mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,307
- 6,514
Mheshimiwa Spika, adhma ya nchi yetu kuwa ya Viwanda ni adhma yetu sote. Jambo hili ni jambo la Maendeleo na halina ushabiki wa kivyama. Tumepitisha Mpango wa Maendeleo katika Bunge hili na kwa hiyo ni Mpango wa Nchi sio mpango wa vyama tena. Hivyo sote kwa pamoja tunafanya kazi ya kuhakikisha tunafikia malengo. Sisi tulio kwenye upinzani jicho letu pamoja na kushauri na kupendekeza ni kukosoa pale ambapo walio kwenye Serikali wanakosea. Kukosoa ni tendo la kizalendo na walio Serikalini wawe tayari kukubali kukosolewa ili kuboresha zaidi. Kwa maoni yangu, kama tusipofanya marekebisho ya kimkakati mapinduzi ya Viwanda itakuwa ni nyimbo na ngonjera za kisiasa. Watakaoumia ni Wananchi ambao hawatapata ajira na Serikali yenyewe itakosa kodi kuweza kutoa huduma kwa wananchi. Kama nilivyosema hapo awali Serikali inahitaji kufanya uratibu ili kufikia malengo. Sekta ya Viwanda au Maendeleo ya Viwanda yanapaswa kufungamanishwa na sekta nyengine za uchumi kwa sababu kuna kutegemeana. Kwa Tanzania unahitaji Sekta ya Kilimo inayokua kwa kasi ili kuzalisha malighafi kwenye viwanda. Sekta nyingine kama Elimu, Afya, Nishati, Mazingira nk zinahusiana na Viwanda pia. Kwa leo tutazame Sekta Kilimo na Viwanda kwa muktadha wa Hotuba ya Waziri wa Viwanda na kulinganisha na Hotuba ya Waziri wa Kilimo.
Mheshimiwa Spika, Sekta ya Viwanda na Sekta ya Kilimo kwa pamoja zinachangia nusu ya Pato la Taifa ( GDP) na nusu nyingine ni sekta ya Huduma. Nadharia za Uchumi zinatuambia kuwa Tija ikiongezeka kwenye ya Kilimo inawezesha sekta ya Viwanda kukua na kisha sekta ya Huduma. Hapa Tanzania nan chi nyengine nyingi za Afrika, sekta ya huduma iliruka hatua hizi na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa sana kwenye Pato la Taifa. Ndio maana tuna kitandawili nchini kwetu kuwa Uchumi unakua lakini umasikini haupungui; ni kwa sababu sekta ya huduma haijiri watu wengi kama sekta ya Kilimo na hivyo uchumi unaokuzwa na sekta ya huduma ni nadra kuondoa umasikini. Tanzania bado inapambana na umasikini. Juhudi zote tunazofanya lengo lake ni kuondoa umasikini kwa watu wetu. Sekta za kuondoa umasikini ni Kilimo na Viwanda hivyo lazima mikakati ya Serikali iendane na kufungamanisha haya. Ndio Maana Nchi nyengine Wizara ya Kilimo hujumuisha uongezaji thamani ( Ministry of Agriculture and Agro-processing ). Hatuhitaji kufanya hivyo, tunachohitaji ni kufungamanisha. Hata hivyo Serikali imeshindwa kufanya hivyo katika mwaka wake wa kwanza tu wa Bajeti. Nitaeleza kwa kutumia changamoto tuliyonayo kuhusu Sukari, Mafuta ya Kula na Nguo.
Mheshimiwa Spika, Malengo ya Serikali kwenye Viwanda yapo uk.140 ibara ya 191 ya Hotuba ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Serikali imepanga kutekeleza mambo 9 na katika mambo yote hayo hakuna hata moja linalohusiana na Viwanda vya kuzalisha bidhaa zinazohudumiwa na wananchi wengi zaidi kama Sukari na Mafuta ya kula. Bidhaa hizi ni bidhaa zinazoleta maneno ya kisiasa ndani ya nje ya Bunge. Nadhani baada ya madawa ya kulevya, bidhaa zenye mizengwe mingi zaidi katika duru za kisiasa ni Sukari na Mafuta ya kula. Sukari na Mafuta ya kula imeangusha Mawaziri kadhaa hapa nchini katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. Hata hivyo Wizara ya Viwanda na Biashara haina mkakati kabisa kushughulika na Bidhaa hizi licha ya uwezo wake wa kutenegenza ajira na kuokoa fedha za kigeni kuziagiza. Wizara imezungumza kuhusu viwanda vya nguo lakini haijafafanua changamoto kubwa zinazoikabili sekta ya nguo nchini na hasusan biashara haramu ya magendo ya Nguo inayoathiri sana ukuaji wa sekta ya nguo nchini.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, ukitazama hotuba ya Waziri wa Kilimo ambayo Bunge lako tukufu limeshapitisha bajeti yake kuna ‘mikakati’ ya kulima Miwa kwa ajili ya Sukari. Ukurasa wa 44 ibara ya 107 ya Hotuba ya Wizara ya Kilimo na ukurasa wa 25 ibara za 63 na 64 zinaeleza ‘mikakati’ ya kukabiliana na uhaba wa Sukari nchini. Kiambatanisho namba 6 cha Hotuba hiyo kimeeleza kwa kina changamoto nzima ya Sukari na miradi ianyopaswa kutekelezwa ili kumaliza kabisa suala la uhaba wa Sukari nchini. Nimejumlisha miradi ile kutoka kona mbalimbali za nchi na nimekuta ni takribani Hekta 300,000 za kulima Miwa. Kwa Hesabu ya chini ya wastani wa kuzalisha Sukari kwa kila Hekta, miradi hii ikitekelezwa Tanzania itaweza kuzalisha Tani 1.5 milioni za Sukari. Ukiondoa Sukari tunayotumia nchini, ziada itakayouzwa nje inaweza kuliingizia Taifa Fedha za Kigeni USD 500 milioni, sawa na 30% ya malengo ya Mpango wa Maendeleo kwa sekta ya Viwanda katika mapato ya Fedha za kigeni ya USD 3bn. Hapo sijaeleza kiwango cha Ajira kitakachopatikana, ukuaji wa biashara kwenye sekta nyengine na Umeme utakaozalishwa ( Multiplier effect ).
Mheshimiwa Spika, swali la kujiuliza, chukulia Wizara ya Kilimo inalima hiyo miwa hekta 300,000 halafu Wizara ya Viwanda haina mpango wa hivyo viwanda, hii miwa itakwenda wapi? Sio kwamba inapaswa kufungaminisha Kilimo cha Miwa na Viwanda vya Sukari? Ni kwa nini Wizara 2 zilizo chini ya Serikali moja zinashindwa kusomana? Baraza la Mawaziri linajadili nini? Ndio maana Rais anajikuta akitoa matamshi ya Mawaziri barabarani. Suala la Rais kutoa matamko kuhusu Sukari sio sawa, hii ni Kazi ya Mawaziri maana mnam expose Rais. Rais sio mtu wa kuhangaika na masuala ya kunywa Chai na Uji.
Mheshimiwa Spika, nashauri Bunge lako tukufu leo lisipitishe Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ili Wizara hii ikakae na Wizara ya Kilimo wawianishe mipango hii na kisha walete hapa Bungeni ndio tupitishe.
Mheshimiwa Spika, suala la Mafuta ya Kula halina tofauti na suala la Sukari. Ukipanda gari ukapita njia ya Singida unaona wananchi wamepanga madumu ya mafuta ya Alizeti wanauza. Nguvu kazi hii ya Wananchi inapotea kwa sababu Serikali imetoa unafuu mkubwa wa kodi kwa wanaoagiza mafuta ya kula kutoka nje ya Nchi. Leo kodi kwenye mafuta ya kula kutoka nje ni 18% tu. Tukiendelea hivi tutaendelea kuwaona wananchi wetu wanapigwa na jua kuuza mafuta ya Alizeti. Tunaposema mapinduzi ya Viwanda tunataka kumsaidia nani kama sio huyu Mwananchi anayeshinda juani? Kama tunataka kubadilisha hali ya Wananchi ni lazima tuwawekee mazingira mazuri. Ni Aibu kubwa nchi hii kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi. Tunatumia USD 340 milioni kila mwaka kuagiza mafuta ya kula kutoka nje. Leo hii bei ya lita ya mafuta ya Alizeti ni kubwa kuliko bei ya lita ya petroli kwenye soko la dunia. Lakini wazalishaji wetu, wananchi wetu masikini tunawatazama tu tukipita na mashangingi yetu barabarani. Hali hii lazima ibadilike. Serikali ndio yenye wajibu wa kubadili hali hii kwa kuweka kodi kubwa zaidi dhidi ya Mafuta ya kula kutoka nje na kuwekeza kwenye viwanda vya kukamua Mafuta kwa kutumia Alizeti na Mawese.
Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Kigoma kuna Mradi tunaotaka kuanza wa kupanda Michikichi ili kuzalisha Mafuta ya Mawese. Tuna mpango wa kila familia 1 kupanda hekta 1 ya michikichi kwa lengo la kufikia familia 100,000. Uzalishaji huu wa Mawese unaweza kuondoa kabisa suala la Tanzania kuagiza mawese kutoka nje maana tutaweza kuzalisha Tani 200,000 za Crude Palm Oil (CPO) kwa mwaka, kuzalisha ajira nyingi, kupandisha hali ya maisha ya wananchi wakulima na kukuza biashara nyengine. Tunahitaji watu watakaowekeza kwenye Viwanda vya kuzalisha mawese. Wizara ya Viwanda ishirikiane na Uongozi wa Mkoa wa Kigoma kuhakikisha tunazalisha mafuta ya Kula ya kutosha ili kuondokana na uagizaji huu. Mawese na Alizeti ndio suluhisho la kudumu la suala la Mafuta ya kula. Bunge liitake Serikali ikae upya kuandaa Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ili kuifungamanisha na Bajeti ya Wizara ya Kilimo.
Mheshimiwa Spika, Suala la Mwisho ni sekta ya Nguo. Nchi nyingi duniani ambazo zimefanikiwa kuondokana na umasikini zimetumia sekta ya nguo ( textile industry). Mnyororo wa thamani wa Sekta ya Nguo ni mrefu kuanzia kwa Mkulima mpaka kwenye nguo tunazovaa. Hii inapaswa kuwa sekta ongozi kwenye suala zima la uchumi wa viwanda. Hata hivyo tuna tatizo la Pamba.
Mheshimiwa Spika, uzalishaji wa Pamba umeporomoka kwa asilimia 47. Tutapata wapi Pamba ya kulisha viwanda vya nguo? Wizara ya Kilimo na Wizaara ya Viwanda lazima zikae pamoja ili kuhakikisha kuwa tunafufua zao la Pamba. Vinginevyo nchi hii itaishia kuagiza pamba kutoka nje au tutajikuta tunaunganisha nguo za kutoka China tu.
Mheshimiwa Spika, Viwanda vya Nguo nchini vinapata shida kubwa sana kutokana na magendo ya nguo. Kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi kwenye bidhaa za nguo zinazoingizwa hapa nchini na hivyo kuua viwanda vya ndani. Viwanda vinapata shida kubwa ya matumizi ya Umeme maana umeme hauna uhakika na ni bei kubwa. Matokeo yake viwanda vingi vinafungwa na watu wetu kukosa ajira. Serikali lazima ifanye kazi ya ziada ya kuzuia magendo ya nguo vinginevyo viwanda vilivyopo vitakufa na hakuna atakayekubali kujenga kiwanda hapa nchini kwani atajua kuwa Serikali haifanyi ziada kuhakikisha tunalinda viwanda.
Mheshimiwa Spika, hakuna nchi duniani isiyolinda viwanda vyake. Leo Taifa kubwa kama Uingereza linahangaika na kiwanda cha Chuma na kutaka hata kuingiza mtaji wake ili kulinda ajira za Wanananchi wake. Tujifunze kwa wenzetu. Kama tunataka kupata ajira kwa watu wetu ni lazima kulinda viwanda vyetu. Viwanda vya nguo nchini vipo kwenye tishio kubwa sana kutokana na magendo ya nguo. Serikali ichukue hatua stahiki. Nguo zitatuoa kuanzia kwa mkulima mpaka kwa wenye viwanda.
Mheshimiwa Spika, Naomba kutoa hoja kwamba Tuahirishe mjadala wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ili kuiruhusu Serikali kuwianisha mipango ya Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda. Wakiwa tayari ndio Bunge lije kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo.
Zitto Zubeir Ruyagwa Kabwe
Mbunge Kigoma Mjini (ACT Wazalendo)
Mei 9, 2016