Zitto ataka wanaoikosoa ACT-Wazalendo waanzishe chama chao

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,477
51,043
Nimeshangazwa na majibu ya mkuu wa chama cha ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe aliyoyatoa kwenye mtandao wa twitter.

Zitto alikuwa akimjibu mwananchi mmoja aliyekuwa akionyesha frustrations zake juu ya uamuzi wa chama cha ACT kujiunga na Serikali ya CCM huko Zanzibar katika kile kinachoitwa serikali ya umoja wa kitaifa. Mwananchi huyo anaonyesha kuwa kuingia kwa ACT katika hiyo serikali hakuwezi kusaidia wananchi kupata uhuru mpana waliokuwa wakitamani kuwa nao.

Katika hali isiyo ya kawaida, isiyo ya uungwana na isiyo ya kiuongozi mkuu wa chama cha ACT ndugu Zitto badala ya kutumia fursa hiyo kumuelewesha au atleast akae kimya wananchi watumie haki yao ya kutoa maoni, yeye anamjibu kwa ufedhuli na jeuri kuwa "Kama unaona tumekosea basi anzisha chama chako".

Kwa kweli sikutegemea kiongozi haswa wa upinzani kutoa majibu ya nyodo kama haya kwa wananchi wanapouliza maswali ya msingi juu ya mienendo ya kisiasa nchini.

Labda Zitto afahamu tu kuwa sababu mojawapo ya leo ACT-Wazalendo kuwa hapa ni haohao wananchi ambao leo anawajibu kwa nyodo kuwa "anzisheni chama chenu"

Lakini pia Zitto akumbuke kuwa kuna watu wamekifia hicho chama, Wakati akijibu kwa majibu ya "Anzisheni chama chenu" Je amelifikiria hili kuwa kuna watu wame-pay ultimate price kwa hicho chama au kwa course yake waliyoinadi kwao na kwa hiyo ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wana haki ya kuhoji ukinyongakinyonga wa misimamo iliyowafanya hapo awali wawe tayari kukipigania hicho chama?

Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, Viongozi wa ACT sasa hivi wameacha kujibu maswali magumu ya wananchi juu ya hatua yao ya kuingia kwenye SUK wakati waliitangazia dunia na nchi kiujumla kuwa uchaguzi uliopita ulikuwa haramu, Zitto mwenyewe akaweka saini tamko la pamoja la Upinzani kuwa hawautambui uchaguzi ule pamoja na natunda yake, Sasa leo wananchi wakihoji wanaambiwa jamani eeh kama hamtaki tulichokifanya basi nendeni CCM, au NCCR yaani ni majibu ya kifedhuli uliopitiliza!. Sasa wameacha kutoa majibu kwa wananchi, wameanza kublackmail wanachama wa ACT na kutoa kauli za nyodo kwa wananchi, kuwa "ACT ina wenyewe na nyie kaanzisheni chama chenu"

Sasa leo tunaona kwa macho yetu, watu tuliodhani ni wakomavu wa kisiasa, tuliodhani kuwa mashambulizi yao kwa CCM basi wao labda wana ngozi ngumu na kwamba labda wao wakipewa nchi basi watakuwa humble, watakuwa na humility, watajibu hoja kwa hoja kumbe hawa jamaa ni arrogant(wenye viburi), intolerant(wasio wavumilivu) na wanajiona wao ni wamiliki wa taasisi kwa kuwa walizianzisha na si wahudumu tu wa taasisi ambazo wao ni wanachama.

Hawa wapinzani hawana blank cheque ya kutuletea jeuri sisi wananchi, Kwa miaka mingi tumekuwa tukiishabumbulia CCM, lakini na wenyewe hawana impunity, tutawaekeza ukweli maana hivyo vyama kwa namba moja au nyingine vinanufaika kwa jasho la wananchi iwe kwa ruzuku au wanasiasa wao kulipwa kwa kodi za wananchi n.k

Zitto acha jeuri kwa wananchi, Jibu hoja na frustrations zao kwa hekima, utulivu, nidhamu na utu. Bila wananchi usingekuwa hapa kuwa na humility.

Hebu kwanza tumsikilize Zitto wa baada ya uchaguzi kisha tusome kuhusu Zitto wa sasa na tweet zake za nyodo kwa wananchi:



Kisha tazama majibu yake ya sasa mwezi mmoja na nusu tu baada ya uchaguzi:
Img-1607829694250.jpg


Na mahali pengine anamjibu mwananchi hivi:

Img-1607847798316.jpg


Pia ameanza kublock watu wanaomcriticize mitandaoni:

Img-1607878745388.jpg
 
Ukweli siku zote unauma sana, kajitahidi kuvumilia siku zote kwa kutoa sababu za uongo kujiunga kwao SUK sasa uzalendo unamshinda, nafsi yake imeanza kulegea kwa ile mistake waliyoifanya.

Japo wanapenda kujidanganya ni upepo tu utapita, lakini nina hakika hilo swali litaendelea kuelekezwa kwa Zitto miaka kadhaa ijayo, na kila akiulizwa lazima akose hamu ya kula that day.
 
They will never get peace kwa kusaliti big course

Yaani hawa jamaa wameiondolea serikali ya CCM pressure kubwa ya ndani ya nchi na hata ya nje ambayo ingewaminya wafanye reforms fulanifulani za msingi.

Yaani ACT wamewazawadia CCM zawadi ya uaminifu kwa mchakato haramu na feki wa uchaguzi na kwa kufanya hivyo wameihakikishia CCM kuwa hakuna consequences zozote watakazozipata hata wakirudia michezo yao hiyo kwenye chaguzi zijazo!. Kwa kweli hakuna usaliti mbaya kama huu kwa future ya demokrasia ya nchi hii!.

Yaani kacheo kisicho na kichwa wala miguu cha Maalim na pengine "behind the scene deals ikiwemo hongo" vimesababisha hawa watu wasaliti movement nzima ya kuiminya CCM ifanye reforms za maana kwenye tume ya uchaguzi

Inasikitisha sana.
 
Heshima kwako mkuu. Tatizo la maandishi haliwezi kuonyesha umyenyekevu au nyodo katika jibu la Zitto.

Nikuombe kurejea hapa:


Alichoonyesha Zitto ni maana pana zaidi ya demokrasia.

Ni muhimu tukakubali kutokubaliana. Tumpe muda Maalim.
 
Wanaoumia na SUK ni CHADEMA, cha kushangaza CHADEMA waliamua kununa huku hawana leverage yoyote dhidi ya serikali, walikuwa wanategemea leverage ya ACT Zanzibar. CDM waendelee kununa tu hadi 2030 hakuna kitakachopungua wala kuongezeka.
Haya ni masuala ya faida kwa wananchi, ni ujinga kuleta divide and rule.
 
Wanaoumia na SUK ni CDM, cha kushangaza CDM waliamua kununa huku hawana leverage yoyote dhidi ya serikali, walikuwa wanategemea leverage ya ACT Zanzibar. CDM waendelee kununa tu hadi 2030 hakuna kitakachopungua wala kuongezeka.

Sidhani kama kuna ukweli kwenye hili.


Pia kumbuka Maalim na ACT ni watu wawili tofauti. Maalim ni mpambanaji na hapa alipo kudhani kesha choka ni kujidanganya!
 
Heshima kwako mkuu. Tatizo la maandishi haliwezi kuonyesha umyenyekevu au nyodo katika jibu la Zitto.

Nikuombe kurejea hapa:


Alichoonyesha Zitto ni maana pana zaidi ya demokrasia.

Ni muhimu tukakubali kutokubaliana. Tumpe muda Maalim.
Kwa hiyo Kila asiyekubaliana na ACT katika hili suala akaanzishe chama chake, na kesho ambaye hatokubaliana na ACT katika mtizamo meingine akaanzishe chama chake.

Kiufupi hilo jibu la Zitto ni jibu tu la kifedhuli, kuwa sisi tumeshaamua usituambie lolote!. Kwa maoni yangu hii siyo kauli ya kiuongozi!
 
Kwa hiyo Kila asiyekubaliana na ACT katika hili suala akaanzishe chama chake, na kesho ambaye hatokubaliana na ACT katika mtizamo meingine akaanzishe chama chake.

Kiufupi hilo jibu la Zitto ni jibu tu la kifedhuli, kuwa sisi tumeshaamua usituambie lolote!. Kwa maoni yangu hii siyo kauli ya kiuongozi!

Mkuu jaribu kusoma tena hapo ukiwa na mawazo chanya:

IMG_20201213_064211_588.jpg


Tukubali kutokubaliana. Ila Seif Zanzibar kaipigania na huenda akawa anaipigania bado kuliko sisi sote.

Ikumbukwe Seif kajielekeza zaidi kuipigania Zanzibar. Mcheza kwao hutunzwa. Tumpe muda.

Kukubaliana kutokubaliana ndiyo ukomavu wa kisiasa. Kumbuka mifarakano ndani ya vyama na baina ya vyama inashabikiwa sana na wale nzi wa kijani.

Rejea pia maoni yao katika uzi huu.
 
Tabia za wanasiasa wa hii nchi bado hujazifahamu tu?

... Anyway wenye chama chao (ACT) walishaamua kujiunga na SUK hivyo heshimuni maamuzi yao.
 
Wanaoumia na SUK ni CDM, cha kushangaza CDM waliamua kununa huku hawana leverage yoyote dhidi ya serikali, walikuwa wanategemea leverage ya ACT Zanzibar. CDM waendelee kununa tu hadi 2030 hakuna kitakachopungua wala kuongezeka.
Hivi unajua sakata la covid 19 wanaoongozwa na Mdee linavyoitesa CCM?
 
Kilichowazuia kutoka barabarani ni nini wakati mlitakiwa kuidai hiyo haki na hamkutoka?
Zitto kachanganya na za kwake baada ya kuona mmemtelekeza siku ya kuandamana.
Sasa wenye hasira na hiyo SUK anzisheni chama nanyi mkapinge kujiunga nayo.
 
Back
Top Bottom