Zitto ataka hatua kali zichukuliwe dhidi ya askari polisi aliyemtishia bunduki Malima

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Katika hali isiyokuwa ya kawaida iliyotokea mapema hii leo jijini Dar es salaam kwa kitendo cha cha aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Fedha katika utawala wa awamu ya nne. Adam Malima kutishiwa bunduki na askari mmoja aliyekuwa doria kimewashangaza wengi na kupelekea Mbunge wa Kigoma Mjini, Zuberi Zitto Kabwe kuonyesha masikitiko yake hadharani kwa kitendo alichofanya askari huyo.

Zitto Kabwe ameonesha masikitiko hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii Facebook akihoji kama polisi wanafundishwa kuwafanyia hivyo raia wasiokuwa na hatia kiasi cha kuibua hofu katika jamii inayowazunguka na kupoteza imani na jeshi la polisi.
 
Back
Top Bottom