Zitto Asisubiri Kuvuliwa Uanachama; Ajiondoe Mwenyewe: Mahakama Isiingilie kazi za Chama!

Nimewahi kusema na nitasema tena

Uongozi ni KAZI NGUMU SANA.

Lakini yule mwenye hekima atafikia hatima.

Pande zote hapa zilihitaji hekima zaidi kuliko nguvu, tusingefika hapa!

Lakini kwakua tumefikia hatua hii, namna pekee ni kundi moja kulishinda kabisa kundi jingine.

Ungeniuliza mimi, ningekuambia Utaratibu sahihi ukifuatwa, Zitto atakosa haki(Moral right) ya kuendelea "kupigania" uanachama wake. Anapata hiyo Moral Right yakuendelea kupambana kwakuwa tu CHADEMA imeendelea kukosea taratibu za kumuondoa nakuonyesha mashaka katika dhana ya haki katika utaratibu unaotumika.

Zitto hana ubavu wakupambana na chadema, hakuna mtu aliyenao!

Anaweza kuondolewa CHADEMA bila yeye kung'ang'ana kabisa, kwakua hatakua na HAKI hatakidogo kama taratibu sahihi ziki tumika kumuondoa.

Naomba kusisitiza tena hapa umuhimu wakuonyesha ushahidi unaomtia hatiani kwa tuhuma zake nakutoa nafasi kwa maamuzi kufanywa na vyombo sahihi tu, na kwa wakati sahihi ili kuonyesha kutendeka kwa haki. Na kama HAKUNA USHAHIDI WOWOTE THABITI juu ya USALITI wake adhabu ya kumvua uanachama Sihaki. Kama UPO uwekwe wazi, utaratibu ufuatwe aondolewe!

Utaratibu SAHIHI na wa HAKI ufuatwe iliwote waone HAKI IKITENDEKA!

Zitto hatakua na sababu wala nguvu ya kuendelea kupambana.

Comrades.
Nawashukuru
 
Aje hapa aseme hayo maana kwa wanasiasa kama wassira anayekana hadi watoto wao unatarajia nini.Hebu waulize akina Mwampamba juu ya hili.Ni aibu kwa watu wanaojiita viongozi kuwa waongo kupindukia

Ni kama uongo wa leo asubuhi kupitia Channel 10 kudai kuwa yupo tayari kupokea uamuzi wowote wa Kamati Kuu lakini jioni hii yupo mahakamani kupinga kujadiliwa

Compulsive lier!

Mkuu Ben, Nadhani bado tunanafasi, uchambuzi huu murua wa Mwanakijiji uwafikie wajumbe wote wa KK... Zitto lazima atimuliwe na iwe fundisho kwa wasaliti wote! Yawezekana sisi wengine tayari tumeshachelewa kufaidi matunda ya nchi yetu, Basi tuwarithishe watoto na vijukuu vyetu Tanzania yenye Neema inayolingana na Utajiri ambao Mwenyeezi Mungu ametujaalia... Change in X / Change in Y = Mzee Mwanakijiji...
 
Aje hapa aseme hayo maana kwa wanasiasa kama wassira anayekana hadi watoto wao unatarajia nini.Hebu waulize akina Mwampamba juu ya hili.Ni aibu kwa watu wanaojiita viongozi kuwa waongo kupindukia

Ni kama uongo wa leo asubuhi kupitia Channel 10 kudai kuwa yupo tayari kupokea uamuzi wowote wa Kamati Kuu lakini jioni hii yupo mahakamani kupinga kujadiliwa

Compulsive lier!

6.3.6 Mamlaka za Nidhamu na Uwajibishaji
(a) Kiongozi aliyechaguliwa na Mkutano Mkuu ataweza kusimamishwa uongozi tu
kama ifuatavyo:-
(i) Kiongozi ngazi ya Msingi na Kamati Tendaji ya Tawi
(ii) Kiongozi wa Tawi na Kamati ya Utendaji ya Kata/Wadi
(iii) Kiongozi wa Kata/Wadi na Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya.
(iv) Kiongozi wa Jimbo/Wilaya na Baraza la Mkoa
(v) Kiongozi wa Mkoa na Kamati Kuu.
(vi) Kiongozi wa Taifa na Baraza Kuu.
(b) Kiongozi aliyeteuliwa na vikao vya uongozi ataweza kusimamishwa au kuachishwa
uongozi na kikao kilichomteua.
(c) Bila kuathiri masharti ya vipengele (a) na (b) hapa juu, kiongozi yeyote anaweza
kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa au kuachishwa
uongozi na kikao cha juu ya ngazi yake ya uongozi.
(d) Kiongozi aliyechukuliwa hatua za nidhamu na mamlaka yake ya nidhamu anayo haki
ya kukata rufaa ngazi ya juu ya ile ya mamlaka yake ya nidhamu na uamuzi wa ngazi
hiyo utakuwa wa mwisho.
(e) Rufaa yoyote lazima ifanyike katika muda wa siku thelathini tangu tarehe ya
kupokea rasmi kwa maandishi maamuzi ya mamlaka iliyotoa adhabu.
(f) Viongozi wa ngazi ya kitaifa waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wanaweza
kusimamishwa uongozi endapo theluthi mbili ya wajumbe wa Baraza Kuu watapiga
kura ya siri na kutokuwa na imani na kiongozi mhusika. Baraza Kuu litakuwa na
wajibu wa kuteua atakayeshika nafasi hiyo kwa muda hadi uamuzi wa mwisho
kufanywa na Mkutano Mkuu.
 
Tatizo la zitto ni kutokuwa na knowledge ya collective responsibility ndani ya chama na wenzake! Hili litamgharimu popote aendapo kwenye vyama!
 
Aje hapa aseme hayo maana kwa wanasiasa kama wassira anayekana hadi watoto wao unatarajia nini.Hebu waulize akina Mwampamba juu ya hili.Ni aibu kwa watu wanaojiita viongozi kuwa waongo kupindukia

Ni kama uongo wa leo asubuhi kupitia Channel 10 kudai kuwa yupo tayari kupokea uamuzi wowote wa Kamati Kuu lakini jioni hii yupo mahakamani kupinga kujadiliwa

Compulsive lier!

Chapa nyundo kamanda. Mwongo ni msaliti tuuu
 
Mzee Mwanakijiji

Niliwahi kusafiri kwenda Kigoma, usafiri wetu ulikuwa ni wa treni kutoka Dar, njia nzima mijadala ilikuwa mingi, hapo ndipo niliwajua ndugu zangu Wahaa... jamaaa hawapendi kushindwa mjadala, tangu pale niliwajua hawa watani zangu

Tanzama Kafulila....., Tazama Kabouru, Tazama............,

Wasiwasi wangu, Hebu kuna siku hawa watani zangu watapata Rais toka Kigoma? 2020 - 2025 ni Lazima Zitto angeukwaa, Mtani wangu kawaongezea Mzigo mzito watu wa kigoma, Maskini jamii itawahukumu kwamba ni wasaliti kumbe siyo si kwenye ajira hata ujiranini.

Mzee Mwanakijiji, sijui nini kifanyike hapa hii jamii ya Kihaa iendelee kuaminiwa na watanzania wenzao kwenye fursa za kiutawala.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu sikio la kufa halisikii dawa. Jemedari Zitto amejiaminisha kwa plant followers wanaomjaza ujinga kuwa bila yeye CDM haitasonga.Inavyoaminika kwa sasa amekimbiwa na washauri wake wa mwanzo hivyo anajiongoza mwenyewe kwa sasa kupitia ALBERTOMSANDO .
 
Huyu Msaliti hana namna nyingine zaidi ya kufukuzwa kama Nguchiro..!
 
ZZK aliapa atakua wa mwisho kuondoka CDM,
Pia akasema "hii ni vita kati ya wahafidhina na wapenda demokrasia"
Tatizo lenu mnaangalia upande mmoja tu wa zzk,mbowe na slaa mapungufu yao yanamezewa,We cannot solve problems in a such situation ndo kwanza tutazidi kupandikiza mbegu ya kukipeleka chama jehanamu

Mkuu Mwekundu, jaribu kuwa neutral kidogo na rejea makala za Mwanakijiji za hivi karibuni kuhusu matatizo ya viongozi wote wa Chadema wakiwemo hao Slaa, Mbowe etc ambao wewe unasema huwa wanamezewa. Viongozi wote wa Chadema mapungufu yao yamejadiliwa na Mzee Mwanakijiji. Tatizo la Zitto ni approach yake ya kutaka kubomoa chama kizima kwasababu tu anaamini kuwa Mbowe na Slaa hawafai kuwa viongozi wa Chadema. Angeweza kutumia njia inayojenga badala ya approach yake hii ya sasa ya kuibomoa Chadema nzima. Mfano, kwenda kufanya mkutano Kigoma muda mfupi tu baada ya bosi wake kupita huku akijua kwamba hilo lina madhara kwa image ya chama maana yake nini? Kwanini, kwa mfano, asiunganishe ziara yake binafsi na ile ya chama kujenga umoja ndani ya chama na kuokoa garama zisizo na msingi ? What was he trying to accomplish? He definitely doesn't care about his party, all he cares for is his own power? Hiyo ndo demokrasia mkuu? Hata kama ana haki hana budi kutatua mgogoro wake kwa njia ambao haikibomoi chama.
 
MM
Katika ushauri ulioutoa kuna sehemu mbili ninazoziangalia kwa undani kabisa.

Suala la ZZK kuwa chini ya uongozi uliopo halipo, kama atasema itakuwa ni uongo, moyoni hakubaliani.

Pili, suala la ZZK kujivua uanachama ni gumu kwasababu ZZK ametumia Platform ya CDM kujijengea umaarufu na ame invest kwa muda mrefu.

ZZK anajua ubunge ataupata akiamua akiondoka CDM lakini ile political fame haitakuwepo haatakuwa na platform kubwa tena.

Pamoja na kuondoka na wapenzi na wanachama, ZZK anafahamu kuwa hiyo ni temporary solution kwasababu with time watamwacha peke yake isipokuwa Zittoism ambao humuani kwa chochote.

Anachopigania sasa hivi si masilahi ya CDM ni masilahi binafsi.
ZZK ameshapoteza imani kwa wenzake na si viongozi tu, kufanya naye kazi itakuwa ngumu. Sijui nani atamwamini tena hata kama atatubu malaika wakiwa pembeni wanamshangilia.

Uwepo wake ndani ya CDM hautakuwa na impact kwasababu atakuwa nguvu ya kutenganisha badala ya kuunganisha wanachama. Kundi la Zittoism halitakaa kimya lazima litatafuta sababu za kuhakikisha kuwa ima uongozi uliopo unaondolewa au mwaga mboga nimwage ugali.

Hakuna uwezekano tena wa ZZK kutumia njia za kidemokrasia na taratibu zilizopo kuleta mabadiliko yanayokusudiwa. Historia inamtia hatiani kabla ya kusomewa shtaka lingine litakalokuja awe na haki au la.

Hivyo ZZK ana option moja tu, nayo ni kutumia kila mbinu kuhakikisha kuwa anabaki kuwa mbunge kwa miaka 2 iliyobaki. Hana tena fikra za CDM au masilahi yoyote.
Ndio hizi harakati za mahakamani, vyombo vya habari, mikutano ya kurudi nyumbani n.k.

CDM wana options zifuatazo
1. Kumsamehe waendelee kuishi naye kama walivyofanya kwa masakata yaliyopita
2. Kumtimua ili apate nafasi ya kuondoka na zittoism
3. Kumwacha ZZK na kuifanya CDM itumie sheria za mwituni ambako nidhamu haina nafasi
4. Kumpisha ZZK katika nafasi ya uongozi wa chama ili kuleta 'muafaka' na kuzuaia zittoism wasiondoke


 
What a great analysis!

Mzee Mwanakijiji,

Insurbodination huondoa trust katika leadership


Nakumbuka tarehe 22/1/2011 tukiwa na Mhe.Zitto ndani ya Gari yake mimi Mchange na Emmanuel Mwakajila tulijadili kuhusu matokeo ya urais 2010 na yeye kudai kuwa uchakachuaji uliofanyika ulistahili kweli mass action kutokana na sapoti kubwa ya vijana waliojitokeza kwenye Kongamano tuliloshiriki pale uwanja wa Makuburi

Nilimwambia ni kweli tungeamua kuwa radical kabisa tungeweza kuunda parallel government

Aliniunga mkono na kutoa maoni yake tulipofika pale External Ubungo kupita service road na kudai kuwa wanaoongoza msafara tena wamekosea sana kumpitisha Rais ambaye hakutangazwa upande huu maana ni hatari sana.Zitto anaweza kuja kuthibitisha hili

Sasa mentality hizi za parallel leadership ndizo zinazowa-drive

Katiba ya chama itasimama juu ya maslahi binafsi .

Leo rangi halisi zimezidi kujidhihirisha zenyewe
Ben, Zitto si alisema hajawahi kukufahamu au kukutana na wewe?
Mimi nilishafanya uchunguzi wangu na hitimisho langu ni kuwa Zitto lacks basic skills of an intelligent leader or politician. He's a wrong chap at a right time & place. CHADEMA ilimjenga na kumfanya awe alivyowahi kuwa lakini kwa vile kiburi ni sifa mama ya wapumbavu basi umaarufu ukawa tanzi kwake.
 
Kuna usemi ambao siyo mzuri sana kwamba WAHA ni wabishi na hata sasa ukimtafuta mmoja mnawea kufika asubuhi hamjakubaliana KamA huu ni mwaka 2014 AD au hapana.Unapozidi kuwa na ubishi unausababisa pande mwingine ujitahidi kujenga hoja makini zaid na mzunguko wa hoja dhidi ya hoj unakuwa mrefu-iteration-ZZK anajaribu hilo lakini vyovyote anajua kuwa kisiasa ameshafika mwisho tena mwisho ambao siyo mzuri.CCM na mfumo utamtumia na ataachwa kama YUDA ISKARIOTE alivyoachwa a WAYAHUDI akaishia kujinyonga. CDM mkimwachia ZZK awe nanyi kama kiongozi mmekwisha,mageuzi yataingiwa na VIRUSI FANYENI UAMUZI MGUMU,MSIMVUE UANACHAMA KWA SASA,MJENGEENI NJIA YA KUTOKA AKIIONA ATOKE ASIPOIONA 2015 MSUKUMIENI MITAANI AKAWE MGOMBEA BINAFSI!
 
Kwamazingira na kimkakati Zitto amefeli, ndio, amefeli kujitoa, amefeli kupata anachokiita haki yake, amefeli kwa kila kitu,

Sasa ameiacha cc ishike mpini na yeye kashika makali,

Mahakama haina uwezo wa kuingilia utendaji kazi wa chama au taasisi yote iliyopo kisheria, bali kuangalia tu kama katiba ilifuatwa,
 
What a great analysis!

Mzee Mwanakijiji,

Insurbodination huondoa trust katika leadership


Nakumbuka tarehe 22/1/2011 tukiwa na Mhe.Zitto ndani ya Gari yake mimi Mchange na Emmanuel Mwakajila tulijadili kuhusu matokeo ya urais 2010 na yeye kudai kuwa uchakachuaji uliofanyika ulistahili kweli mass action kutokana na sapoti kubwa ya vijana waliojitokeza kwenye Kongamano tuliloshiriki pale uwanja wa Makuburi

Nilimwambia ni kweli tungeamua kuwa radical kabisa tungeweza kuunda parallel government

Aliniunga mkono na kutoa maoni yake tulipofika pale External Ubungo kupita service road na kudai kuwa wanaoongoza msafara tena wamekosea sana kumpitisha Rais ambaye hakutangazwa upande huu maana ni hatari sana.Zitto anaweza kuja kuthibitisha hili

Sasa mentality hizi za parallel leadership ndizo zinazowa-drive

Katiba ya chama itasimama juu ya maslahi binafsi .

Leo rangi halisi zimezidi kujidhihirisha zenyewe
Ben, Zitto si alisema hajawahi kukufahamu au kukutana na wewe?

Well, mimi nilishafanya uchunguzi wangu na hitimisho langu ni kuwa Zitto lacks basic skills of an intelligent leader or politician.

Certainly he's a wrong chap at a right time & place. CHADEMA ilimjenga na kumfanya awe alivyowahi kuwa lakini kwa vile kiburi ni sifa mama ya wapumbavu basi umaarufu ukawa tanzi kwake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom