Kwa mfano, baadhi ya Zittoism wanaamini kwa dhati kabisa huyu ni mtu wa kusimamia masilahi ya taifa, well amefanya hivyo lakini leo wanajua kuwa alishawahi kutulizwa na Barrick Gold.
Nani alijua hayo?
Umeandika kwa ghadhabu kweli kweli.Tunapochangia mambo ya msingi tujaribu kuweka pembeni mahaba,kama kinachoangaliwa ni nidhamu basi tuangalie kwa ngazi zote,uchafu wa viongozi wa juu pia usemwe bila kupepesa maneno kwani hamuonikuwa mboe ni mchafu au ndo nahaba!
Nakumbuka sana ndio maana nimelisema sana hili. Kwanza, katika uzi ZZK alikana kuhusika na hilo jambo.Nguruvi3,
Mjadala wa Barrick uliwahi kuibuka hapa JF, zamani kidogo na watu walitaka kujua ilikuwaje kampuni inayochimba madini, Mara, Shinyanya, au Kagera inaenda kufanya shughuli za kijamii Kigoma ili hali jamii zinazozungukwa na mashimo wanabaki kuwa watazamaji? Kwa mtindo ule wa 'simfahamu mtu huyu' Zitto akasema waliopekea msaada ni Halmshauri?
Hili la 'hata Mbowe kapewa hela' linaacha maswali. Zitto, akiwa kama naibu katibu mkuu alijua lini kuwa Mbowe kapewa pesa na mtu Mkono? Alifanya nini kama kiongozi? Kama hakukutwa na hii kadhia bado angeendelea kukaa kimya? Hii inatoa picha gani juu leadership style yake?
Nakumbuka sana ndio maana nimelisema sana hili. Kwanza, katika uzi ZZK alikana kuhusika na hilo jambo.
Baada ya evidence kuonyeshwa kuwa amejengewa shule na Barrick akarudi kwa style ya Halmashauri. Baada ya kumbana vema akatokea mkuu mmoja na kusema 'jamani ZZK ni binadamu' naye hufanya makosa na kwamba umasikini wa nchi yetu ulimsukuma hata kusahau maadili''. Mmoja wa watetezi wake ni mshiriki waraka.
Barrick walikata mbuga na kuacha mashimo na halmashauri zingine hadi jimboni kwa ZZK. Hilo lilitosha kabisa kumshtua.
Yeye akasema hawajui Barrick wala walipo kwa style ya simjui Ben wala siujui waraka, leteni ushahidi. Eti tunatakiwa tulete picha ya ZZK na Ben pamoja hata kama Ben amesema wanafahamiana.Kwamba katibu mkuu msaidizi hamjui mgombea uongozi wa BAVICHA? Real!
Wapambe wapo bize wakitaka ushahidi wa kuhusika na waraka.
Tumewaeleza kuwa kwani waraka uliandikwa lini? Hawana jibu wanataka karatasi inayoonyesha ZZK akisaini kukubali waraka.
Wengine tunajua kwasababu tunaangalia mazingira kwa ujumla hatusubiri karatasi ya ushahidi kuwa ZZK ameandika waraka.