Zitto Asisubiri Kuvuliwa Uanachama; Ajiondoe Mwenyewe: Mahakama Isiingilie kazi za Chama!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Hakuna namna nyingine ya kumaliza mgogoro wa nidhamu CDM isipokuwa ama kwa uongozi wa Taifa kuwavua uanachama wale wote ambao wanaonekana kuwa ni vyanzo vya migogoro isiyokoma ndani ya chama au kwa wale ambao wanaona hawawezi kuendelea kuwa chini ya uongozi wa taifa (subordination) na wanataka kulazimisha mabadiliko kwa njia nje ya zile za Kikatiba kuamua kujiondoa wenyewe.

Katika mfululizo wangu ule wa mwisho wa mwaka jana kuhusiana na suala la nidhamu nilieleza kwa kirefu juu ya jambo hili. Mgogoro wa CDM ulipofikia sasa sioni njia yoyote nyingine isipokuwa ama watu kuvuliwa uanachama na hivyo kutokuwa na jambo lolote la kufanya kwa chama au wao wenyewe kuamua kujiondoa baada ya kuona kuwa chama hakiendi au hakikubaliani nao kiasi cha kutoweza kuaminika tena. Binafsi siamini kama mahakama itaingilia kati utendaji wa chama cha siasa na hasa haki yake ya Kikatiba kusimamia nidhamu ya wanachama wake na hasa viongozi wake. Tayari tumeshaona precedence za mahakama kuhusu suala hili huko nyuma.

Kwa maoni yangu Zitto hawezi kuendelea kuwa CDM kwa sasa na sijaona dalili za kuweza kupatana hasa baada ya matukio mbalimbali ya mwishoni mwa mwaka jana. Ametengeneza (ametengenezewa) hali ambayo inamfanya iwe vigumu kuwa chini ya viongozi wengine na yawezekana hilo haliwezi kutokea hadi yeye awe ndiyo kiongozi mkuu wa chama. Katika mfululizo wangu ule nilieleza kuwa ni lazima viongozi na wanachama wajifunze kukubali madaraka yaliyo juu yao na kutumia njia za kawaida kuleta mabadiliko hata kama itatumia muda. Kauli za ndugu yetu Zitto za mara kwa mara (kwenye mitandao na kwingine) zinaonesha pasi ya shaka kuwa hana imani na viongozi walio juu yake na hajawa tayari kukubali madaraka yao juu yake na hivyo kutengeneza kile ambacho katika makala yangu nilikiita "parallel leadership". Chama hakiwezi kuwa na sehemu mbili za uongozi - wale halali na wale ambao wanaamini wana uhalali (hata kama hawajapewa nafasi za kufanya hivyo).

CDM ichukue uamuzi wa kusimamia nidhamu katika chama na kuweka taratibu za kuhakikisha kuwa matatizo haya ya mara kwa mara ya baadhi ya viongozi wake wakuu kugongana yanatatuliwa na kuzuia mapema zaidi. Itakuwa ni kujidanganya kudhani kuwa matatizo haya yanatokea kwa bahati mbaya; ni vizuri kujiuliza kwanini yanatokea na ni kitu gani kinafanya kuwepo na potential ya migogoro ya aina hii. Kwenye mfululizo wangu nilitoa mapendekezo kadhaa na nina uhakika wapo wengine wenye mapendekezo ya tofauti. Ni lazima kisimamia nidhamu kwa sababu kama taasisi haiwezi kufanikiwa kama haisimamii nidhamu bila upendeleo, woga, husda au chuki. Kisipepese macho bali kichukue hatua thabiti za kuhakikisha kuwa viongozi wanaoonekana ni vyanzo vya migogoro wanaelewa uzito wa matendo, kauli, na fikra zao dhidi ya chama. Pendekezo langu la kwenye mfululizo kuwa Chama kitoe masharti makali kwa viongozi hawa ili waendelee na uanachama sidhani kama linaweza kukubaliwa nao; linaweza kujaribiwa lakini sioni dalili ya kukubaliwa.

Nje ya hapo viongozi kama Zitto ambao wanaamini wana wapenzi, kundi kubwa la wanachama na wanakubalika sana na wananchi kuamua kujiondoa wao wenyewe bila kusubiri kufukuzwa kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamesimamia dhamira zao zaidi. Nyerere aliwahi kusema CCM siyo mama yake na hili ni kweli kwa CDM pia. Zitto kama anaona hawezi kuwa chini ya uongozi wa sasa na hawezi kuacha kuonekana anashindana na uongozi wa chama chake ni vizuri akaamua kujivua uanachama wa CDM kwa heshima na kuendelea na siasa kwa namna nyingine. Kwa vile wapo watu wanaomfuata au kukubali fikra zake ni wazi kuwa akiingia chama kingine au hata kuanzisha kingine atakuwa na kundi la wafuasi ambao watafuata nyayo zake na yeye anaweza kuwapa ule uongozi ambao hawezi kuutoa CDM bila kuyumbishwa na "wahafidhina" wa CDM.

Ni maoni yangu kuwa njia pekee ya kumaliza mgogoro huu wa kinidhamu ni ama watu kuvuliwa uanachama au wao wenyewe kujivua uanachama. Njia nyingine ambayo sidhani kama inawezekana ni viongozi wenye mgogoro kukubali makosa na kujiweka chini ya uongozi wa juu yao bila masharti (unconditional) ili kurudisha imani. Hili la tatu sidhani kama linawezekana kirahisi.

Mahakama isiingilie migogoro hii ya kinidhamu kwani itafungua mlango mbaya sana katika siasa za Tanzania ambapo watu wanaweza kujikuta kwenye migogoro kwenye vyama vyao na badala ya kukubali madaraka yaliyo juu yao katika vyama watakimbilia mahakamani kutafuta "haki". Mwisho wa siku vyama vinaweza kujikuta vinalazimishwa kuwa na viongozi wanaotokana na mahakama. Ni pale tu ambapo kuna hoja za Kikatiba au za Haki za Binadamu na zile za Kiraia mahakama zinaweza kuangalia kwa uangalifu bila kujikuta vinaingilia maamuzi ya vyama vya siasa kujiendesha na kujisimamia.

Ni matumaini yangu mgogoro huu utaisha punde ili vyama na watu mbalimbali waanze kujipanga vizuri kuelekea chaguzi mbalimbali zinazokuja bila kujikuta zinatumia muda na raslimali nyingi kushughulikia migogoro ambayo ingeweza kumalizwa mapema zaidi kuliko ilivyo sasa.

Heri ya Mwaka Mpya!
 
Zitto tupa kule kwenye CHAMA CHAKAVU CHA MIZIGO waliomtuma kuchafua hali ya hewa CHADEMA.
 
What a great analysis!

Mzee Mwanakijiji,

Insurbodination huondoa trust katika leadership


Nakumbuka tarehe 22/1/2011 tukiwa na Mhe.Zitto ndani ya Gari yake mimi Mchange na Emmanuel Mwakajila tulijadili kuhusu matokeo ya urais 2010 na yeye kudai kuwa uchakachuaji uliofanyika ulistahili kweli mass action kutokana na sapoti kubwa ya vijana waliojitokeza kwenye Kongamano tuliloshiriki pale uwanja wa Makuburi

Nilimwambia ni kweli tungeamua kuwa radical kabisa tungeweza kuunda parallel government

Aliniunga mkono na kutoa maoni yake tulipofika pale External Ubungo kupita service road na kudai kuwa wanaoongoza msafara tena wamekosea sana kumpitisha Rais ambaye hakutangazwa upande huu maana ni hatari sana.Zitto anaweza kuja kuthibitisha hili

Sasa mentality hizi za parallel leadership ndizo zinazowa-drive

Katiba ya chama itasimama juu ya maslahi binafsi .

Leo rangi halisi zimezidi kujidhihirisha zenyewe
 
Mwanakijiji
Kila mara unaongelea nidhamu nidhamu, hivi nidhamu wewe unayoiona ni yakutofautiana kimawazo wanasiasa tu? Hivi kwa mwanyekiti kutembea na mbunge wa kuteuliwa ni nidhamu ama rushwa ya ngono?

Wenda Zitto anapingana na watovu wa nidhamu wa rushwa za ngono, na watovu wanidhamu wasio na nidhamu kwenye fedha za chama. Kwanini hao wasio nanidhamu kwenye fedha na wapokea rushwa ya ngono, huwashauri wajitoe kwenye chama?
 
Kashaingia Kingi, hawezi jiondoa lazima aondolewe hiyo haina mjadala teeeeena. Mzeemwanakijiji usiseme kwamba 'ulishasema'.
Wewe si CDM futa na kifuto na wala usirudie tena
 
Last edited by a moderator:
What a great analysis!

Mzee Mwanakijiji,

Insurbodination huondoa trust katika leadership


Nakumbuka tarehe 22/1/2011 tukiwa na Mhe.Zitto ndani ya Gari yake tulijadili kuhusu matokeo ya urais 2010 na yeye kudai kuwa uchakachuaji uliofanyika ulistahili kweli mass action kutokana na sapoti kubwa ya vijana waliojitokeza kwenye Kongamano tuliloshiriki pale uwanja wa Makuburi

Nilimwambia ni kweli tungeamua kuwa radical kabisa tungeweza kuunda parallel government

Aliniunga mkono na kutoa maoni yake tulipofika pale External Ubungo kupita service road na kudai kuwa wanaoongoza msafara tena wamekosea sana kumpitisha Rais ambaye hakutangazwa upande huu maana ni hatari sana.Zitto anaweza kuja kuthibitisha hili

Sasa mentality hizi za parallel leadership ndizo zinazowa-drive

Katiba ya chama itasimama juu ya maslahi binafsi .

Leo rangi halisi zimezidi kujidhihirisha zenyewe
Wewe toa uongo wako hapa,Zitto alishasema hajawahi kukutana na wewe,hiyo gari uliipandia wapi?kanywe gongo huko si mmehalalisha?
 
Msaliti haijawahi akajitoa maana ni kosa ktk kazi, ni mpaka afukuzwe, ana-take chances hadi dakika ya mwisho, huyo ndo msaliti, si unaona anavyotumia mahakama na sheria kucheleweshwa kuchukuliwa hatua zinazostahili, anapata support kutoka kwa wafadhili wake
 
ndio nazidi kufahamu upeo wako wa uzee unaokupelekesha. Haki ya mahakama ni paramount katika democratic society. Chama tunachokitegemea kuongoza nchi hii leo kiwe immune kutoka mikono ya mahakama halafu tupige makofi? Kwani kuna siri gani hasa asijadiliwe na baraza kuu? woga wa nini? Nidhamu iendane na haki, sio nidhamu na ukandamizaji. naamini katika misingi imara ya mahakama isioyumba, unapohisi unadhulumiwa mahakama ndio sehemu kuu ya kupata haki yako. Amka mzee, kweli ujamaa ni chanzo cha kulemaa kwa muamko wa akili..
 
Mwanakijiji
Kila mara unaongelea nidhamu nidhamu, hivi nidhamu wewe unayoiona ni yakutofautiana kimawazo wanasiasa tu? Hivi kwa mwanyekiti kutembea na mbunge wa kuteuliwa ni nidhamu ama rushwa ya ngono?

Wenda Zitto anapingana na watovu wa nidhamu wa rushwa za ngono, na watovu wanidhamu wasio na nidhamu kwenye fedha za chama. Kwanini hao wasio nanidhamu kwenye fedha na wapokea rushwa ya ngono, huwashauri wajitoe kwenye chama?

CDM ngazi ya juu ina uwezo mdogo wa kutatua matatizo. Kama ni nidhamu basi iwe kwa kila mtu.
 
Mwanakijiji umenena Watu wote wanajua mwisho wa siku mahakama haitafanyia maamuzi vyama.zitto kawarahisishia kazi viongozi wake
no more mshipa wa aibu

Unaweza kujiuliza ni kwa nini Kafulila alikipitia kikombe hiki? ni nani alimuhamasisha? ..... ni nani alimwambia Kafulila ni yeye pekee anaweza kuwa Mwenyekiti NCCR? Hawa jamaaa history itaandika, ni jambo tu la muda.....
 
Kila mtu ana haki ya kutafuta haki mahakamani kwa vyovyoye vile kama anaona ameonewa.

ila namshangaa sana Zitto kufanya hivi kwani nasikia walijiuzuru kwenye cc ya mwisho, sijui kwanini bado anang'ang'ania madaraka tena ambayo hayafanyii kazi, alikuwa kama kivuli tu. Au ni kutaka kuichafua Chadema tu.
 
Back
Top Bottom