wanapenda kusikia shari tu, hawapendi kuona ushirikiano walau katika mambo tunayo yakubali wote. I see ho harm on what kabwe has said and ofcourse I am quit sure that the press man modified it to "sound" like he was speaking for CCM. This does not need a degree in quantum physics. I must say however that Zitto Kabwe needs to be careful on the use of hyperboles. Kutumia nchi nyingine kama kigezo au kilinganishi is wrong in its very root. Hatushindani. Matamanio yao ni tofauti etc. It is a sign of ignorance for a politician to start taking an imaginary journey to all countries he has been to (physically and mentally) only in the attempt to make his point wakati walengwa ni watu wa Meatu, Katerero na Ilembula!
   
 12. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mimi KARATA YANGU nilishaiondoa kwa huyu jamaa muda mwingi sana, nilishaona kama anatuchezea akili tangu pale alipokuwa na kurupushani kwenye chama akitaka kuondoka na kuachana na siasa. simwamini asilimia miamoja, na sitaki hata kusikia anavyoongea, kwasababu simwamini na sipendi, yaani sipendi. tatizo la watz, mtu akishapata kidogo tu, huwa anaona amefika, na anasahau hata ile imani watu waliyokuwa wameweka juu yake, anawatosa wafuasi wake yaani kwa kifupi. hii si vizuri.
   
 13. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #13
  Apr 22, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Well said brother, we should have our own standard of achievement, comparion with other countries is always wrong one! because we have different priorities, visions, etc.
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  Apr 22, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280

  Nyie mmejaa mjungu na hatred, afadhali Nndondo , Mwana wa Mungu pamoja na kuwa alarted kuwa mwangalifu na lugha iliyotumika na nini hasa kilichozungumzwa bado umekazania, kuwa 'anakuchezea akili' tumeona in past few years baadhi ya watu kumchukia sana Zito humu ndani ya JF simply kwa sababu amewaza tofauti! na wewe pamoja na jina zuri umetumbukia kwenye kundi la haters msio na sababu ya kumchukia! still Mwana wa Mungu?
   
 15. Kiwalani

  Kiwalani Senior Member

  #15
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Natabiri kwamba katika Baraza la Mawaziri baada ya uchaguzi kutakuwemo na at least mmoja toka upinzani ..... ninampa nafasi kubwa Zitto Kabwe. JK ataiga Marekani .... waziri wa ulinzi ni kutoka Republican party!
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  Apr 22, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,593
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Kwa katiba ipi? tumeshakuwa na serikali ya Mseto? Katika wana CCM milioni 4 hakuna atakayefaa ila wampe mpinzani?

  Hao akina Zito inabidi watengeneze mazingira (wapigane)ya kuunda serikali ya Mseto na sio sandakalawe! nimefurahi unaona umuhimu wa serikali ya Mseto , yenye sura ya utaifa zaidi na sio kuwa colonised na CCM! However, wapinzani wachache sana au hamna wanaowaza swala la serikali ya Mseto! upinzani utakuwa upinzani tu baada ya Mseto( mabadiliko ya katiba) hali ya sasa ilivyo hamna upinzani Tanzania na ndio maana simply Mr. Kiwalani umeshaipa CCM urais wa mwaka 2010 na tayari uko hatua ya kuunda baraza la mawaziri! wakati wengine wanawaza uchaguzi. I van not blame you that is reality!
   
 17. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Zitto wala hajakosea, Kusini mwa jangwa la Sahara hakuna nchi kwa miaka mitatu iliyowekeza kwenye Elimu ya JUU kama Tanzania ilivyofanya. Kwa chuo kikuu cha UDOM pekee yake kuna nchi gani ndani ya miaka hii mitatu imejenga chuo kikubwa kama UDOM si mseme??? Waswana wamewekeza kwenye chuo cha Limkokwing University ambacho kinajengwa kwa nguvu ya Malasia lakini bado hakijaifikia UDOM. Hajadanganya, wanao bisha waseme ni nchi gani na imejenga chuo kipi kikubwa kuliko UDOM?
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  System yetu ya sasa inatengeneza, inalinda na ku-perpuate watu waongo, wadanganyifu na pretenders and all other egoistic personalities. The guy is clown period. The highlight of his pathetic political lil 'career' ni pale alipokimbia challenge ndogo tu hapa JF. Huhitaji kujiumauma maneno.

  Maendeleo ya nchi yetu yanatakiwa yapimwe na POTENTIAL YETU sio against mediocre performances kutoka kwa nchi nyingine zinazo-underperform.
   
 19. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160

  Wewe unachanganya mambo, Zitto amezungumzia uwekezaji kwa ujumla hakuwa specific katika masuala ya elimu. Pili, hoja yake iko flawed kwani inawezekana wenzetu kwa sasa vyuo sio priority kwani walishajenga miaka ya nyuma.
   
 20. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Hujasoma Post ya kwanza, Nenda kasome post #1 Utaona jinsi alivyongelea mfano wake kwa kutumia UDOM. Kwa hiyo kama hawajaweka Priority kwa mipango yao ya maendeleo miaka hii ya karibuni na sisi tumeweka na tumewekeza kuliko wao tusifanye uringanisho???

  Mkuu Kama Zitto angekuwa amefanya general comparison ya kuwekeza kwenye elimu kwa miaka yote katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara hapo ningekubaliana na wewe, lakini kaweka kipindi maalumu kasema for the past 3 years. Sasa hata ukisema kuwa uwekezaji wa jumla njoo na Data, Nchi gani kusini mwa sahara ilifungua uwekezaji mkubwa katika kipindi cha miaka 3 ya hivi karibuni na kwa maeneo gani? Embu tuambie na Tanzania imeshika nafasi ipi kwenye eno lipi?
   
Loading...