Zitto ataka Tanzania isitishe uhusiano na nchi za Magharibi: Kisa? Libya

Nampenda sana Mbunge kijana, machachari na mahiri, Zito Kabwe. Lakini katika wazo la kusema kuwa Tanzania ivunje uhusiano na mataifa yanayoishambulia Libya ambalo Kabwe amelitoa leo Bungeni, amekosea. Kwanza ni lazima afahamu kuwa Nato pamoja na marafiki zao ndio wanaowezesha bajeti ya tanzania kwa sehemu kubwa. Plili miradi mingi ya huduma na maendeleo inapata pesa kutoka kwa washirika hao. Kwa hiyo kufuta 'diplomatic relations' na watu hao ni sawa na kuiua serikali ya CCM. Jambo hilo haliwezekani hata kidogo. Wana jamii mnasemaje katika hilo.

zitto amesema hayo kama nani?
 
Safi sana mheshimiwa ZITTO atleast sasa bungeni kuna watu wanaoweka mbele maslahi ya Afrika, haihitaji kuwa mtaalamu wa Nyuklia kuona kwamba kinachofanyika Libya ni ubeberu wa waziwazi na ni hatari kwa Uhuru wa Afrika, leo hii mijamaa ya NATO ikifanikiwa katika kampeni yao huko LIbya itaset precedent moja mbaya sana, kwa sababu yatafanya tena na tena kwa nchi nyonge.
nikinukuu maneno ya Martin Luther King , "Injustice anywhere is an injustice everywhere", Ishu ya Libya siyo Ghadafi, Ishu ya Libya ni MAFUTA, mijamaa inataka icontrol mafuta ya Libya. hata akiondoka Ghadafi akaja mwingine na kutaka mafuta ya Libya yamilikiwe na Walibya, atakiona cha moto. Ghadafi kwa sasa anapigana kulinda sovereignity ya nchi na rasilimali zake.
 
Waacheni wa Libya waamue mambo yao. Wenyewe ndo walianza kumkataa Ghadafi, NATO inawasaidia kutimiza lengoNyie shida yenu nini? Zitto ni kutaka tu aonekane kila siku anaongea. Nadhani kaanza kuishiwa hoja za maana.Suala la Libya halipaswi kutupotezea muda tuna mambo yetu ya kushughulikia mengi.
Hawa Libya si ndo walimsaidia Nduli Dikteta Idd Amin Dada
 
Zitto si malaika so usitarajie yupo perfect.

Kimsingi NATO wapo right kabsia tena tuwashukuru kwa kutusaidia kuwaongoa marais madikteta kama hawa.
Tunahitaji demokrasia kila nchi ili kila mwananchi aweze ku enjoy haki zake ndani ya nchi na si raisi wa kugawa rasilimali za nchi kwa wale wanaompenda au wasiokua against naye.

Tunataka nchi za africa ziwe huru katika dunia hii ya utandawazi ili kuwezesha biashara ku-flow kila kona bila kujali dini sura wala utaifa wa mtu kama ilivyo nchi za magharibi.....Libya ina mafuta ya kulisha africa nzima lakini je siku zote akiwa madarakani africa tumefaidi nini? au misikiti ya misaada?

Yeye hua anauzia nchi marafiki wafamilia yake na siyo nchi zinazoitaji mafuta kulingana na demand and trade distance.

LETS MARKET ALLOCATE RESOURCES ACCORDING TO DEMAND
 
Nampenda sana Mbunge kijana, machachari na mahiri, Zito Kabwe. Lakini katika wazo la kusema kuwa Tanzania ivunje uhusiano na mataifa yanayoishambulia Libya ambalo Kabwe amelitoa leo Bungeni, amekosea. Kwanza ni lazima afahamu kuwa Nato pamoja na marafiki zao ndio wanaowezesha bajeti ya tanzania kwa sehemu kubwa. Plili miradi mingi ya huduma na maendeleo inapata pesa kutoka kwa washirika hao. Kwa hiyo kufuta 'diplomatic relations' na watu hao ni sawa na kuiua serikali ya CCM. Jambo hilo haliwezekani hata kidogo. Wana jamii mnasemaje katika hilo.
Kama unampenda kanywe nae chai. Hakukua na umuhimu wa kuanzisha thread kama content zenyewe ndio hizo....yani kila atakachosema Zitto lazima mbandike, kuna siku mtakuja kuanzisha thread ya Zitto kajamba na mazuzu yatachangia
 
It seems kuna Daktari alimshauri na kumuanya Zitto kuwa siku atakapoacha kuongea vitu visivyo na Logics atapata matatizo makubwa sana kiafya na kuua ndoto zakee.
Kama anaamini katika anachokiongea kwa nini asianze yeye kukishauri Chama chake kivunje uhusiano na wa-Magharibi wale wanaokisaidia katika mambo mbali mbali?
 
Kuna maswali mengi sana najiuliza kuhusu hawa NATO, hivi ni vita ngapi zinatokea Afrika ambazo zinaleta mauaji makubwa kwa raia? Ni ngapi kati ya hizo NATO imepeleka majeshi kwenda kuwalinda raia? Kwanini Libya? Libya.. Libya... Halafu na wenyewe wanaua raia.
 
It seems kuna Daktari alimshauri na kumuanya Zitto kuwa siku atakapoacha kuongea vitu visivyo na Logics atapata matatizo makubwa sana kiafya na kuua ndoto zakee.
Kama anaamini katika anachokiongea kwa nini asianze yeye kukishauri Chama chake kivunje uhusiano na wa-Magharibi wale wanaokisaidia katika mambo mbali mbali?
Na we ni mshabiki wa posho?
 
Safi sana mheshimiwa ZITTO atleast sasa bungeni kuna watu wanaoweka mbele maslahi ya Afrika, haihitaji kuwa mtaalamu wa Nyuklia kuona kwamba kinachofanyika Libya ni ubeberu wa waziwazi na ni hatari kwa Uhuru wa Afrika, leo hii mijamaa ya NATO ikifanikiwa katika kampeni yao huko LIbya itaset precedent moja mbaya sana, kwa sababu yatafanya tena na tena kwa nchi nyonge.
nikinukuu maneno ya Martin Luther King , "Injustice anywhere is an injustice everywhere", Ishu ya Libya siyo Ghadafi, Ishu ya Libya ni MAFUTA, mijamaa inataka icontrol mafuta ya Libya. hata akiondoka Ghadafi akaja mwingine na kutaka mafuta ya Libya yamilikiwe na Walibya, atakiona cha moto. Ghadafi kwa sasa anapigana kulinda sovereignity ya nchi na rasilimali zake.

Safi mkuu, we unafikira chanya.
 
Zitto we ni mzito wa hoja. You are right thousand times. Acha kumshabikia mtu anayemchukua mkeo kisa analisha familia
 
Kabla hata ya kuitaka serikali uvunje uhusiano na nchi za magharibi, angeuliza kwanza serikali ina msimamo gani juu ya suala la Libya. Siku Chadema wakiandama na kufanyiziwa kama walivyofanyiziwa Walibya na Gadaffi, watakuwa wa kwanza kuomba msaada NATO.
 
hii ndio failure pekee tuliyonayo CHADEMA, kauli za zitto zitakuja kutughalimu sana kama hata pewa semina elekevu
maswali ya zitto yalikuwa ni mtego wa kupima uwezo wa naibu waziri,na km unafuatilia sana utagundua ni utaratibu ambao ndio unatumika sana na wapinzani hata kenya si tz tu
 
Zitto Kabwe yuko sahihi 101%. Tatizo ni mawazo tegemezi ya bajeti na ukoloni mambo leo. ZITTO MBUNGE WANGU NASHUKURU UMELISEMA HILO WATAPINGA LAKINI UKWELI UTABAKI PALEPALE
 
Zitto si malaika so usitarajie yupo perfect.

Kimsingi NATO wapo right kabsia tena tuwashukuru kwa kutusaidia kuwaongoa marais madikteta kama hawa.
Tunahitaji demokrasia kila nchi ili kila mwananchi aweze ku enjoy haki zake ndani ya nchi na si raisi wa kugawa rasilimali za nchi kwa wale wanaompenda au wasiokua against naye.

Tunataka nchi za africa ziwe huru katika dunia hii ya utandawazi ili kuwezesha biashara ku-flow kila kona bila kujali dini sura wala utaifa wa mtu kama ilivyo nchi za magharibi.....Libya ina mafuta ya kulisha africa nzima lakini je siku zote akiwa madarakani africa tumefaidi nini? au misikiti ya misaada?

Yeye hua anauzia nchi marafiki wafamilia yake na siyo nchi zinazoitaji mafuta kulingana na demand and trade distance.

LETS MARKET ALLOCATE RESOURCES ACCORDING TO DEMAND

Kama ndiyo hoja basi NATO ije ituondelee udicteta wa CCM wasioelewa shida za wananchi wanaojinufaisha na rasli mali za nchi
 
Simuonei huruma hata kidogo Ghadafi, acha achapwe. Ni huyu huyu Ghadafi aliyeungana na Idd Amin kutuawa, na kwa kumbukumbu zangu hajawahi kutuomba msamaha, ila alikuja na style ya kutujengea misikiti. Wakati mwingine neno 'sorry' ni muhimu kuliko jengo maana linaonesha kutambua baya na zuri. Na kwa issue ya kutupiga risasi wakati wa Idd Amin bado Ghadafi anatakiwa aseme sorry. Na kwa maoni yangu hela za kutujengea misikiti sio za Ghadafi, ni wananchi wa Libya, wananchi ambao leo hii wako barabani wakimtaka aachie madaraka.

Pili, alitaka kutawala Libya mpaka lini? alingia madarakani (kwa mtutu) akiwa na umri wa miaka 27 tu. na ameshakaa hapo hadi anazeeka sasa. hiyo nchi ni duka lake?
 
Huo ni mtazamo wa zitto lakini sisi watanzania tukivunja uhusiano na USA, UK , FRANCE na RUSSIA na NATO kwa ujumla tutasalimika kweli?
hii sio issue ya kupewa misaada tu hata vituko vya hao jamaa tunaweza kuviimili? Tanzania tusijifanye na sisi tuna sauti bana ukweli unabaki pale pale hata kwenye familia kunakuwa na mkubwa, hata nchi ina mkuu na dunia ni hivyo hivyo hao ni wakubwa na lazima tuwafuate la watatufundisha adabu na uwezo wanao.
wakianza kuujumu mifumo yetu ya computer, bank na ulinzi tunauwezo wakujiposha, IRAQ iko wapi na nuklia zao? tuwe na heshima na wakubwa ili tupate mkate wetu BANA sio kupiga kelele tena za mambo ambayo hata hayatuhusu,
haya ndiyo alifanya NYERERE kuikombo AFRIKA ni nani anatukumbuka kwa vita tulivyowapigania?
LEO HII waafrika kusini wanatunyosha na makapuni yao badala ya kutusaidia kama tulivyofanya wakati wa uhuru, tuliwapa ardhi lakini hata leo hukienda hapo mahali (dakawa) hakuna ujenzi wote wote kutoka afrika kusini kama shukurani
Zimbabwe walijaribu nadhani hali hali hiko wazi, sasa cha kutufanya twende huko kwa manufaa ya LIBYA ni yepi?

mimi ninaishi na walibya wao wenyewe hawamtaki Gaddafi kutoka na ufisadi wake, ZItto kwanza aeleze kama Gadaffi ni fisadi au sio fisadi sio kukurupuka tu na hoja zisizo timilika au sadikiki , RUSSIA walikuwa wanapinga hivyo vita sasa wamekuwa msitari wa mbele kumtoa Gaddafi,

kuna wanawake walibakwa kwa kumpinga Gadaffi wanajeshi wake walipewa Viagra na kuwashugulikia hao hakina mama naposema kina mama nina maana wengi sio wawili watatu na hiyo ni moja ya mashitaka yanayomkabi Gadaffi,
tusiingii kupinga mambo kwa kuangalia AL JEZEERA sometime they wrong.
vita ilipo anza walikuwa ni walibya kwa walibya Gadaffi alionywa kutotumia siraha kali zidi ya waasi lakini hakusikia, sasa yanamrudi watu wanaleta misukumo ya dini kutetetea na kukwamtazamo huu ndio maana mimi huwa naona ZITTO hafai kuwa NATIONAL leader ni mkurupukaji na mtafuta nafsi kutwaa madaraka.

hawa wanasiasa wasitubuluze na kelele zao za makopo, sasa ni wakati wa kujenga inchi yetu mbona Amerika kusini kuna nchi kibao zinamatatizo na marekani jirani tu hapo ajishughulishi nazo.
INDIA ina ikandamiza NAPEL lakini mchina yuko kimya, zimbambwe imetendwa mbaya lakini afrika kusini anaendelea na biashara zao

Hoja ya woga hiyo. Libya inasamabaratishwa machoni petu eti tunyamaze kwa kuwa NATO watatunyima misaada. NI UTMWA ULIOKITHIRI. Nipe faida moja tu ya hiyo misaada. Angalia wanavyopora rasilimali zetu na kuwapofusha viongozi wetu wasione ubaya uanaotendeka kwa rasilimali za Tanzania? NATO wamekosea kama wanavyokiri ki moyo moyo lakini maendeleo ya Libya na kusambaratika kwake ni janga la Africa.
 
Nampenda sana Mbunge kijana, machachari na mahiri, Zito Kabwe. Lakini katika wazo la kusema kuwa Tanzania ivunje uhusiano na mataifa yanayoishambulia Libya ambalo Kabwe amelitoa leo Bungeni, amekosea. Kwanza ni lazima afahamu kuwa Nato pamoja na marafiki zao ndio wanaowezesha bajeti ya tanzania kwa sehemu kubwa. Plili miradi mingi ya huduma na maendeleo inapata pesa kutoka kwa washirika hao. Kwa hiyo kufuta 'diplomatic relations' na watu hao ni sawa na kuiua serikali ya CCM. Jambo hilo haliwezekani hata kidogo. Wana jamii mnasemaje katika hilo.
Ndio maana Kambarage alitaka tujenge taifa linalojitegemea.
 
Wakati wakishirikiana na Uganda kuibomoa Tanzania, Zitto hakuona hayo? au alikuwa kijana... he should stop this kind of lower politiking
 
Zitto aelewe kuwa Safari nyingi za Nje za Kikwete anakwenda nae; kwahiyo akivunja uhusiana na nchi za Magharibi Kikwete atakwenda wapi ?
 
Back
Top Bottom